Ni muda wa kuambiana ukweli. Sisi watu weusi hapa duniani tatizo letu ni nini?

Aiseeh changamoto
 
Tatizo ni fikra za kitumwa kwa walio wengi. Nguvu, akili na elimu za kujisogeza kwa kiwango kinachoeleweka zipo.
Hata hivyo, fikra za kitumwa (kuamini na kutegemea wageni), ndilo tatizo la msingi walilo nalo viongozi na wananchi.
Fikra hizo, hasa kwa viongozi, zikiunganika na ubinafsi unaozalisha rushwa, ni balaa kubwa.
Kama hatua za haraka hazitachukuliwa kwa kufanya mapinduzi ya fikra kivitendo (viongozi wachache wanaojielewa na pia wana usalama wanahusika sana hapa), utumwa wa kiuchumi utafikia kiwango kisichovumilika kwa wanaojielewa.
Vizazi vijavyo vitahitaji kujikomboa na watapata ugumu hata baada ya kumwaga damu.
Adui mkubwa wa mwafrika yupo ndani, ni yeye mwenyewe au mwenzake mwenye fikra mbaya za kitumwa.
 
Mtu ni Roho, anayo NAFSI na anaishi ndani ya MWILI.

Mtu Hana RANGI, RANGI Iko kwenye Mwili,

Ingekuwa RANGI ni tatizo, mzungu asingewekewa Damu ya black na kusurvive.

Tatua matatizo Yako, usisingizie RANGI Yako au uafrika wako.
Sawa
 
😅 sasa jibu swali Mondi wako naye ni mjinga?
Unashangaa akili za wafrica wakati umezamia utumwani kuuza sehemu zako kwa wazungu ili ule burger na kupita kwenye mabarabara mazuri watu waloumiza kichwa kuyaplan na kujenga
 
Unashangaa akili za wafrica wakati umezamia utumwani kuuza sehemu zako kwa wazungu ili ule burger na kupita kwenye mabarabara mazuri watu waloumiza kichwa kuyaplan na kujenga

Chief, wazungu walinifukuza nipo zangu Chitipa huku nalima bilimbi.

Naona unakwepa kweli kumuweka bwana'ako Mondi kwenye kundi la waafrika wajinga, akiona kibarua kinaota nyasi 😅 😅
 
Watu weusi dunia kote tuna fanana kwa mambo mengi sana tena mengi ya hovyo
 
Hivyo tatizo letu ni ubinafsi uliopindukia kabisa kuzidi wengine wote
 
Tatizo tuna roho mbaya sana na tamaa za muda mfupi ,wavivu,wabaguzi,wavivu,tunaenda kitonga,wenye wivu na husuda,hatupendi mtu kufanikiwa na ulifanikiwa hupendi mwingine atoboea tunapenda kusifiwa
 
TATIZO NI VIONGOZI WETU.
Maoni yangu: kila raia aruhusiwe kumiriki bunduki ya aina yoyote apendayo bila mashart lazima tutasonga mbele, kwani viongozi hawatategemea kutumia vyombo vya usalama kufanya watakavyo bali watatumia akili kuleta maendeleo ili waendelee kubaki madarakani.
 
Lakini mbona matatizo yetu watu weusi yana fanana katika maeneo mbalimbali hata nje ya Tz au hizo factors ulizo zitaja zina husika napo huko nje ya Tz ?
 
Umuhimu kwa kina nani? Sisi ni watu muhimu sana kwenye hii dunia kwa familia zetu. Sijui wewe lakini iwapo huna umuhimu i sawa.
 
Basi tunazidi kujichimbia kaburi wenyewe huko tuendako sioni kama hata dalili ya kubadilika
 
Imebidi nicheke tu🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…