Darasa la saba ulipata wastani wa "A" na ukakosa fursa ya kwenda kidato cha kwanza? Kidata cha nne ulipata Division ONE na hukuchaguliwa kwenda Alevel au vyuo (kama ulichagua vyuo)? Alevel ulipata Division ONE ukakosa fursa ya kwenda Chuo Kikuu? Chuo Kikuu ukapata GPA ya "First Class" au "Upper Second" alafu ukakosa ajira?
Wengi wanaolialia wamesoma wakakosa ajira ni wale vilaza na wanaolazimisha ufauru afifu kuwa wamefauru! Katika Dunia hii ya utandawazi ili utoboe unahitaji viwango vya juu vya kudhihirisha kuwa uko vizuri! Sio unajikusanya na Division two au GPA ya lower au Gentleman alafu unalialia sina ajira! Hizo enzi zimepita mkuu! Ukiona umetupwa nje na mfumo wa ajira jiongeze kivingine!
Nashangaaga kuona mtaani vijana eti wanahusstle kwa kuendesha bodaboda, kupika mandazi, vitumbua, samaki, miogo alafu wanategenea kutoboa kuwa na maisha safi ya kumiliki nyumba nzuri, gari zuri, majina na heshima nzuri ya ukwasi! Thubutu!!! Utapata ela ya kula lakini umasikini umeishatia timu!!
Povu ruksa!!
Ajira ni ngumu pia, fulsa ni chache,hata ufaulu vzr kiasi gani, kwa, hapa kwetu mwajiri mkubwa ni serikali,lqkini, yenyewe Ina limit, haiwezi kuajiri kila mwalimu, dokta anayetoka chuo,
Shule zipo, nyingi, na, zinahitaji, waalimu, sasa ukiajiri wote utawalipa kwa pesa, ipi? Wakati mapato hayatoshi? Serikali iliweka tozo,wananchi, wakaja, juu, sasa ikabidi waitoe,
Usijidanganye bro, fulsa bongo ni chache,
Miaka 14,iliyopita, nilikuwa, naweza kuacha kazi kqmpuni moja(telecom industry), nikagonga geti kqmpuni nyingine nikapata ajira, nimefanya kazi, kqmpuni kama Saba! Hawa, wakizingua naenda kwingine, faster! Sasa, hv, hata hizo, kqmpuni nilizopita kumtafutia, mtu field, au, kujitolea tu, hiyo nafasi, hakuna!