Ni Mkatoliki 100% ila hizi ni sababu zangu za kwanini Sihudhurii na Sitohudhuria Jumuiya za kila Jumamosi....

Binafsi naudhika na matumizi mabaya ya mapato ya kanisa. Mapadre ni vimwana na ulevi mtindo mmoja. Hayo ya kutozikwa yanatekelezwa hata kwa wanao sali. Msiba wa rofa misa ina endeshwa na katekista, wa tajiri mapadri ni wahudumu, askofu anaendesha ibada.
 
Nachoka kila Siku tu kuwapeni Ufafanuzi kuwa Mimi siitwi huyu Tapeli wa ID na Mpuuzi GENTAMYCIME aliyeiiga ID yangu ili Kusafiria Nyota yangu Kali ya Kiumaarufu hapa Jamiiforums bali naitwa GENTAMYCINE.

Kwanini huwa hamuelewi tu? Nimejiunga hapa Jamiiforums mwaka 2013 Mwezi July na hili Juha lililoiga ID yangu limejunga mwaka huu huu wa 2022 je, hamwoni hiyo tofauti?
 
Amina Mkuu.
 
Afu wanadai eti michango ni ya Mungu? Hawa ni wafanyabishara kama wengine tu! Afadhali Hela yangu ya sadaka nimpe yatima au mlemavu barabarani sio haya mambo ya kanisani....kanisani ilipaswa kusiwe na sadaka kabisa.
Umeandika Kitu cha Kiakili mno ila tegemea Majuha wa Kiimani ndani ya Kanisa / Makanisa kuja Kukupinga kwa hili na hata Kukushambulia pia.

Wenye Akili Kubwa na zilizobarikiwa tumekuelewa vizuri sana tu Mkuu / Kiongozi.
 
Yaani hili POPOMA nimezaliwa nalo hospitali moja, ila popoma leo umeongea point, eti wana mikwara ukifa hawakuombei
 
Tafuta hela ,ukiwa na hela hukosi wa kukuzika watajaa hata wasiokujua ,wapenda kula mtaani watajaa kwenye mahema.Huo ni utaratibu was duniani Mungu hausiki nao
Hakika Mkuu na nimeliona hili mahala.
 
Mimi Binti wa Mwenyekiti wa Jumuiya yangu Nimembandua na alivyojua akaanza Kunichukia cha Kushangaza tena huyo huyo akiniona akiwa na wana Jumuiya ananisalimia Kikatoliki Tumsifu Yesu Kristo na kujifanya ananihimiza nihudhurie Jumuiya hivi huu kama siyo Unafiki Uliotukuka ni nini?
 
sawa,hiyo ni jumuiya yako mkuu. Umechukua hatua gani kusaidia hili ?Tatizo halikimbiwi na inawezekana wewe ndiye wa kusaidia kuirudisha jumuiya kwenye mstari wa unyoofu.
GENTAMYCINE nasomwa mno na Watu Wakubwa na Muhimu ( tena wa Kada mbalimbali ) hivyo nina uhakika Watu Kanisa Katoliki hasa Katibu Mkuu wa TEC Mwalimu wangu wa Media Law na aliyekuwa pia Vice Chancellor wangu SAUT Mwanza 2006 hadi 2009 Genius Fr. Dkt. Charles Kitima.

Pia na Mwalimu wangu Mpendwa aliyeniambukiza Ujiniasi wake Uliotukuka na aliyenifundisha Print Media na Somo lake pendwa la Critical and Logical Thinking ( sasa Askofu Mkuu Jimbo la Kondoa Mkoani Dodoma ) Dk. Bernadine Mfumbusa kwa pamoja watakuwa wameuona huu Uzi wangu Mwanafunzi Wao GENTAMYCINE na watayafanyia Kazi kwa Niaba ya Kanisa langu Takatifu la Katoliki.
 
Nini ni ulevi kama ulevi mwingine
"Nini"
Wale hawarekebishiki atakaloamua kiongozi ndio hilohilo,
 
Kuna ULAZIMA gani na upi kuzikwa na ibada? Ina maana hiyo ibada itasaidia nini? Itafuta dhambi zako? Ibada ni Hofu za kidini na kiimani tu! Ukisha kufa umekufa hakuna anaye jua huko uliko nini kina endelea.
Huwa nafurahi na napenda mno Kusoma Maoni ya Watu Werevu ( Intelligent ) kama Wewe hivi hapa Jamiiforums. Hongera Mkuu.
 
We bwana kitu Kama huwezi waachie wanao weza. Wengine apa tunahudhuria jumuiya kwa burudan kabisa. Au hiyo jumuiya yenu ndio ina shida nahisi. Jaribu kuchunguza
 
Safi sana huwa napenda Watu 'Defiant' kama Wewe Mkuu. Na najua Walikukoma pia.
 
Mkuu huwezi amini Nimecheka mpaka basi kwa hii post yako na kila nikiikumbuka tu najikuta naangua Kicheko tu. Hakika Jamiiforums ni raha mno na Burudani tosha.
 
Sawa Baba Askofu ila najua Sindano yangu ya Leo imewaingieni vyema tu na najua mtayafanyia Kazi haya yote ambayo GENTAMYCINE nimetiririka na kuserereka nayo Kwenu.
 
Kwani Buji na Genta ni ndugu moja?!mbona kama kuna sehemu mmejichanganya hivi .......
Tunajuana kwakuwa huwa tunalewa Kiwanja Kimoja na Kugombania Mabaamedi wa Sinde Pub Mbezi Beach Tangi Bovu.
 
Hawawezi kuchukua hatua yeyote, maana wananufaika na mfumo unaopigiwa kelele.
 
Dini aliyotaja mtoa mada ni corporate..core product Imani Ila Kuna bidhaa muambata Kama elimu,afya nk,pia rushwa(ruzuku) toka kwa wanasiasa ili wawaswagie waimini wakati wa uchaguzi,utasikia huyu ni chaguo la mungu
Dini na siasa ni kama mjomba na shangazi, hivi vitu viwili vina undugu kihistoria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…