Ni mkoa gani nchini wenye maeneo mazuri kwa vacation?

Huko South sijapenda hata...
Ule ushauri wa yule mkuu kwamba nikimaliza mwanza nipitemo hadi Nai nimeupenda
 
Asante mkuu
Kwakuwa nimeamua kujipa amani nimeamua kuanza na hotel ya 50k kuendelea
Mkuu chaguo ni lako kwa mwanza hotel za 30 hadi 80k nyingi hazina utofauti, kama pesa siyo tatizo malaika beach resort itakufaa, au fika mtaa wa Ghana jichagulie itakayokufaa zaidi.
 
Chato.

Ukatalii jengo la TRA la mkoa.

Benki ya CRDB

Chato international Airport.

Hospitali ya Rufaa ya Chato.

Na mengine mengi.

Hakika hutojutia.

Kila la heri.
 
Njoo mkoa wa Mara wilaya ya Tarime
 
Nenda mwanza gharama ni nafuu pia kwa malazi au mtwara mjini Kuna mishemishe nyingi Sana usiku na sehemu za starehe za kutosha pia unaweza kuwa kutembelea maeneo ya kihisistoria km vile mikindani na maeneo mengine
 
Weka mafuta kwa gari, nenda Selous tafuta lodge iliyo pembezoni mwa mto Rufuji, kama unataka kwenda sehemu ya kutuliza akili yenye mazingira asilia, kwa bajeti yako unaweza kaa night kama 5 hv, utapata msosi wa asbh, mchana na jioni. Sehemu nyingine Arusha ingawa siyo mjini, Arusha kuna sehemu nyingi za kutuliza akili na kutafakari. Ila kama unataka vibe, basi Mwanza ndy sehemu.
 
Mkuu chaguo ni lako kwa mwanza hotel za 30 hadi 80k nyingi hazina utofauti, kama pesa siyo tatizo malaika beach resort itakufaa, au fika mtaa wa Ghana jichagulie itakayokufaa zaidi.
Sawa mkuu
Ushauri wako unazingatiwa sana sana
 
Chato.

Ukatalii jengo la TRA la mkoa.

Benki ya CRDB

Chato international Airport.

Hospitali ya Rufaa ya Chato.

Na mengine mengi.

Hakika hutojutia.

Kila la heri.
Hahahahaha
 
Option nyingine; Ukitaka uinjowi vizuri toka Dar hadi Dodoma pumzika kidogo hapo Dom Jioni nenda zako Pale Bambalaga au Pestana pata wine zako, Kisha ondoka asubuhi kwenda Arusha jioni upumzike pale Picnic-kisha anza safari kesho yake kwenda Mwanza kupitia njia ya Serengeti-kula rough road hiyo kapumzike Butiama kwa Baba wa Taifa ucheki makumbusho. Kesho yake anza safari kupitia Bunda nenda pale Serengeti kacheki zako wanyama kesho yake anza ssafari tena mpaka Mwanza- usiku kapate moja moto moja baridi pale the Cask kesho yake amkia Malaika resort.

Anza safari ya kutoka Mwanza-Dom,ukifika Dom chukua barabara ya Dom-Iringa-Mikumi-Dar.
 
Nenda mwanza gharama ni nafuu pia kwa malazi au mtwara mjini Kuna mishemishe nyingi Sana usiku na sehemu za starehe za kutosha pia unaweza kuwa kutembelea maeneo ya kihisistoria km vile mikindani na maeneo mengine
Asante mkuu
Mtwara ni nyumbani pia nadhan hii nitafanya likizo ya December
 
Asante mkuu
Naona Mwanza ndio habari ya mjini.
 
Hii imekaa poa sana
 
Njoo nikupe lift kesho naenda mwanza na cruiser warbus tutakua wawili tu Mimi na wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…