Ni mawazo yamenizidi au uzembe?

Ni mawazo yamenizidi au uzembe?

Juzi jumatano nilikua namnunulia mtu voucher kwenye max malipo ya elfu 10 nikakosea namba ikaenda kwa mtu mwingine. Leo asubuhi nilikua namtumia dogo hela nikakosea hapa nasubiri ndani ya hizi siku 3 irudishwe hiyo hela maana ilikua ni hela ya dogo nimepewa na mtu nimpe ikapitishwa kwangu.
Kinachoniuma zaidi ni sasa hivi nilikua nalipia tena king'amuzi nimekosea namba elfu 69 yangu imeenda na maji.
Inawezekana nina mawazo sana bila kujijua ndo maana nakosea sana au nimekua mzembe tu? Maana hali Hii si kawaida kabisa
Pole sana!

Naomba nijibu kaswali kangu tuu..!

"Mara ya mwisho umechapwa na msaliboko lini??"
 
ishu ya pesa shughulikia kwanza ukiimaliza (kama itawezekana) ndio uende kwa msaikilojia ili akusaidie tatizi lako la mawazo na kukosa umakini lisijirudie siku za baadae..

Naamini ukipewa huo ushauri utabadilika kadiri siku zinavyokwenda
Sawa mkuu nimekuelewa
 
Back
Top Bottom