Ni masharti gani ya ajabu uliwahi kukutana nayo nyumba ya kupanga?

Ni masharti gani ya ajabu uliwahi kukutana nayo nyumba ya kupanga?

Mtoto wako haruhusiwi kucheza na mtoto wa mwenye Nyumba na wala haruhusiwi kuzagaa hapo nje kwenye baraza ufungue ndani
Kama una mgeni kbla hajaingia ndani umpitishie kwanza Kwa mwenye nyumba umtambulishe
 
Mtoto wako haruhusiwi kucheza na mtoto wa mwenye Nyumba na wala haruhusiwi kuzagaa hapo nje kwenye baraza ufungue ndani
Hii ilinipa tabu michezo ya watoto mara ashike mlango abamize mwenye nyumba anakua kama moyo wake umebamizwa jmosi mtoto asipoenda shule akicheza akumbuke pensel aanze kuchora ukuta unaweza piga mtoto kwa stress za mwenye nyumba lkn mwisho wa siku unapambana mambo yalivyonishinda nikaama kwa kweli
 
Mimi niliambiwa kama nataka kulewa home nataka kumnunulia mama mwenye nyumba bia zake ili anipe kibali.

Wewe ulikutana na sheria ipi ya ajabu?

Hahaaa mkawa mnapiga nae kilaji
 
Mimi kipindi hiko nikiwa bachela baada ya kupigwa kibuti na mama mwenye nyumba..nikiwa nimevurugwa haikuishia hapo,,basi kila akijua nipo lazima apige ile taarabu inayoimba "tuliza bolu kiwanja kidogooo'..sijui aliimba nani vile😇😥😥😂
 
Niliona hii sehemu mama mwenye nyumba anaomba maharage kwa mpangaji wake nilishangaa sana yaan kapika ugali kisha mboga anaomba kwa jirani

Hilo ndio life la uswaziii...

Washa mkaa nije kuomba wa kukolezea moto wangu, hapo nishaua bajeti ya kiberiti na mafuta ya kuwashia mkaa...
 
Back
Top Bottom