Ni matumaini yangu Uongozi wa Simba SC utaandaa Uongo wa kutuambia kwanini Bernard Morrison hatoenda South Africa tarehe 24 April, 2022

Mleta mada chuki tuu ndio inamsumbua, mimi ninachojua Morrison kaupiga mwingi mpaka tumeingia robo fainali, hayo mengine umbeya tuu
 
Sasa mbona toka mechi na kaizer chief watu walishajua sababu nn
 
Hakuingizwa mjini, anajuwa kila kitu, mfano wewe Bongo utanunuwa nyumba bila kusearch wizara ya ardhi? Je utanunuwa gari bila kusearch kwenye simu mmiliki halali ni nani?
[emoji38][emoji38][emoji1787][emoji28][emoji23][emoji23][emoji38] deed assignment
 
Hii sio mpya, tangu anasajiliwa Yanga hizi habari zilikuwapo. Kwa hiyo sio kwamba umefuatilia, ni kwamba habari zipo kwa kuwa zilikuwapo
 
mbona hata siyo habari mpya wewe kiazi mbatata.
 
Gentamycin ni Yanga dam dam na haujawahi kuwa Simba hata siku moja. Ila una lundo la ID. Al rounder, nk.
 
Naomba niweke taarifa ya BM kutoruhusiwa kuingia Afrika ya kusini kwa usahihi na uwazi zaidi.
Kuna mambo matukio mawili:
1. La kwanza Bernard Morrison alibambikiwa na wajanja gari la wizi. Akakamatwa nalo na kufunguliwa mashtaka. Uchunguzi ulionesha kuwa hakuwa ameliiba Ila wajanja wa south walimwingiza mjini. Kwa kuzingatia kuwa hakuwa raia wa south, mwendesha mashtaka wa Serikali aliamua kutokuendelea na kesi na akaachiwa huru. Kwa maana hiyo ni kwamba suala la gari ya wizi si sababu téna inayomfanya asiruhusiwe kuingia south Africa Kama wengine wanavyofikiria. Maana suala Hilo liliisha na akaendelea na maisha yake huko
2. La pili ndilo mgogoro hasa uliomfanya azuiliwe kuingia Afrika ya kusini. Ni kuwa aliamua kuendelea kuwepo Afrika ya kusini wakati visa yake ilikuwa imekwisha na hakushughulikia kuomba visa wakati anajua imeisha! Kwa sheria za huko, ukikamatwa huna visa na ukaamuliwa kuondoka, unakuwa umekosa sifa za kuruhusiwa kuingia téna Afrika ya kusini. Hilo ndilo linalomkabili Bernard Morrison. Na Hilo ni jambo ambalo linaweza kushighulikiwa tu na Nchi yake ya Ghana kwa mazungumzo ya kidiplomasia na Afrika ya kusini. Ni lazima Nchi yake imdhamini na kuithibitishia Afrika ya kusini kuwa mtu wao hatarudia téna kosa la kukaa nchini mwao kinyume Cha sheria!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…