Ni muda sasa wa kumsikiliza Komando Mashimo alichosema kuhusu Simba na Yanga

Ni muda sasa wa kumsikiliza Komando Mashimo alichosema kuhusu Simba na Yanga

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
Kipigo cha tatu bila kwa timu ya Simba kimenifanya niiangalie tena video ya Mchungaji Komando Mashimo kwa sasa anayejiita Nabii Mikaya aliyemuomba Rais Samia awalipie deni Simba na Yanga ili waweze kushinda katika michuano ya CAF. Nabii Mashimo alisema mwaka 2022 Mungu alitenda kwa ajili ya simba na yanga lakini hawakumtolea Mungu walichoahidi ambacho ni kiasi cha Tsh milioni ishirini,Nabii Mikaya aliomba sadaka hiyo ilipwe kufuta makosa ambayo Simba na Yanga waliyofanya mbele ya Mungu,wasipotoa sadaka hiyo hawataweza kushinda kwenye michuano ya CAF.

Nabii Mikaya ni jina lenye unabii mkubwa kwenye biblia,kama Mchungaji Comando Mashimo ameanza kutembea katika njia za Nabii Mikaya basi akisemacho kina nguvu sana kama lile neno la Nabii Mikaya alilolisema kwa Ahabu Mfalme wa Judah, Nabii Mikaya alimwambia Mfalme Ahabu kwamba atapigwa vitani, Mfalme akawaambia askari mtieni jela nikirudi nitamtoa, Nabii Mikaya alimwambia hautarudi, tuliona mwisho wake,timu ya Raja Casablanca wameandika katika ukurasa wao "Simba kafungwa sio mfalme tena katika mbuga ya Serengeti, wao wenye alama ya tai ndio mfalme mpya". Sasa leo wacha nisimulie neno la Mungu (Biblia) katika kuelezea haya yanayotokea katika soka la Tanzania, hususan kuvurunda kwa vilabu vyetu Simba na Yanga a Taifa Stars kwa ujumla katika mashindano mbalimbali.

Wakati wa Utawala wa Ahabu mwana wa Omri,Israel walikuwa wamekaa miaka mitatu bila kupigana na Shamu (ambayo ndiyo Syria ya sasa), lakini katika mwaka wa tatu,Yehoshafati mfalme wa Yuda alikwenda kumtembelea Ahabu kule Yerusalemu, Ahabu akatamani kupigana na Shamu ili aurejeshe mji wa Ramothi-gileadi ambao ulikuwa umetwaliwa na akamuomba Yehoshafati amsaidie katika vita vile, ambaye alikubali, hata hivyo,Yehoshafati akaema, “Tafadhali, kwanza kabisa uliza Neno la Yehova.” Hii ilikuwa kawaida ili kujua kama Bwana alikuwa radhi wakapigane na watashinda au la.

Mfalme Ahabu akawauliza manabii wake mia nne kama ilikuwa sahihi kwenda kupigana, ambapo wote, wakiongozwa na Zedekia mwana wa Kenaana, wakasema akwee kwa sababu angeutwaa mji huo,pamoja na utabiri huo wa manabii mia nne, lakini bado Yehoshafati mfalme wa Yuda hakuridhika, akamuuliza Mfalme Ahabu; “Je, hayupo hapa tena nabii wa Yehova? Basi na tuulize kupitia yeye.”lakini Ahabu akasema: “Bado kuna mtu mmoja ambaye tunaweza kumuuliza Yehova kupitia yeye; lakini hakika mimi ninamchukia, kwa maana yeye hatoi unabii wa mambo mema kunihusu mimi, ila mabaya—Mikaya mwana wa Imla.”hata hivyo, Yehoshafati akasema ni vyema akaitwa naye, hivyo Mikaya akafika mbele ya wafalme hao wawili ilia toe unabii wake, Mjumbe aliyetumwa kwa Mikaya akamuonya kwamba manabii wote wametabiri mema, hivyo naye akienda asije akatabiri mabaya.

