Ni mazoea mabaya kuombaomba kuchangiwa mara kwa mara

Ni mazoea mabaya kuombaomba kuchangiwa mara kwa mara

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Ni vizuri zaidi kumshukuru na kumuomba mungu kila wakati, bila kuchoka wala kukata tamaa.

Sio tabia njema wala sio tabia nzuri kujenga mazingira au hali ya huruma na kuombaomba kwa wanyonge ambao hawawezi kukataa kuchangia kwasabb wamefundishwa utamaduni kutoa. Utamaduni na malezi haya sio fursa ya kuchangiwa ndugu zangu 🐒

Ni vizuri na muhimu sana kujifuza kujitegemea. Kufanya kazi kwa bidii ili kujiongezea kipato cha kutosha na kuepuka fedheha na aibu ya kutegemea kuomba na kuchangiwa mara kwa mara.

Ni aibu na fedheha kubwa kwa wana familia, ndugu, jamaa, marafiki na taasisi uliopo na kwamba kuomba omba kwako kuna maanisha, hawakujali, hawana uwezo, hawakusaidii na hawana kabisaa msaada kwako. Unawaumiza, unawafedhehesha hawasemi lakini wanaumia sana, hujui tu 🐒
 
Kuna ndugu yangu flani alipitisha mchango ili baba yake akatibiwe na akawa anapitisha bakuli na kilio juu.

Wakati huo yeye binafsi anamiliki ng'ombe zaidi ya 100 kule kijijini, pia mzee wake anamiliki ng'ombe zaidi ya 150 kule kijijini.

Ajabu eti alikua anaomba michango kwetu kwasababu tu tunaishi town, ila hatumiliki hata mbuzi 1 kule kijijini na hilo hakuliona.

Alipokuja kwangu sikumkawiza nikampa vyake na mchango sikutoa, then baba yake alipo fariki eti akatoa ng'ombe karibia 10 kwaajili ya kuliwa msibani, yaani yule jamaa namuonaga fala wa dunia aiseeee...
 
Watanzania hasa CHADEMA wanautaratibu wa kuchangiana MAGUFULI aliwabambikizia KESI akiamini Watashindwa kulipa ila AWAFUNGE lakini Watanzania wenye Mioyo safi sio kama wa kwako usiku huo huo walichanga Mil.300 Zikalipwa Mahakama ya Kisutu Chadema wakaachiwa.
Jambo la maana sana, ni kumumba Mungu bila kuchoka wala kukata Tamaa...

Hata na hivyo ni muhimu zaidi kujitegemea kwa hali na mali. Shughuli za kufanya ni nyingi. Fedheha ya kuomba omba kwa huruma sio utaratibu mzuri, na ni usumbufu kwa wanyonge 🐒
 
Kuna ndugu yangu flani alipitisha mchango ili baba yake akatibiwe na akawa anapitisha bakuli na kilio juu.

Wakati huo yeye binafsi anamiliki ng'ombe zaidi ya 100 kule kijijini, pia mzee wake anamiliki ng'ombe zaidi ya 150 kule kijijini.

Ajabu eti alikua anaomba michango kwetu kwasababu tu tunaishi town, ila hatumiliki hata mbuzi 1 kule kijijini na hilo hakuliona.

Alipokuja kwangu sikumkawiza nikampa vyake na mchango sikutoa, then baba yake alipo fariki eti akatoa ng'ombe karibia 10 kwaajili ya kuliwa msibani, yaani yule jamaa namuonaga fala wa dunia aiseeee...
ni mambo ya kushangaza kidogo....

mfano kuna mwanasiasa anapitisha mchango sasa hivi.
Yes, alikua mgonjwa na alichangiwa vya kutosha matibabu yake ingawa alilipiwa na wasio waTz pia huko ng'ambo....

alivyopona,
akarejea nyumbani na alikua na madai yake kwa serikali ya pesa za matibabu, mishahara pamoja na kiunua mgongo. amelipwa akiwa amepona kabisa na akakiri kua amelipwa....

hivi kweli hakua anajua kwamba atajitahidi gari kwa matumizi yake ya kawaida na hivyo akaamua kufuja hizo pesa, kwa matarajio ya kuomba kuchangiwa tena zoezi ambalo linaendelea?

si mazoea mabaya hayo?
nakuhakikishieni, mwakani ataomba tena achangiwe kama sio gari lingine basi mafuta ya gari 🐒
 
Naomba 500,000 baba.
najiskia kukupatia ng'ambe wa maziwa, umfuge na kuvuna maziwa yakupatie kama hizo nyingi zaidi halafu sifa, utukufu na shukrani viwe kwa Mungu, right?
 
Mwenge wa Uhuru licha ya kuwa hauna tija, Hadi Leo umegeuka kero kuchangisha watu bila ridhaa Yao.
mshahara, pesa za matibabu na marupurupu vilitosha kununua gari ya maana sana 🐒

kwasabb ya mazoea mabaya sana ya kuomba omba ndio maana tena anaomba achangiwe, haitapita mwaka ataomba achangiwe mafuta 🐒
 
Back
Top Bottom