Ni maumivu gani ulipitia kipindi huna ajira?

Ni maumivu gani ulipitia kipindi huna ajira?

Ukishatumia Tecno Demu lazima akuache maana anaona huna akili.
Mwanaume mzma wa kuendeshwa na wanawake tatzo la kuanza kuwajua wadada ukubwani inaonekana utotoni ulikuwa unawasikia tu..... Sema we ni bwege Huna point na Huna akili ila tatzo sio wewe tatzo ni wazazi wako kukuzalia kijijini ndo maana Bado tabia za kijijini bado unazo

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Hama uko ulipo ikibidi uende mkoa mwngn wenye maisha nafuu kwa kodi, chakula piga yoyote au biashara yoyote. Hakiksha uko utakakohamia wawe hawajui cv yako weka kando elimu yako.
Mi nimewahi kuosha magari mbezi na wkt mwngn silipwi hata nawafulia madereva na makondakta nguo zao za kazi wakawa hawanipi hata mia hapo nina degree, niliamua kuhama dar kuja mkoa nimefungua biashara zng maisha yanaenda tu.
 
Kwenye swala la kutokuwa na ajira tupo pamoja
Pesa ndogondogo za kitaa tupo pamoja
Hizo dharau bado sijazipata moja kwa moja ila nimeshuhudia likimkuta ndugu yangu
Baada ya chuo nimejifunza mafanikio yanakuja taratibu hayataki haraka tengeneza msingi wako bila kukata tamaa alafu kuwa na subira

Macho na kelele zawatu jifunze kuzivumilia
Apo kwenye mpenzi Pole mnoo ni maisha mangi ata mimi kidogo kamba ingekatika nivile alikuwa anafanyiwa maamuzi siyo maamuzi yake
 
Hama uko ulipo ikibidi uende mkoa mwngn wenye maisha nafuu kwa kodi, chakula piga yoyote au biashara yoyote. Hakiksha uko utakakohamia wawe hawajui cv yako weka kando elimu yako.
Mi nimewahi kuosha magari mbezi na wkt mwngn silipwi hata nawafulia madereva na makondakta nguo zao za kazi wakawa hawanipi hata mia hapo nina degree, niliamua kuhama dar kuja mkoa nimefungua biashara zng maisha yanaenda tu.
Tuko pamoja

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Hizi akili hata sijui huwa mnatoaga wap aisee
Wahitimu wote wakifanya biashara ataajirwa nan?
Wahitimu wote wakitaka kuajiriwa , mjasiriamali atakuwa nan?
Jifunze kubalance mambo
Njia unayopita sio kila mfu ataipita
Mshukuru mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
umewahi kuona muajiriwa tajiri? Yaani unapata hela nyingi una miradi yako. Hao wanasiasa wanajua ni wapi watoto wao wapate ajira, yaani mirija ya hela itiririke muda wote, sehemu kama TRA, Bandari na kwingine kwenye pesa za kupiga ngawira
Ina maan ww hao wenye pesa na ni waajidiwa huwajui ama?
Au ww ni tajifi mjini bila kuajiriwa ?
Utajiri ni akili ya mtu na wala sio pesa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakushauri ujifunze taaluma yoyote itakayokupatia wateja wa moja kwa moja bila kuajiriwa.
Mfano, upigaji picha, graphics design, web development, content creation, digital marketing, etc au tafuta bajaji uingie mzigoni ajira zimekuwa ngumu siku hizi.
 
Najua hali unayopitia kama una degree na uko Dar nenda ofisi za Asa microfinance zipo Upanga peleka CV yako hapo huwa huwa haipiti miezi mitatu au minne bila kuitisha usaili nafasi nyingi huwa ni maafisa mikopo kwa kuanzia utapata channel ya taasisi nyingine pia
 
Noma sana tena sana, sasa ishu ni wewe kujikwamua kiuchumi tu.
Mwenye dhiki hana haya fanya chochote chenye kukulipa vizuri.....if you re not making money then you re making nonesense.
 
Hauko peke yako mkuu, usione kuna uzi wako tu una trendkwa kuwa unapitia changamoto wapo wengi na wana magumu huwenda wewe una nafuu halafu hawakati tamaa na hawajaona issue kuanzisha uzi.

Mtu ni jobless ana familia,amepanga, hata vibarua hana na hakuna connection, mwanamke na watoto wana mwangalia yeye, anatoka asubuhi hana hata issue ,simu haina vocha kakopa na anadaiwa mtaani na mtandaoni!

