Uchafu mbona popote upo? Huwezi kulinganisha India na nchi yoyote ya Afrika. Wamechangia na wako mbali katika nyanja zote iwe sayansi, jamii, uchumi n.k. Wataalamu Wahindi wanatafutwa dunia nzima angalia huko US walivyo kamata sekta mbali mbali
Kwa suala la elimu wanapambana haswa na wako mbali sana hata jengo ghali la Mukesh Ambani lenye gharama ya $2b wanalo
Wao nawapalilia kwa uhodari wa biashara na hata elimu ila uchafu omba siku moja ukatembee huko
Nimeenda sehemu kadhaa India napajua vizuri tu
Wana Maharaja express ni kama Oriental express ya ulaya ila babu kubwa
Hawa wakiona kitu kizuri lazima wapambane waweke
Hiyo Maharaja ni ghali na ya kitalii ukipanda unajisikia sijui uko wapi kwa huduma zao na jinsi ilivyo
Wamefanikisha mambo mengi sana sikatai ila kama ukipita mitaa ya Mumbai ni balaa
Kuna miji mizuri na misafi ila sio mji mkuu na wa pili
Modi aliposhika madaraka akaanza na usafi kama Magu
Ila haikuchukua mda akaachana nayo kwa sababu wahindi walisema tumezaliwa kwenye uchafu vigumu kubadilika mara moja
Natamani na sisi tuwe na hamu ya maendeleo kama wao
Hata tuweke train moja inayozunguka hata nchi nne kwa nauli za kitalii luxury trains ambazo duniani zipo nyingi
Ila hapa tunaongelea uchafu na haya nimeongeza kwa kuwapa credit kwa uwezo wao mwingine maana wanajua maisha