Ni muda gani inapaswa mwanaume akupeleke kwake baada ya kuanza naye mahusiano?

Sisi wanaume tunaogopa sana kuoa asikwambie mtu!nani anapenda ghafula kuwa na familia tatu za kuhudumia!!?yaani familia yake,kwao na kwenu!!?

Ndoa mwanamke ndio anaipigania Hadi kinaeleweka coz muda unaenda na anaing'ang'ania kama anaona huyo Me Ana potential fulani!

Ukisubiri protocol zifatwe utachelewa sana!Kwa usawa huu nani anataka kuoa zaidi ya kucheza game na Sheria ya ndoa ilivyo mbaya!!?
Hiyo sogea tuishi sio ya kumshauri binti mkuu… wanaume wengi huwapotezea muda kwa kuishi nao kama mke na mume akimchoka anaenda kuoa ndoa ya kanisani
 
Kama mnavojua tunakutana tukiwa watu wazima tuliokulia mazingira tofauti..
kabila tofauti mikoa tofauti, hivyo hatujuani wala kufahamiana tunaanzisha tu mahusiano

Natamani kujua ni kwa muda gani mkishakuwa na mahusiano mwanaume anapaswa kukupeleka nyumbani kwake anapoishi ili upajue

Na je Kuna ubaya wowote kama utamwambia akupeleke nyumbani kwake upajue hata kama mna mwezi mmoja wa mahusiano

Wengine wamekuwa wakidate na watu ambao hawajawai kufahamu muhusika anapoishi

Napenda kujua hili especially kwa wanaume ni kwa muda gani mnapeleka wanawake kwenye hizo ghetto zenu
Mwaka mmoja unatosha kupelelezana kila mmoja kumjua mwenzie ila mwanamke usije ukalogwa ukabeba mimba bila makubaliano yenu wawili,utajuta
 
Umepata mwingine Tena?? Ila inaonekana mapenzi unayamudu sana
 
Kama mnavojua tunakutana tukiwa watu wazima tuliokulia mazingira tofauti..
kabila tofauti mikoa tofauti, hivyo hatujuani wala kufahamiana tunaanzisha tu mahusiano

Natamani kujua ni kwa muda gani mkishakuwa na mahusiano mwanaume anapaswa kukupeleka nyumbani kwake anapoishi ili upajue

Na je Kuna ubaya wowote kama utamwambia akupeleke nyumbani kwake upajue hata kama mna mwezi mmoja wa mahusiano

Wengine wamekuwa wakidate na watu ambao hawajawai kufahamu muhusika anapoishi

Napenda kujua hili especially kwa wanaume ni kwa muda gani mnapeleka wanawake kwenye hizo ghetto zenu
mwanaume akikupenda na ana malengo na wewe, atakupeleka tu hata bila kumuomba, ataanza kukusogeza kwa watu wake wa karibu, lakini kama hana malengo na wewe hawezi kukupeleka maana utamharibia kwa yule anayempenda na kumheshimu aliye na malengo naye, akiwa na malengo na wewe hata funguo ya getto unapewa
 
Kama amekuona wewe ni matirio, ata kupeleka ndani ya siku saba; ila kama ameona anapoteza muda na mizinga mingi isiyo na mpangilio baada ya miaka 20 ndio ataweza kukupeleka.
 
Sio wote ndugu wengine mageto yao ni mbadala wa gest anapunguza gharama
 
Kama amekuona wewe ni matirio, ata kupeleka ndani ya siku saba; ila kama ameona anapoteza muda na mizinga mingi isiyo na mpangilio baada ya miaka 20 ndio ataweza kukupeleka.
Na huyu ambae nashinda kwake lakini hanipendi tumuweke wapi
 
Back
Top Bottom