Ni Mkatoliki 100% ila hizi ni sababu zangu za kwanini Sihudhurii na Sitohudhuria Jumuiya za kila Jumamosi....

Umeandika kimajungu. Ujinga mtupu.
 
Dr. Msoka kule Moshi vp?
 
Sababu ulizozitaja baadhi zina UKWELI ila sababu zingine ulizozitaja ni suala linaloegemea mtazamo wako.
(1) Sehemu ya kutongozana, hata kanisani wanatongozana( Mfano: wanakwaya, wanafunzi).
(2) Ishu ya kukuombea kwa MUNGU siyo suala la viongozi wa jumuiya isipokuwa ni mwongozo wa kanisa ( kutoendesha misa kwa asiyehudhuria jumuiya).- Rejea mafundisho yanayosisitiza umuhimu wa MISA.
(3) Hutakiwi kuwa na hasira na watu. Hasa viongozi wa jumuiya ambao ni wapokeaji wa maagizo tu( ndio maana, sasahivi wengi hawapendi kuwa viongozi wa jumuiya).
(4) Hatahivyo, kanisa Katoliki linaendeshwa na michango ya waumini ( tangu mwanzo, ilikuwa hivyo- Rejea kanisa la YERUSALEMU).
NB
-Uko sahihi kabisa kuwa kwenda MBINGUNI kupo katika maamuzi ya MUNGU na siyo vinginevyo.
- Pia kanisa lingekuwa linawapa waumini kama mwezi mmoja hivi baada ya miezi 3 ili wapumue kwa baadhi ya michango, badala ya bandua bandika ili watu wapunguze STRESS.
 
Tatizo jumuiya kila jumamosi zinarotate kwenye nyumba za waumini sasa kama mazingira yako machafu utaichukia tu jumuiya, boresha mazingira yako unapoishi acha kelele
Daah nimecheka sana yani 😂😂😂😂😂😂😂
 
Umenena
 
Nakubali kabisa hii
 
Tatizo jumuiya kila jumamosi zinarotate kwenye nyumba za waumini sasa kama mazingira yako machafu utaichukia tu jumuiya, boresha mazingira yako unapoishi acha kelele
Usijibu hoja kwa ujumla.
Mleta mada ameeleza mambo mengi. Abalaani zinaa ndani ya jumuiya maana anasema mpaka wake za watu wanachukuliwa
Hivi katika hali hiyo atamtaka mwanajumuiya nyumbani kwake?
 
Umeandika kimajungu. Ujinga mtupu.
Michango inatesa sana waamini, kuna mdada tumempa eneo letu atulindie huko shamba basi nikienda namuuliza mbona huendi ibadani anasema hana pesa ya michango, kanisani kwao kuna michango aina 7 ukiacha sadaka,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…