Ni mkakati wa kumuangusha Rais Samia kisiasa?

Ni mkakati wa kumuangusha Rais Samia kisiasa?

Rais huyu ni wa mpito kaja kwa bahati mbaya, amalize kipindi cha mpito aondoke 2025, hana tofauti na Joyce Banda wa Malawi. Mnalazimisha awe mgombea wa CCM 2025 kwa kipi hasa?
Ila yeye ni Mwenyekiti wa CCM kwa sasa mkuu....
Top tier party owner for the time being... unadhan nani anaweza mfanya kitu bila kumsaidia asivurunde?
 
Kuna mambo yanaendelea nchini unajiiza hizi Habari kwanini zinatoka sasa bila maelezo?

Mawaziri viburi na majibu ya rejareja kwenye mambo mazito yanayohitaji utulivu wa akili.

Mambo haya yafuatayo yanamfanya Rais aonekane anatoa maelekezo kwa manufaa ya wachache wasio na uchungu na taifa hili hata kidogo.

Kitu ambacho ni uhakika pengine Rais lazima asisitiziwe na wasaidizi wake ni kwamba Tanzania ni nchi masikini na watu wake ni masikini mno.

Karibu asilimia 50% ya watanzania wote wanaishi chini ya USD 2 kwa siku.... hawa watu lazima maamuzi yeyote yawe yanawazingatia sana.

Habari zifuatazo zitamchafua sana Mh Rais kuelekea uchaguzi mkuu wa 2024/25.

1. Nyongeza ya karibu 40% ya Mishahara ya wabunge? Kulikuwa na haja gani kufanya jambo hilo sasa?

2. Kupanda bei za nishati ya mafuta na kuadimika bila maelezo yanayojitosheleza, awali ilisemekana ni kukosekana kwa $ sasa imegeuka imekuwa kupanda bei kwenye soko la dunia... bado shutuma hizi zinaelekezwa kwa teuzi za Mh Rais kwamba mume wa Spika anaesimamia EWURA wanakula njama na wafanyabiashara. (Rejea hotuba ya Mbunge Tabasam bungeni iliyozimwa na Spika?)

3. Kukatika umeme bila maelezo wala taarifa za kutosha nchi nzima.( Watu wanajiuliza Magufuli aliwezaje? Kalemani alifanyq kitu gani? Majibu hayatolewi.

4. Kuna mgao wa maji unaotarajiwa kuanzia wiki ijayo maeneo ya Dar, Arusha na Tabora....

5. Kuondoa Bima za Afya kwa watoto kwa kisingizio cha gharama, huku NHIF wakilipana posho na Mkopo binafsi na matumiz mabaya ya kias cha zaid ya 129B bila maelezo yakueleweka.(Report ya CAG)

6. Kuongezeka matamasha na warsha nchi nzima bila kutatua matatizo halis ya wananchi wa kipato cha chini.

7. Miradi ya kilimo isiyomnufaisha mkulima wa kijijini moja kwa moja.., kama BBT, Kumbuka kilimo ni maisha ya watu huko kijijini na sio agenda.

8. Kuongezeka maradufu kwa matumizi ya serikali bila kuongeza tija...hii ni pamoja na upanuzi wa Baraza la mawaziri pamoja na uwepo wa tume nyingi zinazozunguka bila matokeo ya utendaji wa tume hizo kuonekana kuleta mabadiliko kwa umma.

9. Kudumaa kwa demokrasia, kulinganisha na Mwaka mmoja wa utawala wako..., hisia zinatawala ukwel kuliko uhalisia, mfano... Katiba mpya nk.

10. Kaa la moto la DP world, na shutuma za Rushwa ambazo hazijajibiwa kwa ufasaha hadi leo.

11. Kuna hili la Cartels (madalali biashara) kuwepo kila kona ya mambo yanayohusu maslahi ya nchi moja kwamoja, ikiwemo mafuta, Gas nk.

