Ni muda sasa sijawahi kumbuka ndoto yoyote niliyoota

Ni muda sasa sijawahi kumbuka ndoto yoyote niliyoota

Bob Manson

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
4,158
Reaction score
7,787
Habari za asubuhi wadau

Kama kichwa cha habari kinavyo sema. Nina uhakika kila siku naota ndoto nikiwa usingizini, lakini cha ajabu ni kwamba nikiamka tu asubuhi sikumbuki ndoto hata moja.

Ni muda mrefu sina kumbukumbu ya ndoto yoyote ile, naota ndoto zaidi ya tatu lakini asubuhi ifikapo nikijaribu kukumbuka nashindwa.

Hili ni tatizo au ni hali ya kawaida tu? Ni zaidi ya miaka mitatu sasa nimekuwa na hali hii. Nifanye nini?

#BM
 
Last week kwa siku 2 mfululizo, nimeota niko mahala ,nina huzuni sana , nafanya maombi huku nalia kwa uchungu sana, nikashtuka ndotoni,ilikua saa 8 usiku, macho yamejaa machozi,moyo wangu mzito sana. Siku 2 mfululizo ndoto hii ya aina moja.
SIjui hii ina maana gani et Rabboni ?
 
Habari za asubuhi wadau

Kama kichwa cha habari kinavyo sema. Nina uhakika kila siku naota ndoto nikiwa usingizini, lakini cha ajabu ni kwamba nikiamka tu asubuhi sikumbuki ndoto hata moja.

Ni muda mrefu sina kumbukumbu ya ndoto yoyote ile, naota ndoto zaidi ya tatu lakini asubuhi ifikapo nikijaribu kukumbuka nashindwa.

Hili ni tatizo au ni hali ya kawaida tu? Ni zaidi ya miaka mitatu sasa nimekuwa na hali hii. Nifanye nini?
Unavuta bangi?? Maana nazo zinakataga uwezo wa kuota
 
Ndoto nyingi ni yale mambo unayoishi nayo kila wakati. Japo wengi wanazichukulia serious,lakini hata pale wanapozichukulia serious kwamba alichokiota kitatokea,hiyo inakuwa nadharia tu wakati hakitokei hata nusu yake,japo InabaKi kwenye Imani ya mhusika kwamba itatokea,mpaka anasahau kwamba imetokea au haijatokea.

Ukitaka kuikumbuka ndoto uliyoota ni rahisi tu ni kama vile unavyostuka mkojo ukikubana,basi unaweza kujitafuta kila wakati ukiota jilazimishe kuamka. Ukiweza kuamka kila wakati,usiamke kwa kama unastuka. Amka soft tu anza kuwaza ulivyokuwa usingizini ilazimishe akili ivute kumbukumbuku ndoto yako. Anza na tukio kubwa kubwa lililojirudia rudia kwenye ndoto yako. Mwisho utaweza kukumbuka ndoto zako. Japo sio muhimu. Mimi huwa nikiota ndoto mbaya najilazimisha sana niamke hata katikati ya ndoto. Ukija kulala huwezi kuota tena ile ile ndoto.
 
Back
Top Bottom