PostGE2025 Ni lini Rais Samia atazunguka nchi nzima kuwashukuru wananchi kwa kumpa kura za kishindo?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,843
Reaction score
29,350
Miaka yote tumezoea kuona Rais anayeshinda kiti cha urais akizunguka nchi nzima kuwashukuru wananchi kwa kumpigia kura za ushindi. Safari hii, licha ya Rais Samia kushinda kwa kishindo (98%) na kujinyakulia karibu viti vyote vya ubunge, amekuwa mzito sana kuwazungukia wananchi na kuwashukuru kwa kujitokeza kwa wingi (zaidi ya milioni 31) kumpigia kura. Anaona aibu gani kuja kutushukuru wananchi tuliompa kura za kutosha na kumuwezesha kutetea kiti chake cha uais?

Inashangaza mgombea anashinda kwa kishindo lakini anaogopa kwenda kuwashukuru wapigakura waliompa ushindi. Kuna tatizo gani na ni nini kinachosababisha Rais ashindwe kufanya mikutano nchi nzima kuwashukuru wananchi na kuwapa matumaini kuwa ahadi zake atazitekeleza 100%?

Wagombea waliopata kura chache wamethubutu kuwashukuru wananchi kwa hicho kidogo walichoambulia lakini aliyekula pakubwa bado amejificha kwenye handaki hataki kuonekana hadharani mbele za wananchi! Haya ni maajabu ya dunia na haijawahi kutokea. Hii ni sawa na mtu kuogopa kivuli chake mwenyewe. Mheshimiwa Rais, kipenzi cha watanzania, tafadhali jitokeze hadharani utushukuru walau kwa maneno matupu kwa kukuamini na kukupigia kura za kishindo.

Huna haja ya kujiona mnyonge bali unatkiwa kutembea kifua mbele kwa kuaminiwa na CCM na kuchaguliwa na wanachi kushika wadhifa huu mkubwa katika nchi. Mama umefanya mambo makubwa sana na maendeleo tunayona. Umejenga mabarabara kila kona ya nchi na umemwaga fedha chekwa kwa wajasirimali. Nani kama mama? Hakuna.

Wewe ndiye Rais wetu kipenzi tuliyekupigia kura za kishindo haijawahi kutokea katika nchi hii. Tuna kiu ya kukuona ukifanya mikutano ya hadhara na kuwapongeza wananchi kujitokeza kwa wingi kukupigia kura, licha ya kuhimizwa na CHADEMA wasusie zoezi la kupiga kura.

MAONI YANGU
Nimeskikia huko mtaani kuna wachochezi wanadai eti polisi wamewaua watoto zao ndio maana unaogopa kwenda kuwaona. Waongo wakubwa! Usiwasikilize hata kidogo. Hivi mama anaweza kuagiza watoto wake wauliwe? Haiwezekani. Haya yote yanasemwa kwa kuwa hujitokezi hadharani ukanushe. Siku ukija kutushukuru hebu njoo ukanushe huu uvumi unaozidi kuenezwa hapa mitaani. Kadri unavyochelewa ndipo wachochezi wanazidi kutengeneza picha na video za uchochezi kutumia AI ilmradi tu wakupake matope. Usikubali mama yetu mpendwa.
​
 
Kuongoza ndiyo kuzunguka kushukuru?..hao waliopita walienda shukuru baada ya muda gani?
Unataka kumpangia muda? Acha kuwapangia watu muda wa kushukuru. Wanaweza kushukuru muda wowote. Kaa chini ule mtori nyama zipo chini.
 
Hawezi anaogopa kuzomewa kwa ushindi wa damu, waliomshauri walimdanganya mazima.
 
Miaka yote tumezoea kuona Rais anayeshinda kiti cha urais akizunguka nchi nzima kuwashukuru wananchi kwa kumpigia kura za ushindi. Safari hii, licha ya Rais Samia kushinda kwa kishindo (98%) na kujinyakulia karibu viti vyote vya ubunge, amekuwa mzito sana kuwazungukia wananchi na kuwashukuru kwa kujitokeza kwa wingi (zaidi ya milioni 31) kumpigia kura. Anaona aibu gani kuja kutushukuru wananchi tuliompa kura za kutosha na kumuwezesha kutetea kiti chake cha uais?

