Ni mkakati wa kumuangusha Rais Samia kisiasa?

Nakumbuka ibara hiyo ya 15 sijui kama nimeinukuu vizuri ndio iliyoanza kuleta uzembe makazini Serikalini na kwenye mashirika ya Umma !
Unyapara ni lazima uwepo makazini ndio kazi zitafanyika kwa ufanisi !!
Ninakuelewa unachoandika hapa, lakini hicho kifungu unakinakiri kwa makosa.

Maana ya kifungu hicho haikuwa kutetea uzembe kazini, lakini kama ilivyo kwa mambo mengi ambayo watu hawakuelewa malengo yake yalikuwa yapi, hapa nawe unashiriki (najua siyo kwa maksudi yako) katika upotoshaji huo.

Wafanya kazi kunyanyaswa kazini haina maana ndiyo ufanisi wa utendaji kazi utaongezeka.

Baada ya kuyaeleza haya mkuu 'mzeewaSHY', usinishangae nami nikisema kuwa kwa hali tuliyo nayo hapa nchini katika maeneo mengi, tunachohitaji ni DIKTETA mmoja mwenye uzalendo, na mtu aliye na akili tulivu kuliko Magufuli.

Tabia za waTanzania zinaonyesha dhahiri kuwa aina ya mtu wa namna hiyo anahitajika sana iwapo Tanzania itaweza kupiga hatua mbele kimaendeleo.
WaTanzania wengi ni watu wanaopenda kusukumwa sukumwa sana ndipo waweze kustuka kufanya mambo.

Ndiyo maana CCM imetumia udhaifu huo wa wananchi wetu kujimilikisha kila kitu, ikiwa ni pamoja na watu hao hao (raia wasiostuka kwa lelemama).
 
Ni kweli Mkuu Kalamu nia ya ile ibara ilikuwa ni nzuri sana na ilikuwa ya kiungwana sana lakini mapokeo yake ndio yalileta kizaazaa makazini !

Maoni yako naunga mkono 100 %
 
8. Kuongezeka maradufu kwa matumizi ya serikali bila kuongeza tija...hii ni pamoja na upanuzi wa Baraza la mawaziri pamoja na uwepo wa tume nyingi zinazozunguka bila matokeo ya utendaji wa tume hizo kuonekana kuleta mabadiliko kwa umma.
.... hapa!
 
Umeona jinsi ulienda kupoteza muda kugombea nafasi za 2 wa EALis A kwa kujufanya mzalendo, kumbe wenzio wanapitishiwa gate la uani.2
Giving a try on anything sio kupoteza muda but getting experience, kiukweli hili la EALA, Tanzania tumebugi step big time.

Japo CCM ndio chama chetu pekee, kwa baadhi ya mambo kinachotufanyia sisi Watanzania, mfano ilichotufanya Bunge la EALA, kitalaaniwa!. Kimewaacha some real good people, kika chagua baadhi ya makokoro!. Nilitoa ushauri mzuri kwa chama changu Ubunge EALA, Wito Kwa CCM, Msiangalie Ukwasi, Tuteulieni, Wazalendo wa Kweli wa Taifa Hili, Wenye Uwezo na Uzoefu wa Kimataifa Kutuwakilisha Ipasavyo hilo kokoro lina kisu kikali!.

Kitu cha ajabu kabisa CCM ikapeleka majina 8 Bungeni, hivyo kazi ya Bunge ni kupitisha tuu na sio Bunge kufanya uchaguzi! Lijue Bunge la Afrika Mashariki na Jee Uchaguzi wa Wabunge wa CCM EALA Ulikuwa ni Uchaguzi Kweli Au Kiini Macho cha Uchaguzi?

Ndipo kuna mtu akanishika sikio kuhusu hilo kokoro, nilibaki mdomo wazi!.
P
 
Huyu rais nilipomuona na yule jambazi Rostam wakifunga mkataba basi nilikata Tamara.
 
Ina maana ndio umejulia hiyo michezo hapo? Hata hivyo sikuona haja ya ww kuhariri post yangu na kuweka maneno ambayo sio yangu. Post yangu namba 57 iko wazi bila hayo maneno uliyoongeza.
 
Ina maana ndio umejulia hiyo michezo hapo? Hata hivyo sikuona haja ya ww kuhariri post yangu na kuweka maneno ambayo sio yangu. Post yangu namba 57 iko wazi bila hayo maneno uliyoongeza.
Sorry it was mistaken typo.
P
 
Rais hana uwezo wa kuongoza nchi.
 
You nailed it
You nailed it so efficiency

Mheshimiwa Rais kazungukwa na waeuliwa wenye nia isiyo njema kwake.

Avunje BMW ateue upya hajachelewa.
 
Hili nalo watalitizama
 
Rafiki wa Mfanyabiashara ni Mfanyabiashara pia na Rafiki wa mwizi ni mwizi pia.
Mama ameamua kujenga urafiki na wezi!
 
Yy SAMIA kama ni mvivu wa kujua shida za wananchi ni Uzembe wake na ndio uwezo wake umeishia hapo.
 
Lakini mkuu kumbuka wengi wa mawaziri waliopo na wabunge waliopo aliwakuta?
Kwani hana nguvu ya kubadilisha mawaziri wote na kuweka wapya?....Kama anayo, je hoja yako inakujaje hapa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…