Mtiririko wa haya mambo ni mrefu sana, lakini watendaji wako walikuwa na nafasi kutafuta ukwel na kuuweka hadharani au hata kwenye baadhi ya mikutano ya Chama kwa ajili ya ufafanuzi.

Namsikitikia Mh. Rais kwamba pengine wasaidizi wake aliowaamini hawamsaidii ipasavyo??
Hayo yote yaliaanzia baada ya Nyerere kupewa nchi na Waingeraza, huku ikiwa na uchumi sawa na Korea ya Kusini(Sio kwa kiduku).
Yaliyobaki ni muendelezo wa somo la historia....
 
Na pia kumekuwa na uminyaji mkubwa wa uhuru wa kujieleza pamoja na kuzuia uhuru wa kuhabarishwa.

Sasa hivi vyombo vyote vya habari vinafanya na kutenda kwa maelekezo kutoka juu serikalini.na hivyo kulaximishwa kutoripoti habari youote ambayo ni opposed kwa serikali ya Samia.

Pia Uhuru wa kufanya siasa za majukwaani umeanza kuzimwa kwa nguvu mpya kupitia jeshi la Polisi.
Mifano hai ni Loliondo na Ngorongoro kisha karatu hivi karibuni.

Rais kukaa kimya huku zikiwa zimevuja habari na Documents zinazoonyesha mwanae akitajwa kijusika kwenye miamala ya kibadhirifu.kupitia malipo ya tenda za polisi.
Hili ni Doa kubwa sana kwake Rais.

Ukiongezea na ile kashfa ya mabilioni ya likosi kazi cha serikali kule Barrick Gold kupitia Acacia mining....
Kwa kweli Mh Rais atafika 2025 amechafuka sana!

Uko sahihi kwenye maelezo yako, lakini unayosema hapa yalifanyika sana kipindi Cha dhalimu na ulikaa kimya. Huna uhalali wa kumkosoa huyu, mama, acha waseme wengine sio ww.
 
Ila yeye ni Mwenyekiti wa CCM kwa sasa mkuu....
Top tier party owner for the time being... unadhan nani anaweza mfanya kitu bila kumsaidia asivurunde?
CCM haiwezi kuwa na aina hio ya mgombea tambua hilo usione watu wako kimya. Akiwa na akili za mbali ajiandae kuondoka 2025.
 
CCM haiwezi kuwa na aina hio ya mgombea tambua hilo usione watu wako kimya. Akiwa na akili za mbali ajiandae kuondoka 2025.
Naweza kukuelewa kuwa Kuna mkakati wa maksudi ashindwe..

Mfano mgogoro wake na Kanisa kuhusu DP world... more of a man made than a natural conflict by any intellectual concept.
 
Hayo yote yamepewa baraka na huyo mama yenu mzigo kwa Taifa..mnajitahidi kumsafisha aonekane mwema eti anaharibiwa ama kushauriwa vibaya kitu ambacho si kweli, anajifelisha yeye mwenyewe kwa kushindwa kusimamia misingi bora ya Uongozi.

Acha tuisome namba ili tuje kuwa mfano kwa vizazi vijavyo kwa maamuzi yetu mabaya na mabovu dhidi ya ulinzi wa Taifa na Rasilimali zake.
Ni noma
 
SERIKALI YA RAIS SAMIA YASHIRIKIANA NA KAMPUN YA DAISY GENERAL TRADERS KUKWAPUA MABILIONI FEDHA TOKA BANK KUU.

4/9/2023: 21:30 HRS Western Indiana.

Taarifa kutoka ndani ya kitengo cha Financial Intelligence Unit (FIU) zinatujuza kama ifuatavyo.

Genge la walafi na wakwapuaji Fedha za walipa kodi likiongozwa na Angela Kiziga, Abdluhalim Hafidh Ameir na Hamad Massaun Yusuph linaifilisi nchi.
Duh...!.
P
 
Namsikitikia Mh. Rais kwamba pengine wasaidizi wake aliowaamini hawamsaidii ipasavyo??
Duh!

Andiko lote lile ulilotumia umakini mkubwa kuliwasilisha, halafu mwishoni unakuja na mstari wa ajabu sana kama huo?

