Ni mambo gani mepesi kufanyika ambayo huwezi kuyafanya?

Ni mambo gani mepesi kufanyika ambayo huwezi kuyafanya?

1. Kukata chips Kama wanavokata wakaanga chips wanamenya kiazi wwnapiga mistari yao sijui ndo ya diagonal chap vipande vinatokea Mimi nahangaika nitaanza kukata kwenye circle Kwanza ndo circle moja nitoe vipande.

2. Kupiga mlunzi aisee nimeshindwaga

3. Kucheza mziki ni rahisi Ila nishapishana nao naonaga hata Soo kwenye watu wengi kucheza kimasai aisee labda ningekuwaga kwenye team ya dance nikaririshwe zile move Ila me na style yangu moja tu ama mbili za mziki hizohizo naishi nazo sitaki shida.

4. Kufungua kizibo Cha chupa ya bia kwa chupa nyingine..hii kitu imenishinda Nisha jaribu mshikaji wangu yeye akikaa kwenye meza haitaji opener anashika chupa mbili anaziumanisha kwaa moja inaachia sijui huu ujuzi unakuja Kama kipaji ama laa.

5. Kuongea na simu bila kuweka loudspeaker hii Sasa ni tabia imejengeka mpaka naona kuongea bila loudspeaker sikuelewi vizuri labda iwe ishu ya Siri Sana Ila mazungumzo yoyote ya kawaida lazima nikuweke loud

Hiyo namba 4, mimi nilishatoka huko kwenye hiyo style!
Kwa sasa mimi naweza kutumia pua, jicho, sikio, kucha ama kiganja kufungua chupa!
Ni concept ndogo tu inatumika hapo!
 
Hii hata Mimi inanipa changamoto unakuta MTU yupo comfortable kabisa anapiga ubwabwa kwenye kisinia mpk huwa nahisi labda waislam wanazoeshwa wakiwa wadogo huko madrasa
Nilikua nawaza hivyo hivyo, hii style ni pendwa Sana kwao hasa kwenye ubwabwa nilishaijaribu nimeshindwa.
 
Back
Top Bottom