Ni muda Cheo cha Makamu wa Rais kifutwe Tanzania

econonist

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
20,189
Reaction score
29,663
Kwa Sasa Katiba ya Jamhuri ya Tanzania inatakiwa kupitiwa upya, na kuondoa cheo Cha Makamu wa Rais. Cheo hili hakina tija kinaongeza tu mlundikano wa vyeo visivyokuwa na maana.

Makamu wa Rais Hana mamlaka Kama aliyonayo Waziri Mkuu, ndio maana Waziri Mkuu anaweza kumfukuza au kumsimamisha kazi Mtumishi ila sio Makamu wa Rais.

Nafasi ya Makamu wa Rais imekuwa ceremonial tu. Makamu wa Rais anaweza kupotea hata miezi SITA na wananchi wasishangae au Makamu wa Rais ataonekana Sana kwenye ufunguzi wa warsha na makongamano.

Ni kweli Makamu wa Rais yupo kwaajili ya kukaimu nafasi ya urais Rais anapokuwa nje ya nchi, ila sio lazima yeye akaimu , Rais anaweza kumkaimisha yeyote madaraka ya Urais akiwa nje.

Nashauri baadala ya kutumia pesa nyingi kumuhudumia Makamu wa Rais na watu wake, ni bora kuondoa hicho cheo na Mazingira pamoja na Muungano vikaunganishwa kwenye Wizara ya mambo ya ndani .
 
Hujielewi kamanda! Hivi unajua nafasi ya urais wewe? Hiyo nafasi haitakiwi kukaliwa na yeyote ambaye wananchi hawamjui! Juzi Phillip Mpango walitoka kuzushiwa kifo sababu wananchi hawajamuona muda mrefu! Rais anapokuwa hayupo lazima hicho kiti pawepo wa kukikalia vinginevyo akikaa mtu ndiye siye anaweza kumzuia hata Rais asirudi nchini au kufanya chochote kwasababu kimamlaka kakalia kiti!
 
1. Mmiliki wa Jengo yupo wapi?
NANI NI MMILIKI WAJENGO.
2. Ramani za jengo ziko wapi??
Uokozi bila Ramani.

3. Ghorofa nne watu wanaokolewa siku nne na sio moja. TAIFA LIMEOZA.

4. Selikali ipo Radhi kununua Mabomu, magali ya Jeshi nk kuizuia CHADEMA na Inashindwa KUNUNUA VIFAA VYA UOKOAJI kwa Raia wake.

5. Niffer amejipeleka Kituoni, Yuko wapi mmliki wa Jengo.

6. Je ni nani aliyetoa vibali vya kujenga na kubomoa anakamatwa Niffer.
TANZANIA YANGU MASIKINI

ZIMA MOTO NA UOKOAJI NI SAWA NA HAKUNA KITU ZERO KABISA.
JESHI LIVUNJWE HARAKA

MAJENGO MENGI KARIAKOO YAMEOZA
 
Hujielewi kamanda! Hivi unajua nafasi ya urais wewe? Hiyo nafasi haitakiwi kukaliwa na yeyote ambaye wananchi hawamjui! Juzi Phillip Mpango ilitoka kuzushiwa kifo sababu wananchi hawajamuona muda mrefu! Rais anapokuwa hayupo lazima hicho kiti pawepo wa kukikalia vinginevyo akikaa mtu ndiye siye anaweza kumzuia hata Rais asirudi nchini au kufanya chochote kwasababu kimamlaka kakalia kiti!

Huko shuleni ulienda kusomea ujinga? Mbona sababu umetoa haina mashiko. Kwa hivyo Makamu wa Rais yupo kwaajili tu ya kuwa Rais au kumkaimu Rais?. Yani tuwe na mtu mwenye cheo Cha kumkaimu Rais akiwa hayupo.

Kama Hilo ndilo shida yako, tunaweza kuamua Rais asipokuwepo nafasi itakaimiwa na Spika wa Bunge, au Jaji Mkuu. Na iwapo Rais atafariki, nafasi yake ikaliwe na Jaji Mkuu kwa muda wa siku 60 kabla ya uchaguzi wa Rais. Hii dhana ya sijui mtu yeyote hawezi kuwa Makamu wa Rais asije kumzuia Rais asirudi akiwa nje ni ya kitoto. Rais anaweza kuzuiwa na CDF na Jeshi lake sio Makamu wa Rais.

Narudia Tena tufute cheo Cha makamu wa Rais Tanzania.
 
Umeuliza maswali ya msingi.
 
Atajielewa wapi pimbi tu huyo kula kulala, hivi ndio vikamanda uchwara.
 
Huko shuleni ulienda kusomea ujinga? Mbona sababu umetoa haina mashiko. Kwa hivyo Makamu wa Rais yupo kwaajili tu ya kuwa Rais au kumkaimu Rais?. Yani tuwe na mtu mwenye cheo Cha kumkaimu Rais akiwa hayupo.

