Ni lini CHADEMA wataacha kutegemea hisia na huruma za wananchi kushinda uchaguzi badala ya hoja, mipango na mikakati ya maendeleo kwa Watanzania

Ni lini CHADEMA wataacha kutegemea hisia na huruma za wananchi kushinda uchaguzi badala ya hoja, mipango na mikakati ya maendeleo kwa Watanzania

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Ni muda mrefu sasa tangu chama hiki cha kisiasa kimekua ni taasisi iliyokosa uelekeo na kupoteza malengo na misingi ya kuanzishwa kwake, na kuamua sasa kutegemea sana propaganda za hisia kali zenye kutia huruma kwa wananchi ili kuleta taharuki, kuwavutia na kuwahadaa wananchi kanakwamba chadema ni kikundi cha kidini chenye huruma sana kwa waTanzania na kwahivyo kipewe ridhaa na nafasi mbalimbali za uongozi wa kisiasa hususan katika chaguzi mbalimbali.

Sasa je ni lini chama hiki kikongwe kitaacha ulaghai huu kwa wananchi na kurejea katika misingi halisi ya kisiasa za ushindani, wa mawazo mapya, fikra mbadala, hoja za maendeleo, mipango, na mikakati yenye uelekeo wa kuleta maendeleo, kuchochea mageuzi na kubadili maisha ya wananchi kiuchumi, kisiasa na kijamii? :NoGodNo:

Mungu Ibariki Tanzania
 
ni kama umekosea chama badala ya CCM umeweka CHADEMA

Jobtruetrue/kiaaaaazi kweli kweli
 
Back
Top Bottom