Ni Mkatoliki 100% ila hizi ni sababu zangu za kwanini Sihudhurii na Sitohudhuria Jumuiya za kila Jumamosi....

Ni Mkatoliki 100% ila hizi ni sababu zangu za kwanini Sihudhurii na Sitohudhuria Jumuiya za kila Jumamosi....

Nilichogundua kupitia haya malalamiko yako; Wewe ni kajitu fulani hivi anti social na kasiko penda kuchangamana na watu! Ni kajitu fulani hivi kenye wivu kupindukia! Sijui mke wako amemsifia jirani yako mnaye sali naye Jumuiya kuwa ni hendsam kuliko wewe, roho ikakuuma!!

Unaishi katika mazingira machafu, nyumba ya hali ya chini kuliko wana jumuiya wenzako, hivyo unajishtukia wana jumuiya wenzako wakija kusali kwako, utaonekana wewe ni mtu wa hali ya chini.

Pia unaonekana ni kajitu fulani hivi kafupi na kabishi ka kila kitu! Unaishi maisha ya kuunga unga, hata kama wewe ni genius uliyesoma SAUT! Maana unalalamikia michango ya elfu 5 tu ya kulitegemeza Kanisa la Mungu! Huku ukiombwa elfu 50 na mchepuko, unatuma na ya kutolea!

Mwisho kabisa unaonekana una itikadi za kiukawa ukawa! Halafu unashangilia timu mbovu ya simba, ambayo kila siku ni kuwalalamikia tu wachezaji, kocha Matola, na CEO Barbara! Hivyo akili yako imevurugwa kiasi cha kuhamishia malalamiko yako Jumuiyani.

Ushauri; hujalazimishwa kwenda kusali kwenye Jumuiya. Na hata usipozikwa kwa kuombewa, who cares!!
Duh!

Mpaka Simba imefika kwenye jumuia!!
 
Mkuu huwezi amini Nimecheka mpaka basi kwa hii post yako na kila nikiikumbuka tu najikuta naangua Kicheko tu. Hakika Jamiiforums ni raha mno na Burudani tosha.
Poa mkuu. Mimi ninapenda maisha halisi.

Mwenyekiti alitangaza 'mpango kazi' wa kanisa. Nikawa na hamu kujua pengine ni mpango kazi wa kusali; ja ajabu ananiambia ni michango ambayo ni matumizi ya kila siku ikiwemo kuwalipa wafanyakazi wa Parokia. Nikasema sawa!

Parokia yetu, kila jumuia huwa inaandaa andiko la Mapato na Matumizi.

Kila week michango mara watoto wakienda kuhiji, sherehe, pasaka na sikukuu zote wanataka hela.

Kanisa sijui linatupeleka wapi. Nimewahi kuambiwa Wazungu wamejitoa kufadhili makanisa yetu na kwa hiyo mzigo upo kwetu.

Kanisa lenyewe halisaidii watu. Hata ukienda kuomba panado hupewi. Sasa ya nini?

Hawana aibu!
 
Halafu Wewe Mwenyekiti, Katibu na Mweka Hazina wa Jumuiya yangu hivi mnavyonitishia kuwa kama nisipohudhuria Jumuiya Nikifa hamtoniombea mmeshazungumza na Baba Mungu na akawaambieni kuwa ataanza Kunitanguliza Mimi Kaburini kabla yenu? Wapuuzi wakubwa nyie.
Umemake sense sana hapa POPOMA...tangu nimeanza kukufahamu..
 
1. Jumuiya kumekuwa ni sehemu za Majungu.

2. Jumuiya imekuwa ni sehemu za Kuchunguzana Kimaisha.

3. Jumuiya imekuwa ni sehemu ya Masutano.

4. Jumuiya imekuwa ni sehemu ya Wanaume Kutongoza na Wanawake kutafuta wa Kuwachapa Nao ( Kuwabandua )

5. Jumuiya imekuwa ni sehemu ya Kutishana kuwa kama hauhudhurii basi Ukifa ( Ukifariki ) Kanisa Katoliki halitokuombea ukiwa Jenezani Kwako.

6. Jumuiya imekuwa ni sehemu ya kila Siku kuja na Michango isiyo na Kichwa wala Miguu.

7. Jumuiya imekuwa ni Gulio Kuu la kila aina ya Unafiki unaoujua na usioujua hapa duniani.

Halafu Wewe Mwenyekiti, Katibu na Mweka Hazina wa Jumuiya yangu hivi mnavyonitishia kuwa kama nisipohudhuria Jumuiya Nikifa hamtoniombea mmeshazungumza na Baba Mungu na akawaambieni kuwa ataanza Kunitanguliza Mimi Kaburini kabla yenu? Wapuuzi wakubwa nyie.

Je, mnavyong'ang'ania Kutoniombea GENTAMYCINE pale Nikifa je, ile Siku ninazaliwa mlikuja Agha Khan Hospital mbele ya Sister Brendah na Sister Aghata waliohakikisha Nazaliwa vyema na salama Kuniombea? Wapuuzi wakubwa nyie.