Kama Hilo ndilo shida yako, tunaweza kuamua Rais asipokuwepo nafasi itakaimiwa na Spika wa Bunge, au Jaji Mkuu. Na iwapo Rais atafariki, nafasi yake ikaliwe na Jaji Mkuu kwa muda wa siku 60 kabla ya uchaguzi wa Rais. Hii dhana ya sijui mtu yeyote hawezi kuwa Makamu wa Rais asije kumzuia Rais asirudi akiwa nje ni ya kitoto. Rais anaweza kuzuiwa na CDF na Jeshi lake sio Makamu wa Rais.

Narudia Tena tufute cheo Cha makamu wa Rais Tanzania.
Logics zinakataa Boss, lakini pia angalia best practice duniani, nchi nyingi zenye Rais Mtendaji huwa Zina Makamu wa Rais ambaye ni Running mate, maana yake amepewa nguvu na watu.

Lakini pia ili kumfanya Makamu awe na kazi ya kufanya day in day out kuna baadhi ya nchi Makamu wa Rais Anapewa Wizara fulani fulani, Mfano hapa kwetu ni Mazingira na Muungano; maana yake sio kweli kwamba Hana kazi za kufanya.

Changamoto kwenye andiko lako nadhani unataka kumuona Makamu Yuko on per na Boss wake, hili nafikiri haliwezekani, refer case ya juzi ya Gachagua/Ruto.
 
Huyo hana akili kichwani.
 
Uko sahihi kabisa.nafasi ya makamu haina tija zaidi ya kuongeza gharama zisizo na tija.Na katiba ibadilike ili ikitokea rais amefariki basi waziri mkuu akaimu Kwa muda wa miezi sita au mwaka mmoja na kuitisha uchaguzi upya ili kuondoa muserereko wa mtu kupata nafasi ya urais chumbani kwake.
 
Kwa Sasa Katiba ya Jamhuri ya Tanzania inatakiwa kupitiwa upya, na kuondoa cheo Cha Makamu wa Rais. Cheo hili hakina tija kinaongeza tu mlundikano wa vyeo visivyokuwa na maana. Makamu wa Rais Hana mamlaka Kama aliyonayo Waziri Mkuu , ndio maana Waziri Mkuu anaweza kumfukuza au kumsimamisha kazi Mtumishi ila sio Makamu wa Rais.

Nafasi ya Makamu wa Rais imekuwa ceremonial tu. Makamu wa Rais anaweza kupotea hata miezi SITA na wananchi wasishangae au Makamu wa Rais ataonekana Sana kwenye ufunguzi wa warsha na makongamano. Ni kweli Makamu wa Rais yupo kwaajili ya kukaimu nafasi ya urais Rais anapokuwa nje ya nchi, ila sio lazima yeye akaimu , Rais anaweza kumkaimisha yeyote madaraka ya Urais akiwa nje.

Nashauri baadala ya kutumia pesa nyingi kumuhudumia Makamu wa Rais na watu wake, ni bora kuondoa hicho cheo na Mazingira pamoja na Muungano vikaunganishwa kwenye Wizara ya mambo ya ndani .
Hata Waziri Mkuu hana lolote kionodolewe hicho cheo haraka
 
Uko sahihi kabisa.nafasi ya makamu haina tija zaidi ya kuongeza gharama zisizo na tija.Na katiba ibadilike ili ikitokea rais amefariki basi waziri mkuu akaimu Kwa muda wa miezi sita au mwaka mmoja na kuitisha uchaguzi upya ili kuondoa muserereko wa mtu kupata nafasi ya urais chumbani kwake.
Nafasi ya Makamu, Viti maalum, RC/DC/DAS vifutwe havina maana yoyote zaidi ya mzigo kwa walipa kodi
 
Kwa sasa usimlaumu sana makamo wa raisi sababu kwa awamu hii ndani ya serikali kuna serikali nyingine tusiyoijua na yenye nguvu kuliko serikali tunayoijua.

Mfano Abdul wa mama Abdul ana madaraka na kauli kuliko hata Waziri Mkuu.

Hii nchi imekuwa mateka ya wapumbavu. Tunatawalia na wapumbavu na kwa vile kabla ya hapo sisi wenyewe ni wapumbavu wakubwa zaidi basi imekuwa ni balanced equation ya upumbavu.

Jamhuri Ya Muungano Wa Wapumbavu.
 
Kwa Sasa Katiba ya Jamhuri ya Tanzania inatakiwa kupitiwa upya, na kuondoa cheo Cha Makamu wa Rais. Cheo hili hakina tija kinaongeza tu mlundikano wa vyeo visivyokuwa na maana. Makamu wa Rais Hana mamlaka Kama aliyonayo Waziri Mkuu , ndio maana Waziri Mkuu anaweza kumfukuza au kumsimamisha kazi Mtumishi ila sio Makamu wa Rais.

Nafasi ya Makamu wa Rais imekuwa ceremonial tu. Makamu wa Rais anaweza kupotea hata miezi SITA na wananchi wasishangae au Makamu wa Rais ataonekana Sana kwenye ufunguzi wa warsha na makongamano. Ni kweli Makamu wa Rais yupo kwaajili ya kukaimu nafasi ya urais Rais anapokuwa nje ya nchi, ila sio lazima yeye akaimu , Rais anaweza kumkaimisha yeyote madaraka ya Urais akiwa nje.

