Ni mjinga pekee anayedhani America itaondoa bases zake middle East na kumuondolea vikwazo Iran

Imeloa
1. nani ameingia au amelazimisha deal la cease fire?

2. malengo ya vita yametimia?
-tuchambulie kamoja baada ya kengne tuone!

Ceasefire, ukisoma statement ya Trump, ni kwamba Pakistan ndio iliweka proposal ya Ceasefire deal. Lakini ukiangalia kwa jicho la umakini, utagundua U.S kwa wiki kadhaa amekuwa reluctant/kusita sita kufanya mashambulizi Iran. Jet imeshushwa chini, Iran bado kavimba hapo Hormuz. Alitoa siku, badae akaongeza masaa, leo amekubali Ceasefire ya siku 14!!

Masharti 10, anayotaka Iran ni ushindi kwake, kusema Lebanon iwe free maana yake, Iran bado ana nia ya kuendelea kuwa na proxies mashariki ya kati na ni hatari kwa Israel.

Kusema aendelee kurutubisha Uranium maana yake aendelee na mpango wake wa kuunda silaha za nyuklia. Iran bado hajaachana na mpango huo wa miaka mingi. Kumbuka Uranium ndio chanzo cha vita yenyewe. Mzozo wa wayahudi na Iran, ni silaha na uranium.

Kusema aendelee kudhibiti Hormuz, maana yake aendelee kuidhibiti uchumi wa Mashariki ya Kati ambao ni mafuta na gesi. Kuna meli karibia 200 zimetia nanga tuu hapo hakuna kutoka wala kuingia kuchukua gesi na mafuta.

Kuhusu malengo kutimia au lah. Nimeshajibu huko juu. Hayajatimia, lengo la kuondoa utawala na dola ya kiislamu halijatimia. Lengo la kuleta hali ya kutotawalika Iran halijatimia.

Tuwape maua yao wavaa vilemba wa Iran. Wapo smart.
 
Katika masharti yake kasema Lebanon iachiwe huru.
Hilo ni pigo kwa Myahudi. Hapo Lebanon pako kimkakati hasa kivita, Myahudi akilala akiamka macho na masikio yake ni Lebanon na Syria. Myahudi hawezi kubali piga ua, Lebanon iwe free. 😁
Hiyo proposal Israel lazima hataikubali.

Kwanini Lebanoni?
Lebanoni ni mwiba mchungu kwa Israeli sababu ni kwamba, Lebanon ni eneo la kimkakati la waarabu/waajemi kumpiga Myahudi siku za usoni. Kusema Lebanon iwe huru maana yake, Israeli iwe kwenye hatari kubwa sana.
Wapo Hezbolah pale ambao ni Iran backed proxy. Iran kaweweka ndie mfadhili mkubwa wa Lebanon. Na siku Lebanon ikawa na utulivu wa kijeshi na uwezo, basi Myahudi hakuna rangi ataacha kuona. Lebanon kuwa dhaifu ndio almanusra ya Myahudi.

Syria ndio Dameski, kibiblia huko Dameski kumetabiliwa katika zama za Abraham kama ni chuki ijayo dhidi ya Israel. Iran kusema Lebanon iwe free anamlenga Myahudi hapo, maana huko ndio proxies za Iran zimejificha na kujichimbia. Lebanon ikiwa huru, maana yake na Syria itapata utulivu pia. Na lengo la Myahudi ni kuhakikisha hawa watu hawana utulivu, ili washindwe kujipanga, washindwe kutulia kupanga mipango, wawe na hofu, viongozi wao wawe na mchecheto katika siku zao zote. Myahudi ni bingwa wa vita ya saikolojia. Myahudi anamini waarabu/waajemi hawatakiwi kupata utulivu, wawe na mchecheto, hofu na mashaka siku zote. Ndio maana utaona amewekeza sana kwenye ujasusi ili kuharibu mipango yao. Myahudi anaamini, Mwarabu hatakiwi kupata utulivu wa nafsi na maarifa. 😁

Hayo masharti 10, ni masharti ya kimkakati na kama kukiwa na maafikiano ya maandishi, basi U.S inaweza muwia vigumu sana kuja kuwavamia Iran huko badae.

Kama U.S atakubali Lebanon kuwa huru, na Iran irutubishe Uranium, Myahudi atamgeuka na wenda atapigana vita mwenyewe. 😁

Masharti hayo mawili ni pigo kwa Myahudi. Sio ajabu Netanyahu hivi sasa yupo vikaoni na viongozi w juu anakuna kichwa. Iran anataka kuponyoka kwa proposal hiyo. 😁
 
Huna akili kafiri la makafiri.
 
