Ni muda muafaka kwa sasa kufunga mipaka janga la njaa linakuja kwa kasi

Ni muda muafaka kwa sasa kufunga mipaka janga la njaa linakuja kwa kasi

Mtalalamika mpaka kiyama na mtaenda mbinguni mmechoka sana kwa ujinga Halafu na adhabu ya Umasikini inawasubiri

Inakuwaje mna mito yote hiyo na maziwa mengi lakini hamyatumii kwa kilimo cha Umwagiliaji?

Kesho ukiulizwa kwa nini unakufa njaa na mnapigana wakati mna maji yote Haya mtajibu nini ?
Eti msisogee mita sijui ngapi karibu na mto
Kwa hiyo ni Mito ya maonyesho ama
Kama wataharibu Kwanini wasipewe Elimu kuhusu kulinda mali zetu ?

Kuna nchi za Afrika wana Mito kama Sisi ila wanatumia haswa kwa kilimo na hata usafiri kwenye Mito huku wengine wakiwa wamejenga mpaka makazi pembezoni mwa mito na wanalima mboga mboga na kuiuza huku wakiibeba kwenye mitumbwi

Sisi tumekalia maneno na kujifungia hapo tu
 
Gunia la mahindi litanunuliwa 200K ikiwa huyu mama (slow learner) hatapata mtu wa kumsanua.

Yani hii ni july wakati wa mavuno ila vyakula bado ni bei ghali, gunia la mahindi kwasasa ni 120K.

Haya ni madhara ya covid-19 na Vita ya Ukraine.
 
Ulishaona nchi gani ambayo kila mtu ni mkulima, lazima serikali iweke control kwenye kila eneo vinginevyo katafute nchi yako utakayojifanyia mambo unavyotaka.

Kwa hiyo inamaana wakulima kulima hayo mahindi kuna sheria iliwekwa wawalimie mnaotaka kununua kwa bei chee?
 
Fresh tu haunikomoi mimi mana Mimi na wewe tumeshiba hadi tumejisahau kuwa wazalendo, kizazi chetu hiki kimejaa ubinafsi tutaua taifa kwa upumbavu. Utampelekeaje chakula jirani yako ili umfurahishe wakati nyumbani kwako watu wanalia njaa. Unachokitafuta ni nini?

Kwa nini mkulima pangiwe kwa kuuza na wa kumuuzia? Nani alimsaidia kwenye kulima hayo mahindi mkulima?
 
Bado tunazungumzia suala lile lile mana nikishindana na mkenya nami nitanunua kwa Bei ya juu nikiuza kwenye soko la ndani bado nitauza kwa bei ya juu na kuwaumiza wengine.

Hao wa kuumizwa kwa nini hawalimi wao wenyewe ili wasiwe wanaumizwa?
 
Vichwa Maji wa Lumumba hawawezi kukuelewa.

Njaa inayokuja, tutatafutana sana ,waacha waendelee kufungua nchi .


Watatafutana wavivu, wachapakazi hawawezi kutafutana huu ujanja ujanja wa kuwa watu wanapanda mgongo wa mkulima inatakiwa ufike mwisho
 
Watatafutana wavivu, wachapakazi hawawezi kutafutana huu ujanja ujanja wa kuwa watu wanapanda mgongo wa mkulima inatakiwa ufike mwisho
Labda kama unaongea haya UKIWA Nyumban kwenu Kwa Baba yako na Mama yako .


unajua Gunia la mahindi ni shingaoi Sasa ??

Uchape Kazi, alafu Pesa unayoipata haiendani na Inflation ??
 
Labda kama unaongea haya UKIWA Nyumban kwenu Kwa Baba yako na Mama yako .


unajua Gunia la mahindi ni shingaoi Sasa ??

Uchape Kazi, alafu Pesa unayoipata haiendani na Inflation ??


Kama mtu huwezi bei ikipanda ya mahindi kwa nini usilime upate hayo ya bei chee? Apangiwe bei mkulima nani alimsaidia kulima hayo mahindi mpaka bei iingiliwe? Mbona watanzania wengi ni wakulima na tena zao hilo hilo la mahindi ndio wengi
 
Wakati Mbolea na pembejeo ipo juu mlikuwa mnajitoa akili na kuwaona wakulima kama hawana maana yoyote sio.Waacheni wauze kwa Bei nzuri Mkitaka kuepusha njaa wewe na familia yako nunueni chakula kwa bei iliyopo sokoni Muhifadhi mapema..

Binafsi naipongeza Serikali kwa kutofunga mipaka na kuendelea kuwasaidia nchi jirani dhidi ya janga la njaa[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
Si ndio hapo , hawaangaliii hata jinsi mkulima anavyopigika , mbolea na pembejeo BEI juu
 
Sawa, ila ni kwanini na wewe hukua miongoni mwa waliolima
Ili uepukane na njaa? Yaani wenzako wapigike na jua kali mashambani, wewe ukae mjini unajipodoa na kupuliza pafyumu halafu naada ya mavuno ndio uanze kulia njaa?
Mbona huyo mkulima ananunua mbolea, dawa za viatilifu, sabuni, mafuta ya taa.......hivyo vyote na vyenyewe analima kwenye shamba lake? akiuziwa bei juu atafurahi kipindi ambacho hana hata debe la akiba.
 
Back
Top Bottom