Inashangaza mgombea anashinda kwa kishindo lakini anaogopa kwenda kuwashukuru wapigakura waliompa ushindi. Kuna tatizo gani na ni nini kinachosababisha Rais ashindwe kufanya mikutano nchi nzima kuwashukuru wananchi na kuwapa matumaini kuwa ahadi zake atazitekeleza 100%?

Wagombea waliopata kura chache wamethubutu kuwashukuru wananchi kwa hicho kidogo walichoambulia lakini aliyekula pakubwa bado amejificha kwenye handaki hataki kuonekana hadharani mbele za wananchi! Haya ni maajabu ya dunia na haijawahi kutokea. Hii ni sawa na mtu kuogopa kivuli chake mwenyewe. Mheshimiwa Rais, kipenzi cha watanzania, tafadhali jitokeze hadharani utushukuru walau kwa maneno matupu kwa kukuamini na kukupigia kura za kishindo.

Huna haja ya kujiona mnyonge bali unatkiwa kutembea kifua mbele kwa kuaminiwa na CCM na kuchaguliwa na wanachi kushika wadhifa huu mkubwa katika nchi. Mama umefanya mambo makubwa sana na maendeleo tunayona. Umejenga mabarabara kila kona ya nchi na umemwaga fedha chekwa kwa wajasirimali. Nani kama mama? Hakuna.

Wewe ndiye Rais wetu kipenzi tuliyekupigia kura za kishindo haijawahi kutokea katika nchi hii. Tuna kiu ya kukuona ukifanya mikutano ya hadhara na kuwapongeza wananchi kujitokeza kwa wingi kukupigia kura, licha ya kuhimizwa na CHADEMA wasusie zoezi la kupiga kura.

MAONI YANGU
Nimeskikia huko mtaani kuna wachochezi wanadai eti polisi wamewaua watoto zao ndio maana unaogopa kwenda kuwaona. Waongo wakubwa! Usiwasikilize hata kidogo. Hivi mama anaweza kuagiza watoto wake wauliwe? Haiwezekani. Haya yote yanasemwa kwa kuwa hujitokezi hadharani ukanushe. Siku ukija kutushukuru hebu njoo ukanushe huu uvumi unaozidi kuenezwa hapa mitaani. Kadri unavyochelewa ndipo wachochezi wanazidi kutengeneza picha na video za uchochezi kutumia AI ilmradi tu wakupake matope. Usikubali mama yetu mpendwa.
​
mama hawezi hiyo labda atume mwakilishi
 
Apigwve mawe, yan huyu saivi anaish kama digidigi.
Hana aman, usalama wake ni mdogo sana huwez gombana na nchi nzima isipokua chawa wako afu uzurure hivyo mitaan.
Labda akawashukuru Wajomba zake Dubei, uganda na Zenj.
 
Anaangalia Upepo
Pia Mwambie Aende Kenya kuweka mambo sawa Na majirani
Bila kusahau Atembelee Nje Kuweka Diplomasia Vyema
 
Siku operation ya kuuwa nyumbu wote wezi na waharibifu wa mali ikikamiliza
 
Kuongoza wananchi si ndio mambo ya viongozi au mambo yao ni yapi labda utuambie mkuu?
Mkuu kwa taarifa yako akitaka kuzunguka atazunguka popote. Sana sana kama hajazunguka ujue hakuna fungu la kulipa wahudhuriaji kwa sasa. Ifahamike hana aibu wala chama chake hakina aibu, sana kwa sasa wameingiwa na hofu kwa ile voters turn out, ama na haya mauaji aliyofanya. Lakini bado vyombo vya dola vitampa ulinzi ambao ndio imani yake ilipo.
 
Siku operation ya kuuwa nyumbu wote wezi na waharibifu wa mali ikikamiliza
Sasa kama anaweza kuua kiasi hicho na wauaji anao anaogopa nini kuwatembelea wananchi wake?
 
Anaangalia Upepo
Pia Mwambie Aende Kenya kuweka mambo sawa Na majirani
Bila kusahau Atembelee Nje Kuweka Diplomasia Vyema
Ila hawezi kwenda Marekani....akitia mguu huko, anatiwa pingu.
 
Back
Top Bottom