Na nani aliyewadanganyeni kuwa Imani ya Ukatoliki inapimwa kwa Kuja Kwake ( Kuhudhuria ) katika Jumuiya za Kikatoliki kila Jumamosi kama ya hii leo?

Nilichoamua tu na najua hata Mwenyezi Mungu ananibariki nacho ni kwamba nitajitahidi Kuhudhuria Ibada zote za kila Jumapili ( hasa Misa yangu pendwa ya Kwanza ) na kutoa Sadaka na Michango ya Kikanisa kama tu nitakuwa Nimebarikiwa na Uchumi kwa wakati huo na kama sina najua hata Mola / Maulana nae atajua na hatonichukia au kuwa na Usununu ( Kinyongo ) nami.

Nawatakieni nyote Jumuiya njema!!!!

Ni wakati kwa wakatoliki kujitafakari kama ni mahali sahihi kulea watoto wao na Familia zao
 
Mkuu fanya tafiti .. baada ya Central gvt kanisa katoliki linafuata kutoa kwa jamii.
Hivi unanielewa. Nina maana kwamba; mimi ninatoa michango bure kwa kanisa, lakini kanisa halinipi bure msaada.

Siyo huduma hizo za kanisa ambazo hata kuzimudu nazo ni tabu tupu. Shule ghali, dawa ghali, hospitali na kila huduma ya kanisa ni gharama sana kuliko za serikali. Sasa si bora nikaacha kuchangia ili niwe na akiba ya kumudu hizo huduma zao.
 
Tatizo linakuja pale ambapo Mtu haendi Jumuiya, haendi Kanisani, hatoi michango yoyote ila akipatwa na shida anataka Kanisa limsaidie, nenda Jumuiya kwa ajili ya kusali kama kuna mambo mengine yanakukwaza achana nayo hayo ni mambo ya wanadamu na hakuna aliyemkamilifu.
Kanisa huwa linasaidia nini?
 
Hao wote mnasema ni wakatoliki nyie sio maana tayari mmesha hasi kanisa.

Moja mmekataa kwa hiari yenu kushiriki jumuiya na sala zingine za vikundi(vyama vya kitume) lakini pia kanisani hamuendi, ila mnataka mzikwe na huduma ya kanisa.

Kanisa ni la walio hai na sio wafu hivyo shiriki ukiwa hai ili ukifa waamini wakusindikize kwa maombi.

Pia jumuiya yako hayo majungu sijui kutongozana sioni maana yeyote zaidi ya uongo maana sala ni dakika 45. Baada ya sala watu wote wanaondoka tena saa 12:00 asubuhi wanatongozana wapi.

Kama wanaweza kwemda wote kanisani, vikoba vya mtaa, wanakutana kila siku mtaani Jumuiya haiwezi kuwa chanzo maana wanakutana mara nyingi zaidi kwenye mambo mengine kuliko huko kwemye jumuiya.

Kuhusu michango, ni kweli ipo kwenye jumuiya kama sehemu ya kuendeleza kanisa. Lakini jumuiya zenye sadaka nzuri hakuna haja ya michango.

Mwisho huna hoja ya kutokwenda jumuiya zaidi ya uvivu, ulegevu wa iman, ulembukeni wa imani na kutaka kujusfy upungufu wako.
Miradi yote ya kanisa katoliki pesa zinakwenda wapi?
 
Katika kanisa Katoliki jumuiya ni kama serikali za mitaa katika serikali, na Vatican ni nchi, hivyo huwezi kukwepa jumuiya. Jitahidi urekebishe mambo na ubaki kwenye jumuiya yako. Kila kitu kinaanzia kwenye jumuiya mf. Ubatizo, ndoa nk.
 
Kwa wenyeji tuliozaliwa Dar maternity ilikuwa ocean road then ikahamia Muhimbili.

Ukifoji birth certificate ukaandika umezaliwa Aga Khan unapigwa pingu mapema tu.
Mqjuha wakubwa nyie jadilini Mada Kuu na sijasema kuwa Nimezaliwa Hospitali ya Agha Khan labda niwe kama najimwambafai Kwenu bali ni katika Kukazia Uzi.

Na kuwatieni Hasira zaidi Majuha na Washamba nyie sikuishia tu Kuzaliwa hapo ila nilipozaliwa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere akatoka Ikulu ( Mita chache tu ) kuja Kunibeba na kunipa Jina langu halisia ambalo ninalo na nitakufa nalo.

Na sijacheza tu na kushinda Ikulu yenu ya Magogoni na kule ( pale ) Msasani bali pia nimechezea na hadi kulala vile vile na Ikulu ya Nakasero nchini Uganda kwake Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Wapuuzi wakubwa nyie mliojaa Wivu, Chuki, Hasira na Ushamba kwakuwa labda hamkuwa / hamjawa 'Privileged' tokea mzaliwe au katika Makuzi yenu kama wengine ambao tumezaliwa na kuyakuta hayo ( haya ) Maisha japo huwa hatupendi Kujionyesha au Kujitangaza ila inapobidi na tukikutana na Waswahili kama Wewe na Wenzako huwa mnatulazimisha sasa 'tujimwambafai' Kwenu ili tuanze Kuheshimiana.
 
Back
Top Bottom