Unadhani pia siku moja jeshi la lebanon likiwa imara litaruhusu huyo proxy wa Iran aendelee kuwepo hapo lebanon? Fikiria pia hilo,maana Israel kama Taifa halina ugomvi na Lebanon kama Taifa..wana ugomvi na hao Hezbolla
 
Unadhani pia siku moja jeshi la lebanon likiwa imara litaruhusu huyo proxy wa Iran aendelee kuwepo hapo lebanon? Fikiria pia hilo,maana Israel kama Taifa halina ugomvi na Lebanon kama Taifa..wana ugomvi na hao Hezbolla

Sidhani mkuu.
 
Unadhani pia siku moja jeshi la lebanon likiwa imara litaruhusu huyo proxy wa Iran aendelee kuwepo hapo lebanon? Fikiria pia hilo,maana Israel kama Taifa halina ugomvi na Lebanon kama Taifa..wana ugomvi na hao Hezbolla
Israel iliishambulia na kuikalia Lebanon kabla hata ya hizbulah kuanzishwa.
 
Eti mossad wa vwawa 😂😂
 
We ndiye mjinga hizo base nani atazitaka tena zimewalinda vipi hao wenye hizo nchi

USA hana ujanja tena Europe kwa sasa wanaelekea kumaliza matatizo na Iran na America sa hivi ameona kuwa karibu na Iran ni bora kuliko kuwa karibu na Israel sababu akiwa karibu na Iran anaweza kubaki hapo Middle East kula pesa za warabu kuendelea kuilinda Israel kuna mcost sana
 
Unajaribu kuleta kile ambacho unatamani kingetokea, Sasa hakija tokea mmebaki na maumivu TU. Vita sio mzuri mkubwa anapo mwonea mdogo watu husimama na mdogo
 
Tupo hapa ,,tusubiri ni Kambi gani ya America itaondoka middle East
 
Unadhani pia siku moja jeshi la lebanon likiwa imara litaruhusu huyo proxy wa Iran aendelee kuwepo hapo lebanon? Fikiria pia hilo,maana Israel kama Taifa halina ugomvi na Lebanon kama Taifa..wana ugomvi na hao Hezbolla
Unatakiwa ufuate mlolongo wa historia. Israel ina ugomvi na LEBANON nzima. 1958 Beirut crisis aliianzisha Israel ili kuivunja Lebanon yenye uchumi mkubwa na yenye nguvu,washukuru mujaheddin wa Hizbollah ndio wameitetea Lebanon
Na kama haujui vita hii waziri mkuu aliliamuru jeshi lisiruhusu Hizbollah wafanye mashambulizi badala yake mkuu wa majeshi akawaunga mkono hizbollah na kuwapa kambi za serikali wazitumie dhidi ya Israel. Hapo unapata picha gani!??
 
jeshi la ardhi ndio muhimili mkuu katika uwanja wa vita.majeshi mengine yoote ni msaada tu. hizo sehemu zoote unaona zinapigwa makombola taarifa zinatoka kwa jeshi la ardhini.
huwezi kukamata maeneo ya adui yako bila ya jeshi la aldhini. labda kama malengo ya vita ni kumtia hasara adui ndio unalipua hovyo.ila kama malengo ni kudhibiti maeneo ya adui lazima upeleke jeshi la ardhi. angalia kinachofanyika rebanoni hii inamaanisha israel anamalengo ya kuchukua maeneo ya nchi hiyo. ila kwa irani wameamua kutiana hasara kwanza ila wakishaamua kwenda kuweka himaya yao lazima jeshi la ardhi nishushwe hapo.
 
Hakuna kitu kama hicho ,wangeanza na ardhi...Hakuna vita ya ardhini anaweza kushinda hata na TZ...Mbona hakupeleka ardhini na akamate maeneo yapi?

Sasa hapo Lebanon kuanzia lini mbona anarudi nyuma ,mzee Hauwezi kupigana na wanajihad vita vya ardhini...Anga na makombora ndiyo nguvu hakuna cha zaidi ...Usidanganye watu ,hata waachie jangwani hawawezi kupigana ..

Jeshi la ardhini kwa dunia ya sasa hakuna nguvu ,hata uwe na silaha za miyonzi ..Pale Vietnam walikimbia .Huko Lebanon wameshindwa mpaka airforce zinawasaidia kulipua majngo 🤣🤣🤣..

Mzee hawezi kushinda na jeshi la ardhini yaani hawezi kupigana hata na Al shabab
 
sasa wewe subili uone timu itakavyoshushwa na kuanza kuivuruga iran kama ilivyofanywa iraq.
narudia tena.jeshi la ardhi ndio baba majeshi yote yaliobaki ni ya msaada na yanafanya kazi kutoka na taarifa zinazotoka kwa jeshi la ardhi.

kama hutaki kaa hivyohivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…