Mbona ni kama umefuta yote uliyoandika huko mwanzo?
 
Genge la walafi na wakwapuaji Fedha za walipa kodi likiongozwa na Angela Kiziga, Abdluhalim Hafidh Ameir na Hamad Massaun Yusuph linaifilisi nchi.
Hawa watu ni kama nilishasoma majina yao mahala fulani...; huyo mmoja mwenye majina ya kiarabu, siyo yule mwenye mradi wa umeme wa Solar anaoshirikiana na yule Dikteta wa Uganda kuujenga?

Ngoja nitafute kumbukumbu zangu kidogo!
 
That you believe someone outthere is genuinely concerned with your daily worries..... !!! Then you need to rethink again !!!
 
Screenshots_2023-09-17-04-57-30.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo yote yamepewa baraka na huyo mama yenu mzigo kwa Taifa..mnajitahidi kumsafisha aonekane mwema eti anaharibiwa ama kushauriwa vibaya kitu ambacho si kweli, anajifelisha yeye mwenyewe kwa kushindwa kusimamia misingi bora ya Uongozi.

Acha tuisome namba ili tuje kuwa mfano kwa vizazi vijavyo kwa maamuzi yetu mabaya na mabovu dhidi ya ulinzi wa Taifa na Rasilimali zake.
Ongezea na vijana wa kanisani pia hawamtaki ndio maana madili ya kitapeli yanafichuliwa mda huu na bado kuna madudu yanaachiliwa zaidi
 
Mama anajimaliza mwenyewe, tusilaumu wengine, mfano mdogo tu alivyo mshushua mwananchi aliyetaka kumueleza duku duku lake siku ya jana ziarani, nadhani kitendo kama hiki amekifanya mara ya pili sasa.

Kuna muda mambo madogo madogo kama hayo yanaweza kufanya wananchi wakaona uko mbali nao.

NakumbuKa niliwahi kutoa ushauri kwenye dawati la siasa jinsi Mama anavyoweza kuwa karibu na wananchi na jinsi anavyoweza kutumia ukaribu huo kama mtaji wa kisiasa cha ajabu niliishia kupewa karipio.
wengine hatukuwepo kwenye mkutano. alimshushua je?
 
Lakini mkuu kumbuka wengi wa mawaziri waliopo na wabunge waliopo aliwakuta?
Lakini alikuwa na uwezo wa kuwabadili wote na hata sasa anaweza !!
Aliharibu sana pale alipo watangazia wateule wake kwamba hapendi mambo ya kufukuzana fukuzana katika Kazi !!
Bila kuwepo na nidhamu ya uoga Nchi hii mambo hayaendi !!
Hata katika kipindi cha Nyerere ipo ibara mojawapo ya muongozo wa Ccm inayosema Kiongozi asiwe mnyapara bwanyenye mkaripiaji mpenda makuu
Nakumbuka ibara hiyo ya 15 sijui kama nimeinukuu vizuri ndio iliyoanza kuleta uzembe makazini Serikalini na kwenye mashirika ya Umma !
Unyapara ni lazima uwepo makazini ndio kazi zitafanyika kwa ufanisi !!

Mwamba alianza kuinyoosha njia ya mafanikio lakini Mungu akawa amempenda zaidi akamtwaa ! 🙏🙏
 
Kuna mambo yanaendelea nchini unajiiza hizi Habari kwanini zinatoka sasa bila maelezo?

Mawaziri viburi na majibu ya rejareja kwenye mambo mazito yanayohitaji utulivu wa akili.

Mambo haya yafuatayo yanamfanya Rais aonekane anatoa maelekezo kwa manufaa ya wachache wasio na uchungu na taifa hili hata kidogo.

Kitu ambacho ni uhakika pengine Rais lazima asisitiziwe na wasaidizi wake ni kwamba Tanzania ni nchi masikini na watu wake ni masikini mno.

Karibu asilimia 50% ya watanzania wote wanaishi chini ya USD 2 kwa siku.... hawa watu lazima maamuzi yeyote yawe yanawazingatia sana.

