Ni kweli Wastara anatudanganya kuwa yupo hospitalini India?

Siku ya February 10, 2018 imetolewa taarifa na Masoud Kaftany ambaye ni Afisa Habari, Uenezi , Mahusiano katika chama cha Waigizaji Kinondoni, kuhusu Muigizaji Wastara Juma taarifa hiyo inasema Wastara ameshafanyiwa Vipimo (Operation ) na anaendelea kupatiwa Matibabu.

Muigizaji Wastara ambaye yupo katika Hospitali ya Saifee (Mumbai ) Nchini India anaendelea vizuri na siku hiyo ya jana alitembelewa hospitalini na Muigizaji wa Bongomovie REGINA KAOLE ambaye yupo Mumbai nchini India kwa shughuli zake za kikazi.

Wanatasnia na wadau wa filam nchini wanaombwa kuzidi kumuombea Muigizaji huyo Wastara ili apone Haraka na kurejea nchini salama.

Chanzo: Millard Ayo.

HEBU TUANZE NA HIYO LOGO HAPO ILI TUJUE NI YA KAMPUNI GANI...
JE NI LOGO YA HOSPITAL..??, HOTELI..?? AU KAMPUNI INAYOTENGENEZA NGUO BAADA YA HAPO TUENDELEE NA MJADALA...

NILIOMBA KUTAFUTA HIYO LOGO NI YA NINI ILI TUWE NA UHAKIKA JUU YA KILE KINACHOJADILIWA NA KUEPUKA KUMZUSHIA BINADAMU MWENZETU UONGO... WACHA PICHA ZIJIELEZE

Kuna baadhi ya dawa huwa zinakuwa injected kwenye artery so huo uelekeo wa cannula ni uelekeo wa arteries! Hii msimhukum moja kwa moja kuwa uelekeo wa cannula umeenda upande tofauti!

Kweli kabisa kama ni hivyo mungu amsamehe maana ni bora uombe msaada kwa njia nyingine sio kwa kuomba ugonjwa maana kinywa kinaumba na ukiomba kuumwa utaumwa je akiumwa kweli ataombaje huu msaada mungu amsamehe kweli kiongozi

Sent from my 5023F using JamiiForums mobile app

Labda yeye kufuta picha alizokuw kapost n kutokujiamin ama ana sababu kwa nn kafuta! Lakin uelekeo wa cannula hauna mashiko kikubwa tu ni aina gani ya dawa alikuwa kaandikiwa na iingie kwenye mshipa upi! Hizo pocha zingine ni uelekeo wa veins ambao dawa na drip nyingi huingia na huo uelekeo wa cannula yake ni uelekeo wa arteries ambako ni dawa chache sana huwez kuagizwa uchomwe!

Nadhani tupate ukweli wa tatizo la Wastara kabla hatujashadidia. Mkuu wa nchi hawezi kuamka tu na kupeleka msaada kwa jambo ambalo hajathibitisgiwa na intelijensia kuhusu uhalisia wake. Kama ni uwongo umefanywa, basi wote waliohusika kumdanganya Mtukufu Rais ikiwa pamoja na wapeleka misaada kwa mapicha ya mitandaoni nao wahusike.

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app

Usishangae sana. Hiki ndicho kiwango cha akili zetu wabongo. Yaani wanaanza kutetea eti inawezekana hospitali anapotibiwa ndio walikosea, hawajui jinsi ya kuweka canula. Yaani with all the help hadi kutoka kwa Rais, aende uchochoroni kutibiwa mahali ambapo hawajui jinsi sahihi ya ku-inject dawa?

Anaweza sana tu. Sometimes anakuwa na frustrations zake (alisema mwenyewe). Kwa hiyo si jambo la kushangaza sometimes akiwa na excitements za ajabu...

issue sio kuzingua ila tumuulize wastara hii tiba anapata wapi? hii ndio itakuwa pivot yetu ya kuendelea na huu mjadala otherwise tunamuonea
Kwani alipopost alisema yuko wapi? Kama hakusema, basi hakutaka tujue, na nina hakika hatatuambia.

Alafu sijui kinatokea nini... Kila mtu saivi amekuwa na tabia hizo.. Si msomi wala wafoo..

Nafikiri njaa imekuwa kali mtaani.
Kabisa mkuu, tunaombeana mabaya tu.

Ukiona mwenzetu ananyanyuka hata kiuchumi au mafanikio yanamjia tunaanza kumjungua

Mengine muwe mnaelewa tu;
Hivi kweli mguu huna akili itakuwa sawa kweli?

Hizo sindano hazina drip bado;
ni kama yuko kwenye maandalizi ya kuwekewa drip;

All in all tujuwe tu kuwa anaumwa;
hata kama kaenda kwa witch doctor siye
hayatusumbui sana;

Mamndeni salamu kwako.
Sikuwahi kufuatilia ishu za ugonjwa wa Wastara.
Ila kuna kitu hakiko sawa mahali fulani.
Ni kwa nini picha aliyoweka kaifuta baada ya watu kuhoji usahihi wa uwekaji wa hiyo canula??
Kuna kitu hakiko sawa mahali.

[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13]

Sent from my SM-G850A using JamiiForums mobile app

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…