Nashauri baadala ya kutumia pesa nyingi kumuhudumia Makamu wa Rais na watu wake, ni bora kuondoa hicho cheo na Mazingira pamoja na Muungano vikaunganishwa kwenye Wizara ya mambo ya ndani .
Cheo Cha makumu wa raisi kimewekwa ili kuwaridhisha wazanzibari wajione nao ni watawala kwenye muungano.
Ikiwa raisi ni mtanganyika

Sasa kibao kimegeuka raisi ni mzanzibar Makamu wa raisi ni redundunt

Tumeishashauri sana juu ya mabadiliko ya katiba mpya hawatusikilizi
 
Uko sahihi kabisa.nafasi ya makamu haina tija zaidi ya kuongeza gharama zisizo na tija.Na katiba ibadilike ili ikitokea rais amefariki basi waziri mkuu akaimu Kwa muda wa miezi sita au mwaka mmoja na kuitisha uchaguzi upya ili kuondoa muserereko wa mtu kupata nafasi ya urais chumbani kwake.
Uingereza waziri mkuu ndiye raisi, najiuliza Marekani kwanini hawakutaka cheo cha Waziri mkuu na ndilo taifa tunaloangalizia mambo mengi. 🙂
 
Naungana na mleta mada cheo cha makamu wa rais kama kilivyo sasa hakina maana yoyote,ule utaratibu wa zamani wa Rais wa Zanzibar na Waziri mkuu kuwa makamu wa rais ungefaa zaidi kuliko huyu wa sasa asiye na kazi zaidi ya kutembea na mkasi wa kwenda kukata utepe kwenye uzinduzi.
 
Naunga mkono hoja na kwenda mbele kwa kudokoa kwenye rasimu ya katiba mpya ya.warioba kwamba mkoa unatosha kuongozwa na mkurugenzi maana ndieanakuwana.sifa na utaalamj labda wa public.finamce. accounting etc

Dunia inapoelekea vyeo vya uchawa havina.nafasi tena eti huyu aligombania akakosa basi apewe ukuu wa wilaya. Lazima serikali i cut.down operating.cost
 
Huko shuleni ulienda kusomea ujinga? Mbona sababu umetoa haina mashiko. Kwa hivyo Makamu wa Rais yupo kwaajili tu ya kuwa Rais au kumkaimu Rais?. Yani tuwe na mtu mwenye cheo Cha kumkaimu Rais akiwa hayupo.

Kama Hilo ndilo shida yako, tunaweza kuamua Rais asipokuwepo nafasi itakaimiwa na Spika wa Bunge, au Jaji Mkuu. Na iwapo Rais atafariki, nafasi yake ikaliwe na Jaji Mkuu kwa muda wa siku 60 kabla ya uchaguzi wa Rais. Hii dhana ya sijui mtu yeyote hawezi kuwa Makamu wa Rais asije kumzuia Rais asirudi akiwa nje ni ya kitoto. Rais anaweza kuzuiwa na CDF na Jeshi lake sio Makamu wa Rais.

Narudia Tena tufute cheo Cha makamu wa Rais Tanzania.
Kiprotocally ya kimamlaka CDF ni mdogo sana! Huyu yuko kutii mamlaka ya juu! Kwenye muhimili wa serikali: hiko hivi: Rais, makamu wa Rais, Waziri mkuu, makamu wa pili wa rais (Rais wa Zanzibar), Katibu mkuu kiongozi. Kijeshi: Rais, Makamu wa rais, Waziri mkuu, waziri wa ulinzi, CDF. Hao wengine sijui spika, Jaji Mkuu wako kushoto sana katika mtiliko wa hamri!
 
Kwa Sasa Katiba ya Jamhuri ya Tanzania inatakiwa kupitiwa upya, na kuondoa cheo Cha Makamu wa Rais. Cheo hili hakina tija kinaongeza tu mlundikano wa vyeo visivyokuwa na maana. Makamu wa Rais Hana mamlaka Kama aliyonayo Waziri Mkuu , ndio maana Waziri Mkuu anaweza kumfukuza au kumsimamisha kazi Mtumishi ila sio Makamu wa Rais.

Nafasi ya Makamu wa Rais imekuwa ceremonial tu. Makamu wa Rais anaweza kupotea hata miezi SITA na wananchi wasishangae au Makamu wa Rais ataonekana Sana kwenye ufunguzi wa warsha na makongamano. Ni kweli Makamu wa Rais yupo kwaajili ya kukaimu nafasi ya urais Rais anapokuwa nje ya nchi, ila sio lazima yeye akaimu , Rais anaweza kumkaimisha yeyote madaraka ya Urais akiwa nje.

Nashauri baadala ya kutumia pesa nyingi kumuhudumia Makamu wa Rais na watu wake, ni bora kuondoa hicho cheo na Mazingira pamoja na Muungano vikaunganishwa kwenye Wizara ya mambo ya ndani .
Umesema ukweli kabisa mwamba!
 
Back
Top Bottom