Habari zifuatazo zitamchafua sana Mh Rais kuelekea uchaguzi mkuu wa 2024/25.

1. Nyongeza ya karibu 40% ya Mishahara ya wabunge? Kulikuwa na haja gani kufanya jambo hilo sasa?

2. Kupanda bei za nishati ya mafuta na kuadimika bila maelezo yanayojitosheleza, awali ilisemekana ni kukosekana kwa $ sasa imegeuka imekuwa kupanda bei kwenye soko la dunia... bado shutuma hizi zinaelekezwa kwa teuzi za Mh Rais kwamba mume wa Spika anaesimamia EWURA wanakula njama na wafanyabiashara. (Rejea hotuba ya Mbunge Tabasam bungeni iliyozimwa na Spika?)

3. Kukatika umeme bila maelezo wala taarifa za kutosha nchi nzima.( Watu wanajiuliza Magufuli aliwezaje? Kalemani alifanyq kitu gani? Majibu hayatolewi.

4. Kuna mgao wa maji unaotarajiwa kuanzia wiki ijayo maeneo ya Dar, Arusha na Tabora....

5. Kuondoa Bima za Afya kwa watoto kwa kisingizio cha gharama, huku NHIF wakilipana posho na Mkopo binafsi na matumiz mabaya ya kias cha zaid ya 129B bila maelezo yakueleweka.(Report ya CAG)

6. Kuongezeka matamasha na warsha nchi nzima bila kutatua matatizo halis ya wananchi wa kipato cha chini.

7. Miradi ya kilimo isiyomnufaisha mkulima wa kijijini moja kwa moja.., kama BBT, Kumbuka kilimo ni maisha ya watu huko kijijini na sio agenda.

8. Kuongezeka maradufu kwa matumizi ya serikali bila kuongeza tija...hii ni pamoja na upanuzi wa Baraza la mawaziri pamoja na uwepo wa tume nyingi zinazozunguka bila matokeo ya utendaji wa tume hizo kuonekana kuleta mabadiliko kwa umma.

9. Kudumaa kwa demokrasia, kulinganisha na Mwaka mmoja wa utawala wako..., hisia zinatawala ukwel kuliko uhalisia, mfano... Katiba mpya nk.

10. Kaa la moto la DP world, na shutuma za Rushwa ambazo hazijajibiwa kwa ufasaha hadi leo.

11. Kuna hili la Cartels (madalali biashara) kuwepo kila kona ya mambo yanayohusu maslahi ya nchi moja kwamoja, ikiwemo mafuta, Gas nk.

Mtiririko wa haya mambo ni mrefu sana, lakini watendaji wako walikuwa na nafasi kutafuta ukwel na kuuweka hadharani au hata kwenye baadhi ya mikutano ya Chama kwa ajili ya ufafanuzi.

Namsikitikia Mh. Rais kwamba pengine wasaidizi wake aliowaamini hawamsaidii ipasavyo??
Wanacheza na mentality yake tu..viongozi wa chini huwa wanaangalia wa juu anataka nini au anafurahishwa na nini au hajali nini.

Ndio maana kuna watu waliibuka kuitetea dp world baada ya kuona mkubwa wao ana influence nayo..kanyamaza nao wamenyamaza.

Hakuna kinachofanyika ye asijue..sema focus yake sio kuongoza nchi..focus yake ni kuwa rais basi.

She fights for the title not leadership. Kwa nini sababu ameshajua hawezi leadership.

Ndio maana hawapendi hata best performers au watu wanaoonekana watamu outsmart yeye..

Sent from my SM-A225F using JamiiForums mobile app
 
Mama anajimaliza mwenyewe, tusilaumu wengine, mfano mdogo tu alivyo mshushua mwananchi aliyetaka kumueleza duku duku lake siku ya jana ziarani, nadhani kitendo kama hiki amekifanya mara ya pili sasa.

Kuna muda mambo madogo madogo kama hayo yanaweza kufanya wananchi wakaona uko mbali nao.

