Kwa maoni yangu,
nadhani kile cheo cha makamu mwenyekiti wa chadema taifa ndicho hasa hakina maana wala umuhimu, na kilichopoteza uelekeo kabisa, na kwakweli kinachochochea uhasama na kuzidisha mpasuko na mgawanyiko chadema, ndicho haswaaa cha kufutilia mbali...
kuhusu kwingineko,
nadhani kuna tatizo la uelewa na ufahamu tu, juu ya umuhimu na maana ya makamu au naibu rais. Ukijua malego na madhumuni yake licha ya gharama yake, kamwe huwezi kufikiri wala kusema ulichokiandika. Akina Aristotle na Plato hawakua na ufinyu wa fikra kama huo wa kwenye hoja ya msingi, ndiyo maana wakabuni na kuweka nafasi hiyo.
Na kwa binadamu alivyo,
mpaka kwanza apate tatizo ndipo aone umuhimu wa jambo alilokua akilidharau au haelewi wala kuona umuhimu wake.
Nachelea kusema,
kama kuna nafasi muhimu, nzito na ya maana sana ambayo kamwe haistahili hata mjadala wa kuwepo kwake basi ni nafasi ya Makamu au naibu wa rais.🐒
Mungu Ibariki Tanzania