Ni muda muafaka sasa TRA mtoke hadharani mtuambie hayo mabango yenye picha ya Rais nchi nzima nani anayalipia na yanaingiza kiasi gani

Samahani, nimeshindwa kuelewa mkuu 'Mr mutuu'!

Ulikuwa na "kakibanda" uchochoroni. Hapa nimeelewa kuwa ulikuwa na kibiashara chako.

"TRA wakakupigia hesabu laki 3 kwa mwaka"- nimeelewa kwamba hiyo laki tatu ilikuwa kodi uliyopaswa kulipia hiyo biashara yako kwa mwaka.

"ikabidi nilitoe lile bango" - hapa ndipo nilipochanganyikiwa hasa. Hilo bango ndilo TRA walilolikadiria laki 3 kwa mwaka?

Mwisho. Nani aliyekuwekea/kupa hilo bango; na ulipoliondoa uliliwasilisha wapi?
 
Kwa hiyo mabango ya rais yanalipiwa, na nani na kwa kiasi gani. Hii pesa inatoka mfuko gani?
 
Kodi ni ya bango tu, achilia mbali biashara, wanapima size ya bango kwa upana na urefu afu wanakupa makadirio
 
Mabango ya kuzuga tu lakini wamepanga kuiba Kura.
 
Rostam Azizi kasambaza haya mabango
 
Kodi ni ya bango tu, achilia mbali biashara, wanapima size ya bango kwa upana na urefu afu wanakupa makadirio
Ahsante. Sasa nime elewa.
Ila nina swali, kwa vile sina uzoefu kabisa na maswala ya aina hii.
Unapo pewa bango, na kuliweka hapo mahala pako, unapewa chochote kuhusiana na bango hilo; au ni kama kivutio tu cha biashara yako; au kuunga mkono/shabiki tu wa huyo mwenye bango lake?
Siyo muhimu ujibu hili kama linakupotezea muda. Sehemu muhimu ni hiyo uliyo nipa elimu juu yake hapo juu.
 
Bango hupewi, unaweka mwenyewe kujulisha watu uwepo wa Hio biashara yako
 
Zaidi watakuambia ni maagizo toka juu.Baadhi ya nchi za Kiafrika na Asia ni Sawa na sehemu za kutolea haja kubwa,kauli hii ya Donald Trump ipo Sawa Sawa kabisa.
 
Watanzania tushakua kama makondoo, mtu nauliza swali basic tu mtu anajibu uchochezi, tumerudi enzi za utumwa sasa huku tukitawaliwa na weusi wenzetu
Baada ya mataifa mengi ya kiafrika kupata uhuru miaka 1960s,Mengi yalijikuta yameingia kwenye utumwa mpya,tena mbaya zaidi kuliko ule wa wakoloni.
 
Mkuki kwa nguruwe ee. Mbona jpm alisambaza mabango nchi nzima kwama yeye ndo rais aliyetumw na mungu. Unajua tanzania kwa mara ya kwanza tuliishi na shetani bila kujua
 
Mkuki kwa nguruwe ee. Mbona jpm alisambaza mabango nchi nzima kwama yeye ndo rais aliyetumw na mungu. Unajua tanzania kwa mara ya kwanza tuliishi na shetani bila kujua
Jpm nae alipokua anakosea tulihoji vile vile, kwa kua jpm aliharibu basi tumuache na huyu aharibu? Akija mwingine nae vile vile?
 
Kuna jamaa ana bango aliliweka kama week hivi hao wakaja, hesabu waliyompigia alilitoa hapo hapo.
 
Main road huwezi kutoboa, mi kwangu vichochoroni tu nilipigwa laki 3
Ni main road jamaa alisema potelea pote asipouza basi ila hawezi toa hela yote hiyo kulipia bango heri aijazie hadi bidhaa πŸ˜ƒ
 
Ni main road jamaa alisema potelea pote asipouza basi ila hawezi toa hela yote hiyo kulipia bango heri aijazie hadi bidhaa πŸ˜ƒ
Main road bango likiwa kubwa kidogo tu tunaongelea millions sio malaki tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…