NakumbuKa niliwahi kutoa ushauri kwenye dawati la siasa jinsi Mama anavyoweza kuwa karibu na wananchi na jinsi anavyoweza kutumia ukaribu huo kama mtaji wa kisiasa cha ajabu niliishia kupewa karipio.
Tena kuwajibu vile wananchi ndio kunafanya hao viongozi wake wazidi kulala na kupuuza matatizo ya wananchi..sababu wanajua wananchi hawana pa kwenda kulalamika.

Cha ajabu utaona 2025 akitafuta kula atajifanya kujibu hizo kero ambazo leo hataki kujibu..wanazindukaga kumekucha.

Sent from my SM-A225F using JamiiForums mobile app
 
Duh...!.
P
Inaendelea hapa (jana ilikuwa bodini moderator akaitoa):

Mama Samia aliruhusu malipo hayo yafanyike kwa kampuni hiyo na ongezeko zaidi kwani kampuni hiyo badala ya kulipwa tsh Bil 10.9 sasa imelipwa tsh Bilioni 21.9 na chanji inabakia.

Pesa hizo zililipwa katika akaunt namba 01530390577600 CRDB, mali ya DAISY GENERAL TRADERS kwa mafungu mawili ambapo tarehe 25/3/2023 akaunt tajwa ilipokea kiasi cha tsh Bilioni 2,737,986,111.86 na baadaye kiasi cha tsh 19,223,257,320.00 hivyo kukamilika kiasi cha tsh Billion 21,961,243,431.86.

Hata hivyo kampuni ya DAISY GENERAL TRADERS ilipata tender Wizara ya Mambo ya ndani kutengeneza sare za jeshi kwa gharama ya kiasi cha tsh Bilioni 10 na baada ya kuchelewesha inaonyesha fedha hizo zilizuiliwa kulipwa.

Katika Mazungumzo ya wamiliki wa kampuni ya DAISY GENERAL TRADERS ambao ni Angela Kiziga na Elvis Peter Kilango na Serikali waliomba kulipwa ongezeko la tsh milioni 900 ambazo zilikuwa ni kwa ajili ya kodi na wakakubaliana hivyo. Jumla walistahili kulipwa kiasi cha tsh bilion 10.9. Cha kushangaza ni namna mgao na malipo yalivyofanyika. Baada ya kiasi cha tsh Bilioni 21,961,243,431.86 kuingizwa kwenye akaunt no 01530390577600 CRDB mali ya DAISY GENERAL TRADERS inayomilikiwa na Angela Kiziga na Elvis Peter Kilango mgao ulikuwa kama hivi.

Bwana Elvis Peter Kilango inaonyesha ana akaunti no 2012322 mali yake binafsi katika Bank ya ABSA BANK TANZANIA. Ambapo sasa hapo ndio mchezo ukaanza.

Akaunt No 2012322 mali ya Elvis ikaanza kupokea miamala kama ifuatavyo.

Tarehe 30/3/2023 ilipokea kiasi cha tsh Bilioni 7
Tarehe 5/4/2023 ilipokea kiasi cha tsh Bilioni 8
Tarehe 12/4/2023 ilipokea kiasi cha tsh bilion 4.9

Mpaka hapo ukipiga hesabu utaona akaunti hiyo binafsi iliingiza Jumla ya kiasi cha tsh Billion 19.9

Mgawanyo mwingine ukaendelea kwa watu binafsi sasa.

Elvis Peter Kilango alijiingizia kiasi cha tsh bilion 4,769,200,000.00
Elvis akalipa fedha kwenda kwa KARMJRR JIVANJEE LTD tsh 83,132,485.00
Malipo kwenda TOYOTA TANZANIA LTD tsh 389,161,125.00
Malipo kwa anayedhaniwa ni Mbunge ndugu LIVINGSTON JOSEPH LUSINDE tsh 10,000,000.00
Malipo kwa VELVE AUTO INVESTMENT tsh 103,776,974.00
Malipo kwa HANDCRAFT NISSAN LTD tsh Bilioni 1,061,658,000.00
Malipo kwa Paul Joseph Meela tsh Bilioni 5,000,000,000.00
Malipo kwa SANGAM INDIA LTD tsh 493,616,833.00
Malipo kwa TAJ EDGE COMPANY tsh 201,835,693.00
Malipo kwa HEAVENLIGHT EDWARD KAVISHE tsh 141,000,000.00.

