Namuunga mkono mtoa hoja % 💯.
Dira ya 2050 kiuchumu ni porojo kwa ukwapuaji na uuzaji wa rasilimali za Tanganyika kiholela na kwa fujo ya kukomoa na kuifilisi kabisa. Bandari, wamasai, gas, nk.
Maandalizi ya kielimu kwa vijana kuingia katika dunia ya uchumi wa viwanda hakuna.
Nidhamu na huduma ya utumishi Serikalini imeshuka mno tofauti na wakati wa Magufuli na rushwa kupata kwa kasi maofisini.
Matajiri wameachwa wafanye lolote kwenye eneo la Kodi, na kuvunja sheria sababu wanamiliki uchumi.
Niambie hiyo 2050 tunavuka vipi wakati siasa tu ndiyo inayotukuzwa.
Ukifungua taarifa yoyote unakutana na Rais kasema, Waziri kaamua, RC kafukuza jambo ambako sio baya.
Ila tungerudi utaratibu wa zamani, ukifungua vyombo vya habari unakutana na kilimo, uvuvi, ufundi na waelimishaji kadha wa kadha