boda
JF-Expert Member
- Apr 4, 2014
- 341
- 290
Hakika boda
Amina.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakika boda
Mithali 3:1 Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu.
Mithali 3:2 Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani.
Mithali 3:3 Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
Mithali 3:4 Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu
Mithali 3:5 Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe..
Mithali 3:6 Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.
UJumbe wowote wa maneno huwa unabadilika maana pale ambapo maneno halisi yakabadilishwa kwa namna moja au nyengine na kutiwa mengine .Muhimu sana kama wewe ni Mkristo ujue kwamba lengo la Biblia kuwepo kwa toleo la lugha tofauti tofauti ni ili kila atakaeisoma aielewe kiurahisi kwa lugha anayoielewa na kutafakari kitu akiwa amekielewa Biblia siyo kitabu cha siri au cha uganga kwamba isomwe huku msomaji akifungua codes
Na tujue huwa hakipungui kitu neno na maana inabaki vile vile muhimu ni mimi ninaesoma naelewa?mfano huo mstari uliopandishwa hapo kuna eneo ukisomwa wasikilizaji wanabaki njia panda same to unaoujua wewe ukisomwa watu hawauelewi.
Ufunuo 12:11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.Bwana wetu Yesu kristo asifiwe wana Jf
Katika maisha yetu hapa duniani kuna wakati tunapitia nyakati zilizo na mambo magumu sana, kiasi kwamba kwa uwezo wetu unakosa majibu na kubaki kujiuliza maswali magumu yasiyo na majibu.
Nyakati kama za Kufukuzwa kazi, Ugumu wa maisha, kupoteza wapendwa wetu tuliowapenda sana. Usaliti katika maisha ya mahusiano na ndoa, kukosa kazi, kupakaziwa maneno yasiyo na ukweli pengine ugonjwa wa muda mrefu.
Tunapitia dhiki, mateso na maumivu katika maisha. Ukipata hiki unakosa kile ndivyo maisha yalivyo.
Natumaini letu linabakia kwa Muumba wetu.
Je ni mstari gani kutoka kwenye biblia unautumia sana kukupa faraja mpendwa.
Kwa upande wangu, Mstari unaoniongoza kila siku ni
Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.
Zaburi 23:6
Karibu.
Tusichoke kutenda wema.