Red black
JF-Expert Member
- Nov 29, 2019
- 5,962
- 17,648
Ukiwa huna, kila mtu hakutaki unakuwa takataka mbwa. Ukipata usigeuke nyuma unapaswa kuwa katili kweli kweli kwa sababu dunia haina huruma wala msalia mtume.Binadamu ni wabinafsi sana tena sana.
Zamani nilikuwa nina moyo wa kuwapigania na kuwapambania watu au kuwatetea lakini baadaye nikagundua watu wote wana roho ya korosho na kila mtu anajipigania nafsi yake. Hata wale unaowatetea nao wana choyo kali.
Kwa jinsi hii, sharti watu wote wasimame kwa miguu yao wenyewe. Hata viwete wajiburuze mpaka kieleweke.
Ukipata mkate ufiche, kula mwenyewe usimpe mwingine. Hata anayeomba kwa kulia mkanyage mateke.
Ukiwa huna, kila mtu hakutaki unakuwa takataka mbwa. Ukipata usigeuke nyuma unapaswa kuwa katili kweli kweli kwa sababu dunia haina huruma wala msalia mtume.
Cc: min -me Mine -me Poor Brain
Kila mtu ajipambanie kivyake bhana