Ni mkoa gani ambao hata ukipata ajira huwezi kwenda?

Jina lako linasanifu ulichoandika
 
Kuna rafiki yangu alitoka Dar akahamia Mafinga anasema anapenda baridi na hakuna mmbu.

Mwingine alikuwa analalamika kuhama Lindi sababu alikuwa anapenda yale maisha ya utulivu na samaki kule ferry.

Ila miye Lushoto ilinishonda aisee.Ile baridi na ile barabara kitonga mwa mwiii hatari sana.
 
Jamaa primitive kwelikweli, siku akipata KAZI ofisi ina kiyoyozi ataacha pia. Huyo kazoea kuwa winga.
 
Kila mkoa Tanzania hivi sasa ni fursa na hasa ukiyatumia matatizo ya mkoa husika
 
Mie popote nafanya kazi.
Huyo kijana ana namna nzuri ya kuishi nje ya ajira yake ya huko Njombe.
Eti baridi..., wengine wanaishi vipi huko Njombe, Mafinga, Lushoto, na baadhi ya nchi za Ulaya zenye baridi kali zaidi ya Njombe?
 
Asingeomba kazi tuache kuongopeana hapa.Mtu aliye stable kiuchumi huwa hakubali kuajiriwa narudi huwa hatukubali kuajiriwa kwa namna yeyote ile.ACHENI UONGO UONGO
 
Mtu ambaye haijui laki tatu inafananaje anaweza kuacha mashahara wa 1m kisa baridi?

Mimi nimetoa maoni yangu, nawe toa ya kwako.
Ulianza kusema ana option nyingi..nikasema mtu aliyestable kiuchumi na awe na biashara inalipa hawezi omba wala apply hizi kazi za TGS atakuwa hana akili sawa sawa.
Kitu pekee nimejifunza watu wenye uchumi hupeleka watoto wao maeno kimkakati sio ku apply.

Ila kama aliomba huyo yeye mwenyewe na akaacha basi toka awali hajui anachofanya..Wafanya biashara hawana muda wa kupoteza kirahisi
 
Watanzania (weusi) asilimia 80 tunasoma kuajiriwa...

Haijalishi nyumbani pesa ipo au haipo...

Hiki ndiyo kinafanya niamini jamaa alikuwa na option nyingine, na aliomba ajira kama desturi ya watanzania wengi...

So alipoona changamoto ikawa rahisi kurudi kwenye option zake za mwanzo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…