Mikaya akamwambia atasema maneno ambayo Mungu atamwambia na siyo vinginevyo, alipoingia, Mfalme Ahabu akamuuliza: “Mikaya, je, twende kupiga vita juu ya Ramothi-gileadi, au tujiepushe?” Lakini moja Mikaya akajibu: “Panda uende na kufanikiwa; na Yehova atakutia mkononi mwa mfalme wa Shamu.”kauli ile ikamkasirisha Ahabu ambaye alisema: “Ninakuapisha mara ngapi kwamba usiniambie jambo lolote ila kweli katika jina la Yehova?” Ndipo Mikaya akasema: “Hakika ninawaona Israel wote wametawanyika juu ya milima, kama kondoo wasio na mchungaji. Na Yehova akasema: ‘Hawa hawana mabwana. Kila mmoja na arudi kwa amani nyumbani kwake.’”Ahabu akafura kwa hasira na kumwambia Yehoshafati: “Je, sikukuambia, ‘Hatatoa unabii wa mambo mema kunihusu, ila tu mabaya’?”

Sasa basi tumeona kipigo cha goli tatu bila walichokipata Simba,na leo saa moja, Yanga itacheza na T.P Mazembe,siku ya jana basi la Simba liliingia kinyume nyume lakini Simba ikala 3 baada ya kuingia kwa makalio kama wangeingia mbele wangekula sita, Waganga wamesaidia kupunguza idadi ya magoli lakini tumefungwa na point tatu tumezipoteza, waganga sio watu wa kuwaamini, timu iliondoka toka saa saba mchana kwenda Uwanja wa Mkapa Stadium wameenda na basi kinyume nyume hadi uwanjani bado tukafungwa tatu naamini game ingekuwa saa kumi Simba wangeshinda, maana mwarabu sio mzuri kwenye joto kali tatizo muda wanapanga caf sio team mwenyeji, mganga akafeli hapo,ni wakati sasa wa kumsikiliza Mchungaji Comando Mashimo a.k.a Nabii Mikaya.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management

Recent Publications;-
-Assessment on the effect of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Hyo ahadi ya Simba na Yanga ya million 20 walitoa wapi na lini, huyo nabii aache siasa na utapeli, alaf muache kumfananisha Nabii mikaya na vtu vya ajabu ajabu!
 
[emoji848] Hayo ya huyo mchungaji mbona kama yalinipita? Mkuu naweza kupata hiyo link nikashuhudie.
 
Nabii Mashimo alisema mwaka 2022 Mungu alitenda kwa ajili ya simba na yanga lakini hawakumtolea Mungu walichoahidi ambacho ni kiasi cha Tsh milioni ishirini,Nabii Mikaya aliomba sadaka hiyo ilipwe kufuta makosa ambayo Simba na Yanga waliyofanya mbele ya Mungu, wasipotoa sadaka hiyo hawataweza kushinda kwenye michuano ya CAF.
Huyo naye ni tapeli ana shida na pesa, kamwe sadaka huwa haidaiwi, inakuja yenyewe kwa mtoaji kuwiwa na jambo alilofanyiwa na Mungu, na wala Mungu hana malipizi na wala hahitaji kupewa ili atoe
 
timu iliondoka toka saa saba mchana kwenda Uwanja wa Mkapa Stadium wameenda na basi kinyume nyume hadi uwanjani bado tukafungwa

naamini game ingekuwa saa kumi Simba wangeshinda,maana mwarabu sio mzuri kwenye joto kali tatizo muda wanapanga caf sio team mwenyeji,
Uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa Simba ulizidiwa kwa mbaali saana na wa Raja.

Team work, Raja walikuwa bora mara 1000 zaidi ya Simba.

Accuracy, Raja wametisha!

Miaka nenda rudi wanacheza hii michuano kwenye mazingira yale yale yanayojirudia, nini kikusababishe udhani hali ya hewa inaweza kuwa chagizo la wao kufeli ilihali kimchezo wako vizuri?
Nabii Mashimo alisema mwaka 2022 Mungu alitenda kwa ajili ya simba na yanga lakini hawakumtolea Mungu walichoahidi ambacho ni kiasi cha Tsh milioni ishirini,
Hata kama ni kweli waliahidi hivyo, huyoo jamaa anataka apewe yeye hizo 20m * 2 kama nani, Mungu? Angeshauri hata kuwavika walio uchi, kuwalisha wenye njaa n.k sio kusema raisi awalipie, kwa nani sasa?

Mwisho, ni ujuha na upumbavu mkubwa kuendelea kuamini kuwa tunguli zinacheza uwanjani....na kama hivyo ndivyo, basi tusipeleke timu kabisa uwanjani tushindanapo na hao WEUPE kwa kuwa mpaka kwenye ULOZI wametuzidi.

Una risk maisha ya timu nzima kwa kuendesha backward only to achieve 0-3 at Home.
 
Back
Top Bottom