Ni masharti gani ya ajabu uliwahi kukutana nayo nyumba ya kupanga?

Ni masharti gani ya ajabu uliwahi kukutana nayo nyumba ya kupanga?

Kung'oa matembele na Kuacha kulima matembele mara moja. Kipindi hiko Sina kazi. Sasa yale matembele angalau watoto walikuwa Wana uhakika wa kula ugali matembele kila siku. Nikaambiwa.... Sitaki kuona huo uchafu wa mamboga mboga unalima kwenye nyumba yangu.... 😭😂

Nikikumbuka.... Nacheka Sana. Glory to God anayetuvusha salama katika mapito mbalimbali maishani.
Pole sana kwa yaliyopita
Ila yanapita na aibu inawaangukia watu wenye roho mbaya .
 
Mwenye nyumba kutumia vyombo vyangu kuhifadhia vyakula vyake!
Tena anaingia ndani bila hodi wala kuomba, anaelekea kwa kabati la vyombo, mara achukue chupa ya chai, hotpot, vikombe vya chai, sometimes hata kuchukua sukari na chumvi nk!
Dah! Huwa nakereka sana!
 
Ni nyumba ya vyumba sita na wapangaji tupo sita,adhabu inaanzia kwenye umeme,hauruhusiwi kununua umeme inatakiwa umpatie mwenye nyumba pesa yeye ndo atanunua na ukijitia umwamba wa kununua ukimpeleka token hakubali
Choo ni kimoja na hakuna bomba ilhali nyumba ina maji ya dawasco,hivyo yeye ndo anachukua maji kujaza chooni ,ndoo moja asubuhi,moja mchana na moja jioni, na maji yakiisha kabla haweki na mtachambia makaratasi......hapa nasubiria Kodi yangu iishe nihame
Aisee
 
Nisiende chooni kuanzia saa sita usiku,kuna mpangaji alijichanganya akaenda,kilichomkuta sisemi,kufuru na uchawi duniani vipo,wanaokataa hawajawahi kuyaona ya nje ya pazia ya dunia hii,hawajawahi kukutwa na baya lolote nje ya dunia hii
...sasa kwa nini husemi? Kwani unahusika? Unamfichia nani Siri wakati Wadau wamesema watiririke hapa kinachowapata kwenye nyumba za kupana ??[emoji52]
 
...sasa kwa nini husemi? Kwani unahusika? Unamfichia nani Siri wakati Wadau wamesema watiririke hapa kinachowapata kwenye nyumba za kupana ??[emoji52]
Inatosha sana mkuu,niishie hapo tu
 
Nyumba nilizopita zote sijaona sharti la ajabu ila lile sharti la usitoboe ukuta kwangu ni gumu ukizingatia mapazia na TV inabidi vikae ukutani.
 
Nakumbuka kuna mama mwenye nyumba alituambia kwenda chooni haja kubwa mwisho saa mbili usiku(vyoo vya nje, halafu yeye nyumba yake ina dirisha linalotazamana na njia ya kwenda chooni)...kuna kipindi tumbo lilivuruga usiku kwenye saa nne ikabidi niende ...alitokea sijui wapi anagonga mlango wa bati eti nimemletea dharau lazima nimeenda haja kubwa maana nimekaa chooni muda mrefu 🐒
 
Hiyo gereza.
Nashukuru katika kipindi chote cha kupanga sijawahi kutana na vimbwanga.
Na nilijiwekea kanuni uwa sipangi nyumba ambayo mwenye nyumba anaishi maeneo hayo na ambayo mwenye nyumba anaitegemea kuendesha maisha yake.

Nadhan ni huko kwako tu
Mim nyumb nyingi nlizokaa full aman n wala sisumbuan na mtu
Hi ya saahz nmewek n meter yangu
Kwahyo sijawah pigana kelele na mtu
Na hata yeye hana time n mim
Tukikutana Usiku utasikia viiip!!!
Najibu poa mkubwa
(Jamaa mwenye nyumb kijana tu)
 
Mimi niliambiwa kama nataka kulewa home nataka kumnunulia mama mwenye nyumba bia zake ili anipe kibali.

Wewe ulikutana na sheria ipi ya ajabu?
Kuambiwa siruhusiwi kuingiza mgeni wa kike chumbani kwangu, Wala kuingia chumba cha mpangaji wa kike ambaye hajaolewa Wala nisiwe naongea na mke wake hiyo ilikuwa kipindi Niko Chuo second year nimepanga mitaa Fulani ya keko
 
Sio poa kuna nyumba kila kukicha mchango wa buku buku mbili hauishiii na umeme unalipa elfu 10 na bado mchango kila siku alafu mwenye nyumba yeye atoi pesa ya umeme na pesa anakusanya yeye
 
Vituko vya nyumba hizi utazipata maeneo kama dar es salaam basi ni:
manzese
buguruni
tandale
mbangara
temeke
buza
kinondoni maeneo machache
kawe maeneo machache
keko
vingunguti 100%
gongo la mboto

hukipanga hizi sehemu utaona maajabu zaidi ya musa
 
Kuambiwa siruhusiwi kuingiza mgeni wa kike chumbani kwangu, Wala kuingia chumba cha mpangaji wa kike ambaye hajaolewa Wala nisiwe naongea na mke wake hiyo ilikuwa kipindi Niko Chuo second year nimepanga mitaa Fulani ya keko
dah sijajua kwani ukiingiza dem geto mwenye nyumba anakereka utasema mashuka anakuja kufua yy
 
Hii ni kwa wapangaji wote, kama wewe haujapanga basi umepangisha mtu.

Hebu tushirikishane sheria mbovu na za kukera ulizowahi kukutana nazo katika nyumba za kupanga.

Kama wewe ni mpangishaji tuambie sheria za hovyo ulizowahi kuwawekea wapangaji wako.
 
Back
Top Bottom