Ni mambo gani mepesi kufanyika ambayo huwezi kuyafanya?

1. Kutoa au kupokea rushwa
2. Kuendelea kuwa Mtanzania kama watapitisha sheria ya kinga mwa maafisa wa usalama,
 
1. Kupiga mluzi, kuna dada mmoja tangu ajue siwezi kupiga mluzi basi kila akiniona anakuja nikuringishia kwa kunipigia mluzi masikioni.

2. Kula taratibu. Yaani kila nikikaa na watu kula pamoja, lazima niwe wa kwanza kumaliza.

3. Kupiga kura, yaani mimi ninyanyuke kwenda kituoni kupiga kura? Lata nikirogwa siendi...

4. Kubargain bei wakati wa kununua kitu. Mimi huwa natoka na bei yangu nyumbani. Ukifika sawa, usipofika natembea mbele...
 
Kuvuta sigara ........ Nishashindwa kabisa ! Sijui wanawezaje kuvuta ,Nilijaribu nikawa na nunua hadi pakiti ,ila najikuta nasahau kuvuta na najikuta nazifulia kwenye nguo

siku moja nikashushuliwa eti sina sura ya uvutaji sigara na pisi kali moja hivi .

Soo nishaamua kuachana nayo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…