Ni lini tutataka nchi zilizotutawala, dini zilizotudanganya, kutuibia na kutuharibu zitulipe fidia kwa uharibufu na hasara vilivyotusababishia?

Ni lini tutataka nchi zilizotutawala, dini zilizotudanganya, kutuibia na kutuharibu zitulipe fidia kwa uharibufu na hasara vilivyotusababishia?

Ukoloni ni hali ya nchi moja kuitawala nchi nyingine kisiasa,kiuchumi na kiutamaduni.Sidhani kama hapa duniani kuna taifa ambalo halijawahi kutawaliwa.Kwetu waafrika tatizo ni kuendekeza athari za ukoloni.Wachina, wahindi nao pia walitawaliwa lakini baada ya uhuru wakaondoa misingi yote ya kikoloni na mpaka leo India wanafikiria kufuta jina hilo kwani lina chembe za ukoloni wakati sisi bado tunatukuza ukoloni.Hoja ya mleta mada haitaji mkoloni wetu ni nani na hivyo hoja ni jumuishi.Kataa ukoloni na tukuza uv wako ili jina la Afrika tulifute kwani ni la wakoloni.
 
Jaboja, umekunywa ngapi leo mwanangu au umevuta bangi. Sasa ndiyo nini umesema na unajibu nini na nani? Tafadhali acha bangi.
Labda nikuongezee dini gani iliyokudanganya na kueneza chuki? Labda utaelewa kidogo
 
Kwa wataalamu wa historia, sayansi ya jamii, na uchumi, umaskini na kubakia nyuma kwa Afrika ni matokeo ya ukoloni uwe wa kisiasa au kiimani au kiutamaduni kama siyo kijamii.

Kupitia jinai hii, nchi za magharibi na za mashariki ya kati ziliingiza dini na kutuibia mali nyingi huku zikiharibu na kufuta mila zetu za maana. Kutokana na hali hii, Afrika ni kama mbuzi aliyefundishwa na fisi kula nyama na akaanza kuwatafuna watoto wake mwenyewe.

Rejea chuki za kidini, migogoro ya kisiasa baina ya nchi na nchi na uoza mwingine mwingi. Ni Waafrika tu wasiotumia majina yao au tuseme waliopoteza utambulisho wao. Akiitwa Mwafrika, kwa walio wengi mbali na wale walioshikilia mila zao, kabla ya kumuona, ima utajua ni mwarabu au mzungu, mkristo, au muislam.

Ajabu, zaidi ya ardhi, madini, utajiri, na vyakula vyetu, hawa waliotuhadaa kutuibia, wanachukia kila tulicho nacho kuanzia rangi yetu hadi mila zetu. Je ni lini tutawabana lau watufidie vinginevyo tuwapige marufuku kwenye bara letu? Je, kwa uzwazwa tulio nao, tutaweza?

NAOMBA KUWASILISHA WANANGU.
Huwa nachukia sana ninaposikia eti Waafrika wanadai fidia. Stupid!!!
 
Mfano wangechukua kila kitu chao walichokijenga Africa yaani kubomoa kila kitu chao walichokijenga kuanzia miji majengo madaraja barabara viwanda mashamba mashule vyuo tuanze upya je tungeweza?
 
Umasikini sio matokeo ya kutawaliwa bali ni fikra za wananchi husika.
Kipimo cha fikra je watu wetu toka asubuhi hadi usiku wanajaza nn kwenye fikra zao kama una taifa 80% ya fikra zao kwa siku wanajaza ushabiki wa mipira, miziki ya kipumbavu inayoua fikra zaidi ya kufundisha watu ngono haina jipya, habari za udaku na umbea je tuwalaumuje wakoloni kama hatuna macho ya kuona fursa tele kila kona.
Shida ni fikra na sio mkoloni.
Mkoloni aliondoka miaka 60 iliyopita tena na begi lake tuache kutumia history kuhalalisha kushindwa kwetu.
 
Nikukumbushe tu kwamba hizo dini bado wanajitwalia sadaka kutoka kwa waamini walima vibarua na wavuja jasho.
Wapo wanaojiita mitume na manabii hapo bila hela hutii shoo. Yaani mleta mada umeleta uchonganishi jukwaani
 
Nikukumbushe tu kwamba hizo dini bado wanajitwalia sadaka kutoka kwa waamini walima vibarua na wavuja jasho.
Wapo wanaojiita mitume na manabii hapo bila hela hutii shoo. Yaani mleta mada umeleta uchonganishi jukwaani
Hakuna jambo linafanikiwa bila sadaka hata kwa shetani bila sadaka huwezi kupata utakacho
 
Back
Top Bottom