Ni mimi tu au? Maji ya DAWASA ukinywa bila ya kuchemsha yanaumiza tumbo

Mleta mada nahisi hili swali la mtego! Sidhani km ndiyo anachomaanisha! 😄
Anamaanisha maji yanayosemwa kuwa safi na salama sio ya DAWASA.
1. DAWASA maji yake ni machafu, wakati mwingine yanatoka meusi kabisa.
2. DAWASA maji yake si salama kama wasemavyo, ukinywa bila kuchemsha ujiandae kwenda kulazwa kwa matatizo ya tumbo.
 
Kama maji wanatakiwa kuwekea dawa za kuondoa uchafu (flocculants) na kuua wadudu (chlorine) wanataka tuchemshe ya nini? Mbona wizara ya afya Uingereza inatoa angalizo kuwa maji ya bomba ni safi na safe kuliko ya kwenye chupa, sisi tunashindwa nini?
Unafananisha Uingereza na Tanzania!!!
Hivi hua mnajikuta wakina nani nyie Wamatumbi
 
Ni kweli mim ni zaidi ya mara tatu nimeugua mpaka nikafwatilia kwa kina ndio nikagundua kunamaeneo nikiwa natumia maji ya bombani ndio nikaidhinisha ndio sababu.
 
Matumbo yenu wengine yapo kizembe sana na mwili uko dhaifu..tumekua tunakunywa maji msituni pamoja na mifugo pamoja yaliyotuama baada ya muda kunyenyesha Wala ata kuumwa tumbo No,haya ya Dawasa ukichemsha Mimi Huwa siwezi kunywa..ukiweka water guard Ile harufu yake tu kunywa siwezi kwahiyo hapo tafuta Hela uwe unanunua tu maji ya kiwandani...
 
Maji mengi ya Dar es salaam ni machafu sana hata kama yanang'aa

Mengi yana mikojo ya watu ndani yake na wanaua harufu ya mikojo kwa kuweka madawa mengi makali yanayoumiza tumbo na kuleta kansa ya utumbo

Chemsha maji sana ndipo unywe
 
Dah, unakunywaje haya maji ya Tanzania bila kuchemsha? Pole kwa kuumwa tumbo
 
Dah, unakunywaje haya maji ya Tanzania bila kuchemsha? Pole kwa kuumwa tumbo

Nimeyakanyaga.
Nina familia ya watu saba, watoto watano na mimi na mke wangu. Kuchemsha Maji ya Watu saba sio poa ujue.

WaterGuard nayo hazipatikani
 
Awamu ya sita ya Rais Samia ,maji ya dawasco yanamatope did masafi.Dawasco viongozi fanyeni kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…