Ni Mimi tu inanitokea au lah! !!!

Ni Mimi tu inanitokea au lah! !!!

Kwa umri wako ni kawaida kuwa na hali hiyo, zaidi ni kama hujazoea kutongoza, ila usikate tamaa wala usiogope, jiamini kama walikukataa achana nao tafuta wengine mpka utazoea tu
 
Hiyo ni hisia yakawaida kwa kila kijana anapoanza mahusiano na husaidia kupunguza kasi ya kujiaminisha na kumtaka kila anayepita mbele yako kwa lugha nyingine hutia adabu.

Na hata utakaye mpata baadae lazima utamthamini sana kutokana na majeruhi ya wale waliokupuuza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nshatongoza wengi,nshatoswa mara kibao,nshadinya wengi....jitahidi kutongoza kwa akili....alafu jitahidi kuwa nadhifu na mcheshi utazipiga mpaka utakinai........
 
Hivyo pambana na hali yako ila nakushauri mapenzi yana nguvu na ni hatari kwani yanaua hata watu wazima kama hao wanaokukejeli

Cha msingi usiwakwepe maana wataendelea kukunyanyasa kisaikolojia na kukuzungumzia zaidi.
Kuwakwepa ni kukosa kujiamini.
Jipe moyo na endelea kuwasalimia ukikutana nao watapunguza kukusema wala usiweke uadui ila usijisushe sana kwao hadharani watakudharau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pambana dogo usikatishwe tamaa kiboya,.. Utadumaa, ukose mke,
 
Pole Kazana na kitabu
Ila wasichana unaofukuzia ni umri gani??? Kama ni umri wako jiweke smart yaani oga, vaa nguo safi, nyoa nywele vizuri (achana na viduku ) jiweke busy usikae vijiweni wala kuzurula ovyo na ujiamini jiwekee ratiba nzuri watajileta tu na jioni uwe unapiga tizi
 
Habari za wakati huu wanajf!!
poleni na majukumu ya siku ya Leo!!

Niende moja kwa moja kwenye mada.
mimi ni kijana Nina miaka 21.
Nina tabia moja ambayo nashindwa kujua ni tabia ya aina gani.
Nimetongoza wasichana wawili toka nianze Ku..... na wote wamenikataaa kwa sababu wanazozijua wenyewe...
sasa inakuja hivi naumia sana mpaka hata nikimuona msichana mwenyewe natamani kubadilisha njia ili hali tusionane.
Naomba kuuliza kwa wenye uzoefu na mambo haya! hii hali inanitokea mimi tu.... au hata na wengine? Na kama ni hali ya kawaida wewe ulitumia njia gani kuishinda hali hii?

Sent using Jamii Forums mobile app
Pitia huu uzi wa Joseverest
Kutongoza mwanamke: Siri 15 za kumfanya mwanamke yeyote akupende

Sent using Jamii Forums mobile app from my Android phone
 
kweli dunia haieleweki wengine tunasumbuliwa na wanawake hadi kero wengine mnawatafuta
 
Sikiliza kijana kupata na kukosa kupo kushindwa Mara mbili tuu usha kata tamaa je ungekuwa yule aliye gundua umeme ambaye alishindwa Mara 9999 na ushee cha msingi kuwa msafi usinuke kokote unapo ongea usi cheke cheke jiamini na mwangalie USOni pia usitumie pesa kumpata demu mwache alizike nawe ukimpata tulia usianze madharau .

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha
 
Hiyo ni hisia yakawaida kwa kila kijana anapoanza mahusiano na husaidia kupunguza kasi ya kujiaminisha na kumtaka kila anayepita mbele yako kwa lugha nyingine hutia adabu.

Na hata utakaye mpata baadae lazima utamthamini sana kutokana na majeruhi ya wale waliokupuuza

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha
 
Back
Top Bottom