Ni kweli umaarufu wa marehemu Kanumba ulikuwa ni zaidi ya Diamond Platnumz?

Ni kweli umaarufu wa marehemu Kanumba ulikuwa ni zaidi ya Diamond Platnumz?

Eti malegend, Ni kweli umaarufu na mvuto wa kukubalika wa Kanumba enzi za uhai wake huwezi linganisha na umaarufu wa Diamond, je ni kweli Kanumba alikuwa akikubalika sana na angekuwepo mpaka leo chibu tusonge msikia?
Kila enzi na kitabu chake. Ni kweli kuwa Kanumba ndiye msanii wa kwanza Tanzania kutambuliwa Nigeria, Afrika ya Kusini na Holywood Marekani, ilikuwa apewe role ya movie fulani ya Holywood lakini akafariki kabla hajaanza kazi. Hata hivyo hiyo ni zaid ya miaka 15 iliyopita, hiwezi kujua leo mambo yangekuwaje
 
Kanumba sana sana umaarufu wake ulikuwa ni kwa hizi nchi zinazoizunguka Tanzania, Diamond kavuka hapo ndio tofauti
Kacheza movie na ramsey noah akiwa kwenye peak na kipindi anafiriki omotola jalade alituma pole ya rambirambi that's means alikua anajulikana Nigeria.

Kwenye mashindano ya big brother yanayofanyika afrika kusini alishasahi kualikwa kwenye uzinduzi.
 
Mpaka anakufa kanumba alikua ndio maarufu zaidi kwenye sekta ya sanaa, yaani mziki na maigizo ukichanganya kwa pamoja.

Ukilinganisha umaarufu aliokua nao kanumba wakati anakufa na umaarufu wa diamond wa sasa nafikiri diamond yupo juu kidogo, mitandao imechangia pakubwa sana.

Kama kanumba angekuwepo hai mpaka leo hii kiumaarufu angekua mbali sana zaidi ya diamond. Kabla hajafa alipata dili hollywood na iyo ni miaka takribani 15 hivi iliyopita
 
Eti malegend, Ni kweli umaarufu na mvuto wa kukubalika wa Kanumba enzi za uhai wake huwezi linganisha na umaarufu wa Diamond, je ni kweli Kanumba alikuwa akikubalika sana na angekuwepo mpaka leo chibu tusonge msikia?
Kama kipindi kanumba anaaza kuigiza ulikuwa unamuona mpka kifo chake na pia Diamond unamuona huwezi kuuliza hilo swali. Mpka Sasa hivi hakuna msanii wala mwanamichezo au mtu yoyote wa burudani anayemzidi umaaruf wa kidunia Diamond. Si Mzee Jangara Wala Majuto, Wala Kingwendu. Yaani kinumaaru Diamond anasoma level za wanasiasa kwa hapa bongo
 
Humu leo ndio utajua kuna watu either watoto au basi vichwa vyao vinawaka moto .....

kanumba yupo hai muziki na bongo movies zilikuwa mbingi na ardhi,msiba wa kanumba 2012 niko form 2 azaboy mond alienda msibani halafu watu hawana time nae.

Kanumba alikuwa anapata deals za kutosha hapa tz kama ile ya star times diamond bado anahangaika na wema ambaye wema ndio kachangia kumleta mjini diamond lakini wema huyo huyo kaletwa mjini na kanumba

Acheni kabisa imagibe jamaa alikufa na 28yrs huu umri kwa aliyoyafanya inabid apewe heshima yake.....
 
Back
Top Bottom