Ni mambo gani uliwahi kuona kanisani kwako ya kakuacha mdomo wazi? Mimi kuzikwa mifupa ya mwanzilishi wa kanisa hilo mimbarini

Ni mambo gani uliwahi kuona kanisani kwako ya kakuacha mdomo wazi? Mimi kuzikwa mifupa ya mwanzilishi wa kanisa hilo mimbarini

NB kwa maelezo ya mleta mada ninathubutu kusema sio mkatoliki maana naona hajui kila kitu.
Ni mkatoliki wa kuzaliwa,ubatizo,kumnyo,kipaimara na ndoa. Kwenye kitambulisho changu Bado sehemu ya kifo tu ndo ipo wazi Kwa sasa.

Sijui Ili niwe mkatoliki inahitajika niwe na Nini zaidi. Awali nimesema wazi sijawahi ona tangiapo hii niliyoona
Sijawahi hudhuruli kwenye kutabaruku kanisa hii ndio mwanzo Huwa ikifanyika mara kadhaa Huwa sihudhurii.

Unaposema masalia sisi katekista aliyekuwa kama Mc ndo alikuwa anasema mifupa. Sasa tukuamini wewe au yeye au sisi tuliokuwepo?
 
Kwa kifupi Mimi kwenye kitu nilichoshuhudia Huwa sihitaji debate otherwise ningekuwa nimesimuliwa na hiki ndo nilichoona na kusikia pale kama unataka USHAHIDI/ uthibitisho njoo pm nikuambie kanisa lilipo uende ukafukue kama utarusiwa ushuhudie kilicho zikwa hapo kama ni makapi au kope za marehemu.
 
Mi Nashangaa tuu eti kama hauna Jumuiya hawakuziki kikanisa. ila kama ni tajiri wanakuzika.
Hukuona Kingunge Ngombare Mwiru walivyomuingiza kwenye ukristu ghafla bin vuu wakati anakaribia kufa?! Angekuwa mtu wa kawaida ambaye hana mkwanja na umaarufu nani angehangaika nae ?!
 
Umezunguka sana lakini hapo unamaanisha RC.
Kwanza hakuna kitu kinachoitwa kusimika au kuzindua kanisa.Na masalia yanayowekwa sio ya muanzilishi wa kanisa maana muasisi wa kanisa ni Yesu mwenyewe alipomuambia Petro ya kwamba atalijenga kanisa lake juu yake.

Tukio unalosema ni kutabaruku kanisa.Maana yake ni kuliweka wakfu jengo hilo na kulitenga mbali na shughuli nyingine za kidunia/kijamii ili litumike tu kwa ajili ya sadaka ya ibada takatifu ya misa.

Ubani unawekwa katika chungu na kufukizwa juu ya altare (meza ile ya kutolea dhabihu)ishara ishara ya kupatakatifuza na kumsihi Mungu ya kwamba sadaka zitakazotolewa hapo zipae kwake juu na harufu nzuri ya kumpendeza kama moshi huo wa ubani.Kadhalika husuguliwa kwa mafuta matakatifu ishara ya kupatakasa.

Unayosema mifupa ililetwa sina hakika kama uliiona mifupa kwasababu huwa sio mifupa haswa bali chembe ndogo sana ya masalia ya huyo mtakatifu aliyewekwa kuwa msimamizi wa kanisa mahalia.Kwa imani yetu sisi wakatoliki watakatifu wanao uwezo wa kutuombea kwa Mungu ndio maana tuna litania ya watakatifu.Hivyo kuweka alama yake katika kanisa husika ni ishara ya kukabidhi usimamizi wa kanisa husika kwake.

NB kwa maelezo ya mleta mada ninathubutu kusema sio mkatoliki maana naona hajui kila kitu.
Bado hizo chembe za masalia ya mtu aliyekufa ni ushirikina.!
Halafu wewe unamuita binadamu mwenzio mtakatifu kwa kigezo gani?!
Mungu pekee ndiye anayejua nani ni mtakatifu!.
 
"sina hakika kama uliiona mifupa kwasababu huwa sio mifupa haswa bali chembe ndogo sana ya masalia ya huyo mtakatifu"

