Ni mambo gani yanadhihirisha utayari wa mwanamke kuingia katika mahusiano ya ndoa/ mapenzi?

RAYAN THE DON

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2019
Posts
679
Reaction score
1,220
Habari za mchana wakuu wa MMU. Natumai mpo salama na mnaendelea vyema kabisa na majukumu ya hapa na pale.

Lengo kubwa la uzi huu ni kutaka kujua ni ishara gani au ni vitu gani vinadhihirisha kwamba mwanamke yupo tayari kuingia katika mahusiano ya kimapenzi/ndoa. Nimeuliza hivyo kwa sababu kila mwanamke ana lugha yake ya upendo (love languages) kwa amapendae, yaani namna ya kueleza upendo kwa mtu wake anayemkubali.

Bila kupoteza muda ni kwamba nimetokea kumpenda dada mmoja kwa lengo la kuwa mke wangu. Nimekuwa nikionesha upendo mkubwa sana kwake na mambo mengine mengi sana ingawa kiukweli nashindwa kumuelewa kwa sababu nimekuwa nikijitahidi kuonesha upendo wangu kwake kwa kumjali. Katika kumjali sina utani kabisa na nimemueka kama my first priority ingawa amekuwa akionesha ishara amabazo zinanipa wakati mgumu sana mfano tukiwa wote pamoja anakuwa ni mtu asiyejali kabisa lakini tukiwa mbali yaani hatuko pamoja huwa anaonesha positive affirmation katika kuchati kwa WhatsApp.

Kadhalika, kwa upande wa mawasiliano ni mpaka nimuanze mimi kama sijamtafuta hawezi kunitafuta kamwe na anapenda kutuma meseji kuliko kuongea kwa simu. Ingawa nikimuanza huwa anaonesha muitiko ambao ni chanya wakati wa kuchati mpaka nafurahi.

Aidha, siku katika mazungumzo yetu niliwahi kumuuliza kwamba inaonesha unakuwa na shughuli nyingi mpaka unanisahau. Alichonijibu ni kwamba yes nakuwa busy sana, labda niwe nakaa nyumbani ili nisiwe busy. Nikamwambia just relax, I was joking. Tukaishia hapo.

Sasa wadau wa MMU kwa muktadha huo hapo juu, je niendelee kupambana au mambo anayoonesha ni ishara tosha kwamba sina changu ili niweze kutafuta mtu mwingine?

karibuni kwa michango yenu wakuu.

Ahsanteni sana.
 
Mapenzi haya daah!!

Ila Mkuu inaonekana wew sio first priority kama wew ulivo muweka

Ata MTU awe busy vip atakutafuta atakukupa hi inatosha

Ila kama wew ndo kila siku unaanza kumtafuta stuka

Itakua wew ni third priority!

Mkuu move on muache na Maisha yake .

Wanasemaga if it's belong to you will find a way.
 
Hakika Mkuu. Nashukuru sana.
 
Inawezekana ana mwanaume mwingine ambaye pengine amemwambia vitu anavyomiliki siunajua tena hawa wanawake wanahitaji zaidi security
 
ushaonesha mwanaume mtiifu hawezi kukupenda kamwe unless uwe na pesa akupendee pesa zako,mkiingia kwenye ndoa jiandae na watoto wa nje[emoji3].
 
Habari za mchana wakuu wa MMU. Natumai mpo salama na mnaendelea vyema kabisa na majukumu ya hapa na pale.

Lengo kubwa la uzi huu ni kutaka kujua ni ishara gani au ni vitu gani vinadhihirisha kwamba mwanamke yupo tayari kuingia katika mahusiano ya kimapenzi/ndoa. Nimeuliza hivyo kwa sababu kila mwanamke ana lugha yake ya upendo (love languages) kwa amapendae, yaani namna ya kueleza upendo kwa mtu wake anayemkubali.

Bila kupoteza muda ni kwamba nimetokea kumpenda dada mmoja kwa lengo la kuwa mke wangu. Nimekuwa nikionesha upendo mkubwa sana kwake na mambo mengine mengi sana ingawa kiukweli nashindwa kumuelewa kwa sababu nimekuwa nikijitahidi kuonesha upendo wangu kwake kwa kumjali. Katika kumjali sina utani kabisa na nimemueka kama my first priority ingawa amekuwa akionesha ishara amabazo zinanipa wakati mgumu sana mfano tukiwa wote pamoja anakuwa ni mtu asiyejali kabisa lakini tukiwa mbali yaani hatuko pamoja huwa anaonesha positive affirmation katika kuchati kwa WhatsApp.

Kadhalika, kwa upande wa mawasiliano ni mpaka nimuanze mimi kama sijamtafuta hawezi kunitafuta kamwe na anapenda kutuma meseji kuliko kuongea kwa simu. Ingawa nikimuanza huwa anaonesha muitiko ambao ni chanya wakati wa kuchati mpaka nafurahi.

Aidha, siku katika mazungumzo yetu niliwahi kumuuliza kwamba inaonesha unakuwa na shughuli nyingi mpaka unanisahau. Alichonijibu ni kwamba yes nakuwa busy sana, labda niwe nakaa nyumbani ili nisiwe busy. Nikamwambia just relax, I was joking. Tukaishia hapo.

Sasa wadau wa MMU kwa muktadha huo hapo juu, je niendelee kupambana au mambo anayoonesha ni ishara tosha kwamba sina changu ili niweze kutafuta mtu mwingine?

karibuni kwa michango yenu wakuu.

Ahsanteni sana.
Mwamba, hamna kazi hapo

Tafuta kazi zingine za kufanya aisee

Kiufupi hupendwi, no one is too busy, its just a matter of priorities
 
Tabia njema, kujua kukata viuno, usafi na mapishi ya mahanjumati.
 
Back
Top Bottom