Sab-Sahara Africa hatuna maarifa, na hatujawahi kuwa na maarifa ndio maana hatujawahi kuwa competitive wala kutoboa kimaendeleo. Hii inaanzia kwa level ya individual, community, state hadi Bara.
Ili uweze kuendelea inahitaji uzalishe au utengeneze kipato kitakachokuwezesha umudu mahitaji yako ya msingi (acceptable standard of living). Ili uweze kuwa mbele zaidi ya wenzio kimaendeleo unapaswa kuzalisha au kutengeza kipato kitakachokuwezesha kuwa na ziada.
Yote hayo yanahitaji maarifa. Maarifa yatakufanya ufanye maamuzi sahihi katika kuzalisha idea (wazo+vision) sahihi katika wakati sahihi na kubuni mikakati, mbinu na sera sahihi katika muda sahihi. Vilevile, maarifa yanakuwezesha kubuni implementation measures stahili na sastainable. Maarifa yanakupa uwezo wa kujikosoa na kufanya reform katika muda sahihi kwa quality stahili. Kadhalika, maarifa yanakuwezesha kufanya maamuzi sahihi kuhusu serving kwa dhamira ya kupata capital, investing and re-investing.
Hayo yote niliyobainisha yanahitaji mtu/community/ Taasisi au serikali kuwa na uwezo wa kufanya utafiti katika muda sahihi na kiwango stahili.
Kwa bahati mbaya sana Waafrica katika ngazi ya individual, taasisi hadi Serikali hatuamini katika utafiti, information na knowledge, matokeo yake huwa tunafanya maamuzi kwa kubahatisha, kuiga, opinio, matamanio binafsi, porojo na utashi binafsi. Kwa mtazamo wangu Hii ndio root-cause of African feilure in every aspect of human develpment. Tunafeli sana katika maamuzi kuhusu sera, mikakati, mipango na miradi mingi ya maendeo. Kuna individual na instutional feilure ya kutisha sub sahara Africa na wala hatujari.
wenzetu walio mbele huwa hawataki kubahatisha na wanaogopa sana kushindwa ndio maana huwa hawafanyi maamuzi based opinion, matamanio au utashi binafsi wa mtu au kiongozi. Wanaamini katika maarifa, utafiti, information na fact. Kama wanaona wana upungufu wa maarifa huwa na utayari wa kuyasaka na ikiwezekana kununua knowledge kutoka eneo lolote la Dunia. Wafrika wengi wenye knowledge adimu wamenunuliwa na hawa wakubwa. US, China na Western Europe ni miongoni mwa mataifa yenye njaa ya maarifa.