Wakati ana kazi au kibarua alikuwa na wengi nyuma yake leo kabaki peke yake na familia yake, mwanamke ameshindwa kuvumilia ugomvi kila siku ndani na vyeti vyake kafaulu vizuri kazi anaomba kila siku hata usaili hajawahi kuitwa.

Tulia pambana una nafuu kubwa.
 
Poleni sana.

Kufanya kazi ambayo una utaalamu nayo ama kwa kuisomea ama kwa kuifanya awali ni haki ya kibinadamu.

I am not making this up, nakumbuka kuwa hii ni sehemu ya "Universal Declaration of Human Rights" since December 10 1948.

Inasikitisha sana kuona haki hii ya msingi kabisa ya kibinadamu inakuwa kama bahati nasibu.

Zamani Tanzania ilikuwa ukioma, ukisoma kidogo tu, waajiri wanakufuata shule kabla hujamaliza.

Mimi mwenyewe sijapata changamoto ya ajira, nilianza kufanya kazi tangu nikiwa chuo,kwa sabau watu walinifuata tangu nikiwa mwanafunzi na kunipa kazi.Nilivyomaliza chuo na kupata distinction, ilikuwa fursa tu ya kujiongeza na kupanda ngazi katika ajira, Tanzania hii hii, kabla sijajiongeza kwenda Marekani.

Enough about me.

Nilitaka kuongelea habari za Watanzania kujiongeza kwenye soko la ajira la kimataifa. Nimesikitika sana kuona muhitimu wa mambo ya mafuta analalamika hana kazi Tanzania, wakati rai Rutto wa Kenya amekwenda outh Korea akawaambia Wakenya walio huko kwamba anataka kuongeza idadi ya Wakenya walio nje.

Naelewa kwamba hatuwezi ku export generation nzima,lakini, mtu yeyote tunayeweza kumu export, export kama tunaweza kumu export na kum replicate, that is a competitive advantage.

Napenda kuongelea internalization of the Tanzanian job market.

Kuna ajira nyingi za kimataifa, hususan mitandaoni,kwa watu wanaojua Kiingerezana wenye uwezo wa kupata internet ya uhakika.

Kiingereza na internet ya uhakika ni hangamoto za kuingia katika soko la ajira za kimataifa mitandaoni.

Kwetu sisi tulio nje ambao tunajua kuna watu wenye vipaji vingi nyumbani, ambao wakiwezeshwa wanaweza, na mara nyingine wanaweza tu bila kuwezeshwa, tunapoona ajira nyingi ambazo watu wengi wa nyumbani wanaweza kuzifanya, tunaweza kusaidia vipi?

Kuna kazi nyingi tu za $15 mpaka $30 kwa saa tunazikataa kila siku, za kufanya mitandaoni. Zinahitaji technical knowledge, Kiingereza na solid internet.

Tunaona Wahindi kibao wanafanya. Tunawaunganisha vipi ndugu zetu Watanzania wenye vipaji wafanye kazi hizi?

Kama kuna Mtanzania anakuja New York City (legally) na ana changamoto za sehemu ya kufikia,au pa kuanzia kazi, tuwasiliane.
Nitakuja soon tu. Mwanzoni mwa muongo ujao
 
Mkuu

Kwenye Maisha tambua Kuna nyakati ni lazima kupitia.

Na anopaswa kupitia magumu ni binadam kama wewe.

Tambua ni nyakati za kumjua.nani wako na nani alikufuata kwa ajili ya vitu vyako.

Ni nyakati za kujua ni wapi penye ujuzi au taaluma au elimu gani uboreshe Ili kuwa mzuri zaidi.

Kataa kabisa kujilinganisha na mwingine zaidi yako.

Umri si kigezo Cha kushindwa wala kufanikiwa,Ila ni Ile hali ya kuthubutu kufanya mambo yako Kila siku.

Shukuru na furahia Kila hatua unayofanya haijilishi ni ndogo kiasi gani inayokupa tumaini na kukuonesha unaelekea kupiga hatua Fulani Kila siku.

Acha wacheke,Na wakati wakicheka nawe Cheka,Ila hakikisha cheko lao hulichukulii kama majungu,Bali hamasa ya kuamka Kila siku na kuzidi kujiboresha.

Hatufanikiwi kwa kuumizwa tu na maneno ya wengine kuja kwetu,Bali kunyanyuka na kujituma zaidi pamoja na kutafuta au kutengeneza mbinu nyingi za kutupatia riziki.

Licha ya yote yanayoendelea zingatia hili,

"NYAKATI NGUMU HAZIDUMU"

Karibu PM kwa ushauri zaidi.
Mleta mada pita na hizi nondo utakuja kumshukuru huyu mwamba
 
Back
Top Bottom