Ni muda muafaka kwa sasa kufunga mipaka janga la njaa linakuja kwa kasi

Ni muda muafaka kwa sasa kufunga mipaka janga la njaa linakuja kwa kasi

Kuna mahala nilikuwa naongea na jamaa anasema sembe kilo 5 imefika elfu tisa kwa hapa Dar, na hii ni July kipindi cha mavuno. Majuzi hapa niliona sabuni ya kuogea ya Protex ambayo nilikuwa nainunua kwa 2500 baadaye 2800 imeshafika 3500. Hii kasi ya kupanda kwa vitu muhimu kwa matumizi ya watu linaenda kuwa janga kubwa sana.
 
Shida ya huku vijana wanakuwa wanafiki kwa kutetea kila kitu hata kiwe kina athari kwa Taifa wanaona ndio ukada na wataonwa kwenye teuzi wakati ni ushamba tu na kuumizana.
 
Gunia la mahindi litanunuliwa 200K ikiwa huyu mama (slow learner) hatapata mtu wa kumsanua.

Yani hii ni july wakati wa mavuno ila vyakula bado ni bei ghali, gunia la mahindi kwasasa ni 120K.
Muda si mrefu tutaanza kuagiza chakula kwa hao tunaowauzia kwa bei mala tatu ya tuliowauzia mana wenzetu huwa wana jicho la mbali. Hawatatuuzia kama mahindi ila tutauziwa unga.
 
Gunia la mahindi litanunuliwa 200K ikiwa huyu mama (slow learner) hatapata mtu wa kumsanua.

Yani hii ni july wakati wa mavuno ila vyakula bado ni bei ghali, gunia la mahindi kwasasa ni 120K.
Tuliopo mtaani karibu kila siku tunamshauri tatizo lipo kwa walioshiba, wafanyabiashara wakubwa na wanasiasa uchwara ambao si waumini wa ukweli hawamshaurii vizuri hali iliyoko mtaani.
 
Kwani mliwasaidia kulima hayo mahindi? waacheni wakulima wauze wanapotaka kwa bei wanayotaka, ukitaka rahisi lima yako

Acha bla blaa uwe unalima.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Mimi silimi ila nanunua mazao, wakulima wanauza mazao kwa fujo na wakenya wamekuja kulangua mazao ya chakula tani kwa tani kwa dau la kutamanisha tofauti na nyuma, kweli wamepata hela Ila wanauza hadi wanasahau kuwa kuna kesho na hali ya hewa haitabiriki.
 
Sasa kwann wakenya waweze kununua kwabei nzuri lakini watanzania washindwe?
 
Mama anaupiga mwingi.
Yeah! Mama anafanya vizuri sana maeneo mengi ni suala la kumpa muda zaidi ila pia akumbuke kwenye janga la Covid hatukutikisika sana mana tulikuwa na akiba ya chakula cha kutosha.
 
Nasikia njaa imehamia kaskazini-mashariki ya Uganda,,, sasa ni Kenya,Somalia,Ethiopia na Uganda,,,Mungu atulinde!
 
Back
Top Bottom