Ni lafudhi gani unaipenda katika makabila ya Tanzania?

Ni lafudhi gani unaipenda katika makabila ya Tanzania?

Napenda lafudhi za pwani,wachaga,wanyaturu.

Kisukuma huwa kinakandamizwa Sana kwa hiyo hata mtu akibembeleza ni kama anakomand.Nakumbuka kipindi nimeenda adv.Mwanza nilikua nawashangaa Sana kwanini wanakandamiza maneno.Baadae niliwazoea.
 
Suala la lafudhi hatuna mpinzani mpaka watu wa Arusha na kilimanjaro wanatuchukia , mpaka matusi yaani , kwa Tanga sisi wagosi hatuna lafudhi nzuri , kwanza hata kuongea taratibu ni mtihani ; kelele tu na kutumia nguvu kutamka maneno.
Siku mchokoze Angel Nylon mpaka ashushe povu kitu ambacho ni kigumu sana sababu ni mkimya sana, lafudhi na lahaja zake vile anavykizungusha na kiswahili chake ni burudani sana kumsikiliza...
 
Siku mchokoze Angel Nylon mpaka ashushe povu kitu ambacho ni kigumu sana sababu ni mkimya sana, lafudhi na lahaja zake vile anavykizungusha na kiswahili chake ni burudani sana kumsikiliza...
Watu wa Arusha na kilimanjaro , ukiwaambia watu wa Tanga wana lafudhi nzuri wanachukia ,tena hata ugomvi . Wanachukia sana na matusi juu .
 
Inategemea na maongezi, ya KITANDANI, OFISINI, UBISHANI, UGOMVI etc...

Mchaga anaposema YESU NA MARRIA🤣😂
wadada wa tanga, wale wa mombasa wanapozungumza wananivuruga akili kabisa..
Mwaka fulani nasoma pale DIT, Ilikuwa usiku lazima nikale mgahawa fulani pale kariakoo, tahmeed ile inashusha pale watu toka mombasa, vile wale wadada nikisikia wanazungumza, roho yangu inakuwa kwatu kabisa,

Mpogoro,mmakonde,mhehe, mnyakyusa akiongea mie huwa najisikia kucheka tu, na mhehe kwa mbaali..
Wazanzibar nao sauti lafudhi za dada zao zinavutia.
Wapemba wanakaza sana, na kuna maneno yao ni ya kipekee

Waha wao ni fujo tu, kelele mtinfo mmoja hata kama wanaongea stori za kawaida.
Wahaya ni lafudhi ya majivuno tu
Wasukuma/wanyamwezi lafudhi ya kiume na ushamba humo humo..
Wakurya, lafudhi ya ugomvi ugomvi tu
 
Back
Top Bottom