Ni Mkatoliki 100% ila hizi ni sababu zangu za kwanini Sihudhurii na Sitohudhuria Jumuiya za kila Jumamosi....

Hao wote mnasema ni wakatoliki nyie sio maana tayari mmesha hasi kanisa.

Moja mmekataa kwa hiari yenu kushiriki jumuiya na sala zingine za vikundi(vyama vya kitume) lakini pia kanisani hamuendi, ila mnataka mzikwe na huduma ya kanisa.

Kanisa ni la walio hai na sio wafu hivyo shiriki ukiwa hai ili ukifa waamini wakusindikize kwa maombi.

Pia jumuiya yako hayo majungu sijui kutongozana sioni maana yeyote zaidi ya uongo maana sala ni dakika 45. Baada ya sala watu wote wanaondoka tena saa 12:00 asubuhi wanatongozana wapi.

Kama wanaweza kwemda wote kanisani, vikoba vya mtaa, wanakutana kila siku mtaani Jumuiya haiwezi kuwa chanzo maana wanakutana mara nyingi zaidi kwenye mambo mengine kuliko huko kwemye jumuiya.

Kuhusu michango, ni kweli ipo kwenye jumuiya kama sehemu ya kuendeleza kanisa. Lakini jumuiya zenye sadaka nzuri hakuna haja ya michango.

Mwisho huna hoja ya kutokwenda jumuiya zaidi ya uvivu, ulegevu wa iman, ulembukeni wa imani na kutaka kujusfy upungufu wako.
 
Kuna jirani alikua hajatoa michango ya jumuia....sasa christmass kuna mwanajumuiya akatoa 🐐 wale wanaume wa jumuiya akaomba katika list ya watakaoenda kuiandaa na kuchinja wamhesabu....wakamtema...wakamwambia hujachanga michango una gaps kibao...since then ...🙌
 
Amri ya Kanisa inasema SAIDIA KANISA KATOLIKI KWA ZAKA..
hizo mambo zingine zinatoka wapi?
Wenzetu ulaya hata hiyo sadaka ya katikati ya misa hawatoi.. Kwa sababu Zaka ina fanya kila kitu..

Huku michango michango michango
Neno zaka limeongezea ila kulingana na tafsiri ya kiingereza inasema "You shall help to provide for the needs of the church"
 
Jiandae kukalipiwa na wenzio
 
mkuu kama ujapiga kitu dry na mixer huwa unaandikaga vitu vya msingi
 
Sidanganyi sina jumuiya hata moja. Si hapa nilipo hata nilikozaliwa. Ninachohisi sitazikwa kijumuiya ila itabidi wanizike kimkatoliki kama watapendezewa. Wasipopendezewa basi nitazikwa na sapuri yangu ya mama Maria na mtakatifu Shaber ambaye ndiye mtakatifu wa mwisho kuzuru.
 
Ujenzi wa ukumbi
Ujenzi wa shule
Birthday yaPengo
Radio maria
Radio Tumaini
 
Mkuu umenichekesha, we kauzu Kama Mimi muda mwingine
 
Ww nae akili ndogo aisee!!! Ukisha kufa hauna kitu cha ziada.. kwani ukizikwa vzr unapata faida gn ww marehemu?

Ukisha kufa utazikwa tu na hata usipo zikwa harufu watapambana nayo wenyewe.

Ww ni mtumwa wa kidini na muoga wa kifo, nakwambia utakufa tu Kama sisi tutakavyo kufa. Hata uzikwe vp na sisi tuzikwe na manispaa sote ni wafu tu na tumefukiwa.

Nakushauri toka utumwani na uishi maisha yanayokupendeza ww
 
Mimi ni Mwenyekiti wako wa Jumuiya,malalamiko yako nimeyapokea nitayafanyia kazi.Lkn nakuomba kwa moyo radhi Kabisa njoo Jumuiyani tusali Pamoja,changamoto hizo tutazitatua.
 
Hiyo ya 4 Dr. GENTAMYCINE
nimeipenda
 
Jumuia nyingi, siku ya Jumuia ya Jumamosi, Muda wa sala ni mdogo saana ukilinganisha muda wa kushughulikia michango!
 
Labda jumuiya yenu
 
Kanisa ni nini? ukatoliki ni nini? Na imani ni nini?..Nipe tofauti ya hivi vitatu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…