Ni maumivu gani ulipitia kipindi huna ajira?

Ni maumivu gani ulipitia kipindi huna ajira?

Mkuu kaza moyo tu, Familia zetu za Kiafrika zina shida sana hasa unapokuwa hauna ajira au kipato cha kueleweka cha msingi nakushauri weka elimu yako pembeni na hayo maneno ya watu wako wa karibu yapuuze kabisa wewe fanya chochote kile ambacho ni halali ili mradi unaingiza kipato chako na vilevile unapata mawazo mapya kwa ajili ya kukujenga. Tumepitia huko hasa kwa hawa wadogo zetu huwa wanakuwaga Wapuuzi sana . Kulalamika sio suluhisho Mkuu.
 
Asante mkuu nimekuelewa kwa maneno yako ya busara,

Kuna mda natama kuongea na mtu ila Sina mtu wa kuongea naye.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Jitahidi kusoma vitabu mkuu tafuta vitabu vinaitwa THE POWER OF POSITIVE THINKING AND MAGIC OF THINKING BIG vitakusaidia sana believes me vile ni zaidi ya vitabu
Believe in yourself and release your inner power
Believe yo can move a mountain
Through your body over the bar and your heart will follow
Believe believe believe believe you can overcome this and God will take you through.
 
Asiajiriwe kwanini?Mtu hana mtaji wa kipésa,hana bima ya afya na mengine mengi,kwanini asiajiriwe kwa taaluma yake,akapate mtaji huko,akiona vipi ndiyo aache kazi?
Usiwe kama mwanasiasa,ambaye anasema wahitimu wajiajiri,halafu watoto wao wanapewa mitaji au wanaajiriwa kiulaini.Grow up.
umewahi kuona muajiriwa tajiri? Yaani unapata hela nyingi una miradi yako. Hao wanasiasa wanajua ni wapi watoto wao wapate ajira, yaani mirija ya hela itiririke muda wote, sehemu kama TRA, Bandari na kwingine kwenye pesa za kupiga ngawira
 
Siku zote wakati wa Mungu ndio sahihi, huyo mdogo wangu ni utoto unamsumbua usimfuatilie sana ... kikubwa endelea kumuomba Mungu wako maana yeye ndio mtoaji wa vyote ni suala la muda tu.
 
Da maisha haya!

Leo nimeamka asubuhi nikiwa na simanzi kubwa moyoni. Mpenzi niliye naye kanipiga chini kisa Sina pesa za kutosha, Sina kazi Nina vyeti na kazi ndogo ndogo za kitaa zinazosababisha nilipe Kodi.

Mdogo angu wa mwaka 2002 kaajiliwa jeshini JWTZ (form four) muda huu anakula mshahara uku Mimi sijui hatima ya maisha yangu, katika kuwasiliana kanambia kauli moja. Bro we si unajikuta msomi mara chuo mara nini aya kula chuo chako sasa.

Now anapendwa na Kila mtu kwenye familia. Matusi mtaani Kila kona. Watu mliosoma nao waliokuwa wanakuona best wote wanakushangaa!

Muda mwingine nakaa chini nawaza ila sijui nifanye nini. Kuna mtu aliwahi pitia haya na aliwezaje ku survive?

Asante.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Mtu na akili timamu unatumia Tecno kweli? Sijawahi ona. Bwege wewe.
 
Huko TAMISEMI na kwenye wizara nyingine,waangalie watu waliomaliza muda mrefu vyuo,watupe kipaumbele,no wonder,mhitimu ni wa 2015,unakuja kushangaa,2022 anachukuliwa,anaàchwa huyu,siyo fair,future zinaharibika.
Kuna mtu anajali future yako basi? Wewe endelea kupoteza muda, utakumbuka shuka asubuhi kumekucha!
 
Vumilia tu mkuu pambana kwa vyovyote utafanikiwa, nyakati ngumu zipo na zinapita. Binadamu asilimia 99.9 ni wanafiki sana na ndo maana mm sitaki kuendekeza urafiki na mtoto wa mtu, Kuna kipindi naweza nikaenda zangu bar nikaagiza ugali mkubwa na kitimoto pamoja na bia nikaendelea kula hata mtu ajichekeshe naweka sura ya kazi sitak mazoea
 
Da maisha haya!

Leo nimeamka asubuhi nikiwa na simanzi kubwa moyoni. Mpenzi niliye naye kanipiga chini kisa Sina pesa za kutosha, Sina kazi Nina vyeti na kazi ndogo ndogo za kitaa zinazosababisha nilipe Kodi.

Mdogo angu wa mwaka 2002 kaajiliwa jeshini JWTZ (form four) muda huu anakula mshahara uku Mimi sijui hatima ya maisha yangu, katika kuwasiliana kanambia kauli moja. Bro we si unajikuta msomi mara chuo mara nini aya kula chuo chako sasa.

Now anapendwa na Kila mtu kwenye familia. Matusi mtaani Kila kona. Watu mliosoma nao waliokuwa wanakuona best wote wanakushangaa!

Muda mwingine nakaa chini nawaza ila sijui nifanye nini. Kuna mtu aliwahi pitia haya na aliwezaje ku survive?

Asante.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Pole mkuu
 
Mtu na akili timamu unatumia Tecno kweli? Sijawahi ona. Bwege wewe.
Mmh mkuu kuna kile kipindi TECNO unaiona kama iPhone 14 Pro

Mi nilikua nashika simu nzuri tuyaani jilikua kama wewe nazichukia sana Tecno na infinix , nilikua mtu wa.iphones haya movie inaanza umemaliza chuo, home wamezidiwa majukumu huna kazi and on top unapatwa na majanga unaibiwa na simu

Well nisikuchoshe niliibiwa iPhone 11 ikatokea sina kazi sina source ya income ya iuelewwka nikaanza kutamani hata nipate tecno ile ya elf 70 😃😃😃 by then akatpkea.bro angu akanipa tecno yake ya muda mrefu i had no optioñ zaidi ya kuchukua

Be humble mkuu
 
Back
Top Bottom