Ni msomi yupi mwenye sifa hizi na bado yuko mtaani hana ajira?

Pole ndiyo maisha
wacha tu, kuna mwamba alikuwaga slow lena mbaya, yaani nilikuwa natumia muda mwingi sana kumfundisha, alitoka na lower second, alipata kaz kabla yangu akawa anaongea shit sana juu yangu kuwa nilikuwa najiona kipanga ila nipo mtaani, huku na huku akawa kaharibu jobun kwake wakamfukuza akawa yupo mtaani ila ananikwepa sana, siku moja nikampigia nikamwambia tuonane, tukapiga kit moto na mbili tatu, nikamwambia aje jobuni kwangu, jobuni kwangu kuna hr aliacha kaz baada ya kupata sehemu nyingine, jamaa alipokuja nikamuuliza una cv? akajbu ipo kwenye flash, nikapokea flash nikaprint ile cv nikamwambia twende, tukaenda kwa yule hr, kufika tulisalimiana tu nikamwekea cv mezan nikamwambia mkuu naomba umpe huyu jamaa yangu kaz, yule hr aliniangalia akatingisha kichwa, akajbu sawa mkuu, haikuisha hata wk jamaa akaitwa kazn bila hata interview, jamaa yuko njema sana kwa sasa, ila tukikutana kwenye mazungumzo lazima atasema gpa kali sio maisha,
 
B 👍
 
Kuna dada mmoja alisona SUA mambo ya rural planning ana upper second class na form six ana division 1 na 4m4 alitona na 2 Kama boss 3. ajira muda mwingine ni bahati tu
 
nadhani mtoa mada ni mhaya maana hilo neno ufaulu kaliita ufauru, pili kupata A sio kigezo cha kupata kazi hayo ma A na ma first class yamejaa mtaani na hayana kazi , na ukitaka kuamini muulize mkuu wa ailaya ya Ubungo anayehangaika na maafisa utamu kule riverside wengi ni graduate wenye CV kali lakini ndio wameangukia kwenye mkumbo huo. Kazi sio A kwenye nchi zenye upuuzi na ujinga ujinga kama hiyo ya kwetu.
 
Fursa zinabana.
 
Kama familia ina uwezo peleka kijana Veta ama vyuo vingine vya ufundi achague fani yeyote ya ufundi akimaliza atafungua milango ya kujiajiri.
 
We mafisa utamu wengi ni magraduate?
 
Eeeh jamani kwanini usitafute siku umuombe mkutane utoe kinyongo chako?
Bado mnafanya kazi wote?
hatujawai kufanya kaz sehemu 1, ile kampuni niliyomuunganishia kaz ilikuja ikauzwa, directors walimake hela nyingi sana, mmoja akafungua kampun nyingine akamfanya country manager, anamlipa vzuri sana, aisee huyu jamaa, kuna siku bwana kanipgia, oya wapi hyo? mm home, vp lkizo au? mm yap, aksema afadhali bwana kuna kimeo cha siku 10 hapa nilitakiwa nisafiri kama vp ukakifanye basi, nikamuuliza utanitoaje, akajbu 250usd/dy, nikamwambia poa, yy nakutumia detalls basi uandae work program na budget, nikaandaa nikamtumia, akawa kimya tu, siku nakutana naye ananiambia aisee ile kaz uliandaa poa sana, ila nilimpa dogo mmoja akaenda kuifanya, kuanzia siku hyo sijawai pokea simu yake
 
Duh! Nimejisikia vibaya amekutendea vibaya ila msamehe
 
JF hata hamueleweki msimamo went

Leo munasifia msomi aliyejiajiri kuuza mihogo pale Coco kama Aslay mihogo na kusema anapiga pesa kuliko watumwa, kesho munakuja na uzi umesoma unauza mihogo ujaajiriwa kwaajiri uliferi.

Kesho kutwa munaandika uzi kusema Msomi mwenye akili kasoma anauza uji HUBPAP kisasa mwenge kesho kutwa munakuja kuandika umesoma unauza uji.

Anyway nikuulize swali
MFANO: Mimi nimeajiriwa nikasimamishwa kazi hapa inamaana sija ajira so hii inamaanisha kuwa mtoa mada unaweza nishangaa mimi nimesoma na sijaajiriwa.

Yaani mfano wewe mtoa mada umesoma una ajira nzuri kesho ukafukuzwa kazi, nitakuwa sahihi kushangaa Haa inakuwaje msomi na hana ajira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…