Ni mambo gani uliwahi kuona kanisani kwako ya kakuacha mdomo wazi? Mimi kuzikwa mifupa ya mwanzilishi wa kanisa hilo mimbarini

Ni mambo gani uliwahi kuona kanisani kwako ya kakuacha mdomo wazi? Mimi kuzikwa mifupa ya mwanzilishi wa kanisa hilo mimbarini

Umefanya zaidi ya MC! Kwa nini usiwaulize viongozi wa hilo "unalodai ni" dhehebu lako huko?
Soma vizuri verse ya2 kutoka mwisho nimesema

Hakika kwa haya yameniacha mdomo wazi na sio mimi tu nimejaribu kuuliza viongozi kadhaa wa dhehebu langu sijapewa jibu la kueleweka maana mimi niliona kama ni kinyume na ukristo.
 
Hii siyo hadithi wala story ni mwaka huu tu imetokea kwenye kanisa langu la siku zote.

Basi kulikuwa na usimikaji/kuzindua kanisa jipya tulilo changa ma hela kwa miaka kadhaa hadi mwaka huu likawa limekamilika na hatimae Askofu alikuja kulizindua kanisa hilo pamoja na kupewa hadhi ya kuwa parokia

Jambo lililo tuacha midomo wazi waumini wengi ni mambo kadhaa wa kadhaa (sita yataja yote) tukio la kulisimika kanisa lilianza saa3 asubuhi hadi saa10 jioni.

Moja ya matukio tuliyoona kwa macho ni mifupa ya marehemu aliye fariki siku nyingi kuletwa na kuzikwa kweye arutale(mimbari) Huyu marehemu ambaye kwa sasa tunamuita MT fulani kwa imani yetu.

Kulikuwa na chungu kama vile vya waganga wa kienyeji na vilikuwa na vitu kadhaa mle ndani pamoja na mkaa wa moto huku moshi mzito ukifuka.

Baada ya yote hayo kuisha kiongozi wetu wa dini yaani (.....) alipapaka mafuta na kuanza kupasugua na kupasafisha yeye mwenyewe. Na mengine mengi.

Hakika kwa haya yameniacha mdomo wazi na sio mimi tu nimejaribu kuuliza viongozi kadhaa wa dhehebu langu sijapewa jibu la kueleweka maana mimi niliona kama ni kinyume na ukristo.

Wakuu nahitaji kuuliza maana nilijua najua vitu vingi kwenye imani yangu kumbe bado kabisaaa ni mtoto.je hii ina ulazima gani na kwanini ifanyike hadharani na mc akitangaza hadharani kwenye vipaza sauti na watu wasio sali dhehebu letu wasikie na kujua kinacho endelea?

Je, wewe umewahi kuona kitu ambacho kilikuacha mdomo wazi na maswali mengi .
Wewe huhitaji msaada wowote wa kutaka kujuwa au kuelimishwa. Kwanza ulitakiwa utaje hilo dhehebu la kikristu unalolizungumzia, pili utaje bimbo na parokia husika na pia ungenukuu maneno mawili matatu au hata zaidi alichosema huyo mc au huyo askofu. Wewe umeleta dharau na kashfa tu kwa dhehebu ambalo kila mtu atakuwa na husia nalo. Hayo ndio maoni yangu.
 
sawa
 
Mkuu hayo ni mambo ya kabisa katoliki, ukiona kabisa Linaitwa parokia ya mtakatifu "yuda thadei" ujue Kuna mifupa ya huyo mtakatifu altareni, huo ni upagani kama upagani mwingine eg kuombea wafu,kuabudu sanamu nk..
Kuna vingi vinafanyika kinyume na biblia,
Sasa kama mifupa ya huyo yuda itapelekwa kwenye makanisa yote yaliyoitwa jina lake,si itakwisha.
 
Kwa mfano mtakatifu yuda Thadei ni msimamizi wa makanisa zaidi ya buku duniani kote, sasa ukisema mifupa yake ikazikwe kwenye kila kanisa analosimamia inamaanisha mifupa ya mwili wote haitatosha kugawa kwenye makanisa yote duniani.
Ndio mana unaambiwa ni chembe ndogo sana ya masalia yake sio lazima iwe mifupa.Hapo mifupa mara nyingine inatumika kama lugha ya ishara tu.

Masalia yake mengine kama vile nywele nayo ni sawa?
 
Umezunguka sana lakini hapo unamaanisha RC.
Kwanza hakuna kitu kinachoitwa kusimika au kuzindua kanisa.Na masalia yanayowekwa sio ya muanzilishi wa kanisa maana muasisi wa kanisa ni Yesu mwenyewe alipomuambia Petro ya kwamba atalijenga kanisa lake juu yake.

Tukio unalosema ni kutabaruku kanisa.Maana yake ni kuliweka wakfu jengo hilo na kulitenga mbali na shughuli nyingine za kidunia/kijamii ili litumike tu kwa ajili ya sadaka ya ibada takatifu ya misa.

Ubani unawekwa katika chungu na kufukizwa juu ya altare (meza ile ya kutolea dhabihu)ishara ishara ya kupatakatifuza na kumsihi Mungu ya kwamba sadaka zitakazotolewa hapo zipae kwake juu na harufu nzuri ya kumpendeza kama moshi huo wa ubani.Kadhalika husuguliwa kwa mafuta matakatifu ishara ya kupatakasa.

Unayosema mifupa ililetwa sina hakika kama uliiona mifupa kwasababu huwa sio mifupa haswa bali chembe ndogo sana ya masalia ya huyo mtakatifu aliyewekwa kuwa msimamizi wa kanisa mahalia.Kwa imani yetu sisi wakatoliki watakatifu wanao uwezo wa kutuombea kwa Mungu ndio maana tuna litania ya watakatifu.Hivyo kuweka alama yake katika kanisa husika ni ishara ya kukabidhi usimamizi wa kanisa husika kwake.

NB kwa maelezo ya mleta mada ninathubutu kusema sio mkatoliki maana naona hajui kila kitu.
Shukurani sana na ahsante sana kwa eliminate hii kwa watu wote na yeye mleta Madam.
 
...Hilo Kabisa halina Jina ? Kama ilitokea kweli Kwa Nini unaficha jina la Kanisa ?? Ilikuwa Siri ??...
Umeuliza kana kwamba jamaa ni Muongo. sasa mimi nakupa uhakika ukitaka nenda kathibitishe. Siku ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kanisa Jipya la RC Mjini Dodoma mtaa wa Area A, yalizikwa majivu ya mifupa ya mtakatifu wao katika miambari ya kanisa. Na walienda kwa maandamano kuyapokea Airpot.

So sio uongo maana mwanzo nilizani mleta uzi anazungumzia hilo kumbe stori yake imetokea kanda ya ziwa.
 
Kuna siku niko chachi kuna mzee wa kanisa nikamuona ananyata katikati ya mabenchi akanyanyua mkono juu akamnasa bonge la kibao muumini na akamtoa nje kuulizia nini? Eti yule alikuwa mwana maombi RC wanajua wale karismatik
 
Mkuu kubishana na watu wa hivyo ni kupoteza muda tu. Niseme uongo kwa kanisa ninalo mimi mwenyewe ili iweje na kwa faida ya nani?
 
Kuna siku niko chachi kuna mzee wa kanisa nikamuona ananyata katikati ya mabenchi akanyanyua mkono juu akamnasa bonge la kibao muumini na akamtoa nje kuulizia nini? Eti yule alikuwa mwana maombi RC wanajua wale karismatik
Mimi pangechimbika asee
 
Back
Top Bottom