PostGE2025 Ni lini Rais Samia atazunguka tena mikoani kuwashukuru wananchi kwa ushindi mzito?

PostGE2025 Ni lini Rais Samia atazunguka tena mikoani kuwashukuru wananchi kwa ushindi mzito?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Akifanya hivyo atawatesa sana watu wake waliomuweka kwenye hiyo nafasi. Namaanisha policcm na wale vijana wa Si Di Efu. Maana watalazimika kumlinda mpaka basi.

NB:- Kwanza kwenye demokrasia ya kweli hakuna ushindi wa 98%!!! Badala yake utakitana na ushindi wa 50% - 60%
 
Akizembea kidogo kwenye hizo ziara tunaweza kuhushudia bendera ikipepea nusu mlingoti
 
Baada ya uchaguzi ulioangaliwa kwa karibu na kukosolewa na wengi,.. ambapo "tume huru" ya uchaguzi ilimtangaza na kumrudisha madarakani Rais Samia kwa kura takribani asilimia 98, Watanzania wengi wamekuwa wakijiuliza jambo moja: Ni lini kiongozi mkuu wa nchi atarejea mikoani kuwashukuru wapigakura wake?

Rais Samia, ambaye ameweka historia ya ndoto yake kama rais wa kwanza mwanamke nchini Tanzania na rais wa kwanza kushinda kwa 98%, ameendelea kupata pongezi na mapingamizi kutoka ndani na nje ya nchi kutokana na ushindi huo mkubwa.

Hata hivyo, tofauti na desturi ya baadhi ya viongozi kutoa shukrani za moja kwa moja mikoani kwa wananchi mara baada ya uchaguzi, hadi sasa hakuna ratiba rasmi iliyotolewa kuhusu ziara za shukrani mikoani.

Huku wananchi wengi wakiwa na "shauku" ya kumwona na kumsikia Rais Samia moja kwa moja katika maeneo ya mikoa na wilaya zao, suala la ratiba linabaki kuwa kitendawili kinachosubiri majibu kutoka Ikulu.

Mpaka hapo itakapotolewa taarifa rasmi, swali litaendelea kubaki hewani:
Je, ni lini Rais Samia atazunguka tena mikoani kuwashukuru wapigakura wake?
View attachment 3502909
Inashangaza mshindi wa kishindo kuwaogopa watu waliomshindisha kwa kishindo. Ni aibu kubqa sana.
 
Back
Top Bottom