Bora umeliona hilo kiongozi. Huku nilipo, wakenya wanakuja mpaka mashambani kununua mpunga. Hii ni hatari sana. Kwanza wanaua ajira za vijana waliojiajiri kama wanunuzi wa kati yaani antoa mpunga shambani, anakoboa na kupeleka mchele sokoni. Pili wanaua viwanda vyetu. Tatu, hiyo pesa wanayonunulia huku ni ndogo sana kulinganisha na faida wanayoenda kupata huko kwao. Nne, wanabeba hadi pumba ambazo huku kwetu tunalishia mifugo na pia tunachomea tofali. Kwa kifupi, bila kufunga mipaka taifa litapigwa technical KO.