Makanyaga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2007
- 11,129
- 7,321
Walijenga kwa miaka 20 lile Pramidi kubwa pale Giza lanye tofali zaidi ya million 2Hao watu wa zamani kweli walikuwa na ujuzi na uwezo mkubwa sana
Na ujenzi wa miji mingi sana duniani wamejenga kwa muda mrefu sana
Ukiangalia hata Inca Empire na huko Machu Pichu walivyojenga ni maajabu sana
Unajua watu wa zamani walikuwa na subra sana yaani wanaweza kujenga kitu kwa miaka hata Hamsini
Sasa sisi leo jengo linajengwa kwa miezi tu
Wao walijenga to last
Leo tunashuhudia majengo ya miaka na miaka na bado yana thamani na mazuri pia
Nilienda mji mmoja Uingereza kuna kanisa moja Gloucester lina miaka 1000 nilishangaa sana
Sasa fikiria lilijengwa kwa mda gani hilo ili likae miaka yote hii
Nafikiri na hawa watu labda walijenga pyramids kwa miaka mingi sana na sio mda mchache