Ni mapungufu gani ya mkeo/mumeo umeamua kuishi nayo?

Wewe mbona umepata mke kabisa!! Hayo uliyoyaelezea hapa Kama mapungufu kwangu Mimi naona upendo na si kero kama unavyochukulia.... Ungepata BOMU kama la mleta mada nahisi ungekuwa umeshabwaga manyanga siku nyingi.

Yaani mkeo kukupigia simu na kuongea na wewe muda mrefu Tena anamuita na mwanao hili muongee wote watatu wewe unaona ni kero aisee!! Haya anataka kujua zawadi fedha unazotumia kwenye vitu minor kama zawadi unaona anakukera... Kuna wenzako wanayatamani sana haya yote uliyoyaandika hapa wangeyapata kutoka kwa wake zao, lakini ndio hivyo hata moja wapo tu miongoni mwa hayo hawapati.....!!

Mtu ana shauku ya kujua watu wote unaojichanganya nao kwa ustawi wa familia ya baba wa watoto wake.... aisee uyo mke wako ni mke adimu kwa zama hizi, Fanya kuachana nae Kisha ubadilishane na wa huyo jamaa yako Kisha baada ya mwaka urudi hapa kutupa mrejesho.
 
Huyo mke wako anakupenda hongera mkuu wanaume wengi wameoa wanawake ambao hawapendwi na wake zao
Nimemshangaa sana jamaa kuona upendo anaoneshwa na mkewe yeye kwake ni kero.... Mwambie kuwa Kuna wenzake wakipigiwa simu na wake zao basi ujue ni ama luku imeisha au mtoto ameugua ghafla basi, tofauti na hapo mtu anaweza akakaa hata mwezi mzima bila kuona simu ya mkewe.
 
Sifikirii hata kidogo. Sina hata mawazk hayo.

Ni ishara ya upendo, ila kwangu nisiyependa kuzungumza na simu muda mrefu ni tabu kidogo, nikilala kuamshwa sipendi, pia sipendi vijiswali vingi vingi, najua ni upendo ila kwangu ni changamoto
 
Bado kidogo uzabuliwe makofi kwa kufananisha upendo na usumbufu[emoji3][emoji3][emoji3]
 
ok
 
Sifikirii hata kidogo. Sina hata mawazk hayo.

Ni ishara ya upendo, ila kwangu nisiyependa kuzungumza na simu muda mrefu ni tabu kidogo, nikilala kuamshwa sipendi, pia sipendi vijiswali vingi vingi, najua ni upendo ila kwangu ni changamoto
Ni changamoto kwako, unapenda mwanamke mwenye gubu Mzee yule ambaye mnakaa hata wiki nzima hamuongeleshani pale mnapozinguana
 
Acha nimstiri wangu maana nilisema katika shida na raha, iweje nizipende raha tu, shida nianze kuzilalamikia?
Unapoeleza inasaidia kujua kumbe ni mambo ya kawaida na yapo kwa wengi. Unajifunza jinsi ya kuyakabili bila madhara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…