Hayo masalia ni nini?
Labda ni kucha za huyo maiti wanayemuita mtakatifu!😆😆😆😆
 
kutoka misr kwenda kanaan walibeba mifupa ya Yusufu.Je Yusufu alozikwa wapi? Uvumba ni kitu gani? Acha wazike tu maana ya biblia nayo ni mengi ukiachana na ukristo ambao wengi wanadhani katiba yake ni biblia .Katika imani mengine tujiongeze tu tunaenda .kitimoto ni haramu kwann wana wa Israel waliwafuga?kwanini nguruwe mpaka leo wapo? Kuna miujiza Yesu anafanya mingine anakupaka tope alilofanya kwa mate yake na mingine anasema tu inuka au ona .kwann yote asiseme ona ,tembea .kuwa na imani mdau hata hirizi biblia haikatai .Usinzi tu inategemea mbona Daud alizini nq hakupigwq mawe? Kuna wakati Musa aliua.Yoshua aliua na wanafunzi wa Yesu waliua pia au wewe usomagi biblia ? Unaambiwa hata shetan atauwawa kwa pumzi ya Yesu yaani hata Yesu mwenyewe anaua haah sembuse mimi ?na huko mbinguni kuna vita vinapiganwa yaani hata mbinguni kuna mmama amezaa just image hiyo mimba kama sio ya usinzi n nani aliifungisha hiyo ndoa maanq imeandkwa mbingun hawaoi wala kuolewa.Tafakar ndg .notes mimi sio muislam wala chawa.
Na kama ungekuwa muislamu waislamu tungekuwa na hasara kuwa na mtu mwenye akili mbovu kama wewe!
Endelea huko huko kwa WAVAA MISALABA ndio panakufaa!.
 
Bado hizo chembe za masalia ya mtu aliyekufa ni ushirikina.!
Halafu wewe unamuita binadamu mwenzio mtakatifu kwa kigezo gani?!
Mungu pekee ndiye anayejua nani ni mtakatifu!.
Tuachie ushirikina wetu wewe nenda na utakatifu wako.
Ulishawahi kuona RC imefunga maspika mahali ikiwaita watu wajiunge RC?
Tumejengwa juu ya mwamba Petro mwenyewe hatuyumbi
 
Mkùu sio kweli RC hawaangalii pesa wanaangalia ushiriki wako katika jumuia na kanisani Refer Mzee mrema yule wa Impala na Ngurdoto Padri alikataa wake wakapanda mpaka kwa Askofu akawaambia kaanzieni ngazi ya jumuia mpaka kwa paroko mje na majibu ikabidi watafute walokole uchwara wakawapa mpunga wakaja kuendesha ibadan ya mazishi ill RC waligoma
 
Acha uongo wako ! Mzee Kingunge Ngombare Mwiru alikuwa akishiriki jumuia gani au hakuzikwa kikatoliki yule ?!
 
Mkuu mkaa unawekwa kwenyw chungu kutokana na chetezo kutotosha mkaa uho kisha umwaga ubani ndani ya mkaa ukisema watumie chetezo mpaka ibada iishs moto utazim san

Kuhusu mifupa ni mifupa ya watakatifu ni njia moja wapo ya kuungana nao katika sala zao
 
Mimi sina dini ya aina yeyote ile.

Sasa punguza mihemko yako kudhani kila mtu ana udini.

Ukristo na Uislamu zote ni UTAPELI.
Kutuambia kwamba huna dini huo ni uongo bana ...........walikupaje jina ??
 
Umezunguka sana lakini hapo unamaanisha RC.
Kwanza hakuna kitu kinachoitwa kusimika au kuzindua kanisa.Na masalia yanayowekwa sio ya muanzilishi wa kanisa maana muasisi wa kanisa ni Yesu mwenyewe alipomuambia Petro ya kwamba atalijenga kanisa lake juu yake.

Tukio unalosema ni kutabaruku kanisa.Maana yake ni kuliweka wakfu jengo hilo na kulitenga mbali na shughuli nyingine za kidunia/kijamii ili litumike tu kwa ajili ya sadaka ya ibada takatifu ya misa.

Ubani unawekwa katika chungu na kufukizwa juu ya altare (meza ile ya kutolea dhabihu)ishara ishara ya kupatakatifuza na kumsihi Mungu ya kwamba sadaka zitakazotolewa hapo zipae kwake juu na harufu nzuri ya kumpendeza kama moshi huo wa ubani.Kadhalika husuguliwa kwa mafuta matakatifu ishara ya kupatakasa.

Unayosema mifupa ililetwa sina hakika kama uliiona mifupa kwasababu huwa sio mifupa haswa bali chembe ndogo sana ya masalia ya huyo mtakatifu aliyewekwa kuwa msimamizi wa kanisa mahalia.Kwa imani yetu sisi wakatoliki watakatifu wanao uwezo wa kutuombea kwa Mungu ndio maana tuna litania ya watakatifu.Hivyo kuweka alama yake katika kanisa husika ni ishara ya kukabidhi usimamizi wa kanisa husika kwake.

NB kwa maelezo ya mleta mada ninathubutu kusema sio mkatoliki maana naona hajui kila kitu.
Nimeogopa kabisa!! Yaani 'chembe ndogo kabisa ya masalia ya huyo mtakatifu....' like serious!!?

Huo si uganga kabisa jamani!!!

Chungu, ubani, masalia!! Ukianza kutetea haya utaweza??

Why all that??

Afu hapo 'kwa imani yetu sisi wakatoliki...' where is that imani coming from?

Is it from the Bible? Au from the so called 'mapokeo matakatifu?'

Huyu hawezi kuwa Mungu wa kweli! No!
 
Back
Top Bottom