Ni muda gani inapaswa mwanaume akupeleke kwake baada ya kuanza naye mahusiano?

Ni muda gani inapaswa mwanaume akupeleke kwake baada ya kuanza naye mahusiano?

Kumpeleka mtu kwako si jambo dogo lazima ujiridhishe sana ukiona umewahi kupelekwa basi hapo ni "gheto" huenda ukitoka wewe anaingia mwingine
Kumbe… sasa kwako si nimemaanisha mahali anapoishi mwanaume au wewe umenielewaje hapo
 
Unakuta mtu ana miaka 45 lakini anakupeleka kwenye gheto la kijana wa miaka 22 lina Sabufa ya kumulika mulika anajifanya lake.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 mtu asiwe na sabufa la kumulikamulika jmn
 
Miaka 89.
Kama mnavojua tunakutana tukiwa watu wazima tuliokulia mazingira tofauti..
kabila tofauti mikoa tofauti, hivyo hatujuani wala kufahamiana tunaanzisha tu mahusiano


Natamani kujua ni kwa muda gani mkishakuwa na mahusiano mwanaume anapaswa kukupeleka nyumbani kwake anapoishi ili upajue

Na je Kuna ubaya wowote kama utamwambia akupeleke nyumbani kwake upajue hata kama mna mwezi mmoja wa mahusiano

Wengine wamekuwa wakidate na watu ambao hawajawai kufahamu muhusika anapoishi

Napenda kujua hili especially kwa wanaume ni kwa muda gani mnapeleka wanawake kwenye hizo ghetto zenu
 
Kuna comment zinachekesha. Kupelekana home inategemea na malengo au anavyokuchukulia.
Kama akiona ni wife material, wiki au mwezi utakaribishwa home. Akiona ni gold digger, hit&run itahusika kwenye maeneo nje ya home.
Inabidi pia kuwa mvumilivu sababu kuna wengine wapo slow kwenye kufanya maamuzi, anaweza kumchukua muda mrefu even mwaka kufikia uamuzi kwamba "yes huyu ndiye". Just chill
 
Kumbe… sasa kwako si nimemaanisha mahali anapoishi mwanaume au wewe umenielewaje hapo
Anyway niseme unaweza kupelekwa hata siku ya kwanza inategemeana na mazingira maana what if kama mmepanga nyumba Moja au mko mtaa mmoja na unapajua kwake si unaweza hata ku "surpriiiiiiiise"
 
Back
Top Bottom