Ikumbukwe ABDULHALIM HAFIDH AMEIR ni kijana pendwa wa Mama Samia anayedhaniwa kumuongoza Rais kwa kuwaondoa serikalini watu wanaopingana naye.

ANGELA KIZIGA ni Swahiba na shosti wa Rais Samia na ni Mbunge wa Afrika Mashariki aliyepitishwa Bungeni bila hata kufanya interview katika chama.
THANIA ALI ABDULA ni mke wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi ambaye naye kwenye orodha ya wizi huu yumo.
Paul Joseph Meela ni shemeji yake na Mwigulu Nchemba yaani kaka wa mke wa Waziri wa Fedha.

Wengine tutawaletea mahusiano hayo taratibu.

Hata hivyo mgawanyo haukukomea hapo soma hapa chini utaona.

Tarehe 19/4/2023 ABDULHALIM HAFIDH AMEIR aliingiziwa kiasi cha tsh milioni 500,000,000,00.
Tarehe 19/4/2023 THANIA ALI ABDULA aliingiziwa kiasi cha tsh milioni 500,000,000,00 (mke wa Waziri wa Mambo ya Ndani ndgu Masauni na mtu wa karibu na Rais Samia)
Tarehe 5/5/2023 ndugu ABDULHALIM HAFIDH AMEIR aliingiziwa kiasi cha tsh milioni 500,000,000.00
Tarehe 9/5/2023 ndugu ANATORI NYAKI aliingiziwa tsh 500,000,000.00
Tarehe 9/5/2023 ELVIS PETER KILANGO alijiingizia kwenye Akaunti yake kiasi cha tsh Bilioni 3,676,000,000.00
Tarehe 15/5/2023 ndugu YASSIR KAROUB SEIF aliingiziwa kiasi cha tsh 300,000,000.00
Tarehe 15/5/2023 THANIA ALI ABDULA aliingiziwa kwenye akaunt yake tena tsh 200,000,000.00
Tarehe 22/5/2023 ABDULHALIM HAFIDH AMEIR tena akaingiziwa kiasi cha tsh milioni 120,500,000.00

Kwa mgawanyo huo utaona kama ifuatavyo.
1. ABDULHALIM HAFIDH AMEIR amelipwa kiasi cha tsh Bilioni 1,120,500,000.00
2. Bi THANIA ALI ABDULA amelipwa kiasi cha tsh milioni 700,000,000.00
Hawa wote sio watumishi wa Umma na haijulikani wamefanya biashara gani na Serikali.
Kama mama Samia hahusiki ni vyema asimame na kuwakamata wahusika wote wa jambo hili.

Hata hivyo akaunt no 0152673620900 CRDB mali ya THANIA ALI ABDULA ndio iliyopokea pesa zote ambazo mke wa Waziri wa Mambo ya Ndani alilipwa na yeye kuzigawa kama ifuatavyo.

Tarehe 27/4/2023 THANIA ALI ABDULA alimuingizia ndugu ALI JAFAR SHAURI kiasi cha tsh 100,000,000.00
Tarehe 5/5/2023 alitoa cash yeye mwenyewe kiasi cha tsh milioni 170,500,000.00
Tarehe 10/5/2023 alimuingizia pesa ndugu HAMAD MASAUN YUSUPH (mumewe) kiasi cha tsh milioni 80,000,000.00.

Hapo tunamaanisha kazi iendelee ni pamoja na hayo yote?

Nchi imeshindikana hii.

Ni mimi Mghaibuni toka Ughaibuni kunako haki na kweli naendelea kuwajuza.
 
Back
Top Bottom